Hivi karibuni amirijeshi mpya wa jeshi la Marekani lililopo nchini Iraq Bw. David Petraeus alitumwa huko Iraq kuwa amirijeshi wa awamu ya tatu. Kwenye sherehe ya kushika madaraka iliyofanyika kwenye kituo cha jeshi la Marekani mjini Baghdad alisema, ataongoza jeshi lake kwa mkakati mpya, mbinu mpya za kivita na fikra mpya, na kujitahidi kutumia "fursa" ili kubadilisha hali ya kisiasa nchini Iraq. Lakini watu wana wasiwasi kama amirijeshi huyo ataweza kutimiza ahadi zake.
Bw. David Petraeus ana umri wa miaka 54, aliwahi kuwa mkuu wa divisheni 101 ya jeshi la Marekani na aliwahi kushiriki katika kuupindua utawala wa Saddam mwaka 2003, baadaye aliwahi kuwa mkuu wa kuwafundisha askari wa Iraq, na aliwahi kushirikiana na viongozi wa mji wa Mosul uliopo kaskazini mwa Iraq kuboresha hali ya mji huo. Tofauti na amirijeshi aliyemtangulia Bw. George Cacey ni kuwa, yeye anatilia mkazo zaidi ushirikiano kati ya jeshi la Marekani na jeshi la Iraq "kubeba majukumu kwa pamoja". Anaona kuwa majukumu hayo yatakuwa makubwa kupita kiasi kama upande mmoja tu utayabeba.
Katika siku hiyo alipoanza kuwajibika alisema, atatekeleza mkakati mpya na mbinu mpya za kivita. Wachambuzi wanasema, mkakati na mbinu mpya hizo zikiwa ni pamoja na raia wote wa Iraq kuwa na vitambulisho vyenye maelezo binafsi, kubadilisha hali ambayo baada ya jeshi la Marekani kutuliza vurugu kwenye sehemu fulani na kuziacha sehemu hizo, kujenga vituo vingi zaidi kwenye sehemu zenye migogoro ya madhehebu ya dini, kuanzisha ushirikiano wa kudumu na makazi ya raia na kufanya doria. Kwa hiyo Baghdad itagawanyika katika mitaa tisa na kuanzisha kiasi cha vituo 30 vya polisi na askari wa usalama wa Iraq na jeshi la Marekani.
Lakini wachambuzi wanaona kuwa hata kama mkakati na mbinu za kivita zitabadilika namna gani, hazitaweza kubadilisha chanzo cha vurugu, na haziwezi kutatua matatizo ya kisiasa yenye utatanishi. Bw. David Petraeus atakabiliwa na changamoto za aina tatu.
Kwanza, kushughulikia uhusiano kati ya madhehebu ya Suni na Shia ni tatizo gumu. Ingawa serikali ya Iraq inayoongozwa na Bw. Nouri al-Maliki iliwahi kuahidi kuchukua hatua kali kupambana na vikosi vya Suni na Shia, lakini inahitilafiana na Marekani kwamba nani achukuliwe hatua kwanza na kwa haraka. Marekani siku zote inaishutumu serikali ya Iraq kwa kutochukua hatua zinazofaa dhidi ya vikosi vya Shia likiwemo jeshi la Mahdi, na madhehebu ya Shia yanataka Marekani ipambane na vikosi vya Suni, wakati inapopambana na Al-Qaida. Ni wazi kwamba namna ya kuushughulikia uhusiano kati ya madhehebu ya dini nchini Iraq kunahusiana na mwelekeo wa kisiasa nchini Iraq, lakini suala hilo ni tofauti kabisa na mambo ya kijeshi.
Pili, hata Marekani na Iraq zikiongeza idadi ya askari kwa kiasi gani na kutekeleza utaratibu wa vitambulisho vyenye maelezo binafsi, vyote hivyo haviwezi kukomesha upinzani na wala kupunguza kutokea kwa mashambulizi. Katika miaka kadhaa iliyopita, majeshi ya Marekani na Iraq yalitumia kila hatua inayowezekana lakini mashambulizi yanaendelea kutokea, na majeshi hayo yanashindwa kuzuia mashambulizi.
Tatu, katika miaka minne ya vita nchini Iraq, idadi ya watu wanaopinga serikali ya rais George Bush inazidi kuongezeka kutokana na vifo vya askari wa Marekani kuwa zaidi ya 3100 na gharama kubwa kiasi cha dola za Kimarekani bilioni mia kadhaa. Uchunguzi wa maoni ya raia uliofanyika hivi karibuni nchini Marekani unaonesha kuwa, uungaji mkono kwa rais George Bush umepungua hadi kufikia 30% mwezi Januari mwaka huu kutoka 83% mwaka 2002. hali hiyo inaonesha kuwa sera za Marekani kuhusu Iraq zimepoteza uungawaji mkono na watu wa Marekani. Katika hali ambayo serikali ya Marekani imepoteza uungawaji mkono na watu wa Marekani, hata kama Bw. David Petraeus ana uwezo mkubwa kiasi gani, hawezi kutuliza vurugu za Iraq.
Idhaa ya kiswahili 2007-02-12
|