Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-13 16:23:01    
Athari ya kampuni za China yaanza kuonekana katika biashara ya mali-ghafi duniani

cri

Siku chache zilizopita kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Baoshan, ambayo inachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa miongoni mwa kampuni za chuma na chuma cha pua nchini China, ilimaliza mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa wa mawe ya madini ya chuma duniani, ambapo kilithibitishwa kiwango cha bei ya mawe ya madini ya chuma ya mwaka 2007, hii ni mara ya kwanza kwa kampuni za China kupata haki ya kupanga kiwango cha bei katika biashara kubwa ya malighafi duniani. Wataalamu walisema athari ya kampuni za China imeanza kuonekana katika biashara ya malighafi duniani, lakini hata hivyo hii haimaanishi kuwa kuanzia hapo kampuni hizo zimepata nafasi ya udhibiti.

Katika biashara ya mali-ghafi duniani, si ajabu kuona migongano mikali kwenye mazungumzo kati ya wauzaji na wateja. Tukichukulia mfano wa biashara ya mawe ya madini ya chuma, ambayo kampuni ya CVRD ya Brazil pamoja na kampuni za BHP Billiton na Hamersley za Australia zimekuwa zikichukua nafasi ya kupanga bei ya mawe ya chuma, na kampuni za chuma cha pua za nchi mbalimbali hazina la kufanya ila tu kufanya mazungumzo nazo kuhusu bei ya mawe ya madini, ambapo bei iliyoafikiana inaitwa kuwa bei ya nafasi ya kwanza, na kampuni nyingine hazina budi kuifuata. Bw. Xu Xiangchun ambaye ni mtaalamu wa taasisi ya utafiti wa habari kuhusu chuma cha pua ya Lange iliyoko mjini Beijing alisema, kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Baoshan ikiwa ni mwakilishi wa kampuni za chuma cha pua za China ilipata nafasi ya mazungumzo ya kupanga bei ya mawe ya madini ya Chuma, jambo ambalo linaonesha kuwa uwezo wa China wa kupanga bei katika biashara kubwa ya malighafi duniani kwenye soko la kimataifa umethibitishwa.

"Katika mazungumzo hayo, kampuni ya chuma cha pua cha Baoshan ilichukua nafasi ya kupanga bei, hatua ambayo inaonesha kuinuka kwa uwezo na kujiamini kwa kampuni za China kwenye mazungumzo ya bei ya mawe ya madini ya chuma duniani, na ni mafanikio makubwa kwa China kupata nafasi ya kupanga bei ya bidhaa katika biashara kubwa."

China ikiwa nchi inayochukua nafasi ya kwanza duniani kwa wingi wa mawe ya madini ya chuma yaliyoagizwa kutoka nchi za nje na uzalishaji wa chuma cha pua, ilipata nafasi ya kushiriki kwenye mazungumzo kuhusu bei ya mawe ya madini ya chuma duniani hadi mwaka 2004. Lakini sauti ya kampuni za China ilikuwa ndogo sana hata kama kampuni hizo zilichukua nafasi ya kwanza kwa wingi wa mawe ya madini ya chuma yaliyoagizwa. Katika mazungumzo kuhusu bei ya mawe ya madini ya chuma ya msimu wa mwaka 2005 na mwaka 2006, kampuni za China zililazimika kukubali kiwango cha kupanda bei kwa 71.5% na 19%. Kuhusu nafasi ya uwekaji bei za aina nyingine za mali-ghafi, hali za kampuni za China zinafanana na hiyo. Tokea mwaka 2004, kutokana na kuathiriwa na kupanda kwa bei za malighafi, gharama nyingi zaidi iliyolipa China kuhusu mali-ghafi zilizoagizwa zikiwemo mafuta ya asili ya petroli, petroli, vifaa vya chuma cha pua, maharage na plastiki ni zaidi ya dola za kimarekani bilioni 25 kwa mwaka, hali ambayo imeongeza hatari katika uendeshaji shughuli za kiuchumi na gharama za kampuni na viwanda vya China. Bw. Xu Xiangchun alisema mafanikio iliyoyapata kampuni ya China katika mazungumzo ya kuhusu bei ya mawe ya madini ya chuma, yamezipatia nafasi yenye haki kampuni za China kushiriki kwenye upangaji wa bei za biashara kubwa ya malighafi katika siku za baadaye, kwa upande mwingine imezifanya ziwe na uzoefu mzuri kuhusu mbinu kwenye mazungumzo na kutumia fursa nzuri ya kupanga bei.

"Kuwania nafasi ya kupanga bei ya malighafi ni jambo muhimu sana kwa kampuni za China kulinda maslahi yake, maendeleo ya uchumi wa China na kuungana na uchumi wa dunia."

Kampuni za chuma cha pua za China kupata nafasi ya kupanga bei kwenye mazungumzo kuhusu mawe ya madini ya chuma duniani, inachukuliwa na sekta ya chuma na chuma cha pua ya China kuwa ni hatua kubwa ya maendeleo, lakini watu wa sekta hiyo pia wanasema, mafanikio hayo hayamaanishi kuwa, kuanzia hapo kampuni za chuma cha pua za China zimepata nafasi ya udhibiti. Bei ya mawe ya madini ya chuma ilipanda kwa kiwango kikubwa kwa miaka minne mfululizo, hivyo China inatakiwa kutekeleza sera za udhibiti na kuboresha muundo wa sekta ya chuma cha pua na kuimarisha nguvu yake. Wataalamu wameshauri kuwa China pia inatakiwa kuboresha soko la malighafi la nchini na kuleta nafasi kubwa zaidi ya kuepusha hatari kwa kampuni za China.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-13