Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-14 19:26:57    
Mapishi ya supu ya bata

cri

Mahitaji

Bata mmoja, vitunguu maji gramu 5, tangawizi gramu 5, chumvi vijiko vitatu, chembechembe cha kukoleza ladha vijiko viwili, mizizi ya yungiyungi gramu 20, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, sukari kijiko kimoja

Njia

1. kata bata awe vipande vipande, halafu mimina maji kwenye sufuria kisha chemsha. Tia vipande vya bata kwenye sufuria kwa dakika mbili ili kuondoa damu ya bata. Vipakue.

2. washa moto mimina tena maji kwenye sufuria tena, tia vipande vya bata kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi, mizizi ya yungiyungi, mimina mvinyo wa kupikia, tia sukari, korogakoroga, baada ya kuchemka, punguza moto na endelea kuchemsha kwa saa mbili, kabla ya kupakua, tia chumvi. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kunyuwa.