Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-14 20:33:16    
Profesa wa Kenya awafundisha vijana namna ya kulinda haki ya hakimiliki

cri

Bwana Mtua alianza kueleza ni hasa maana ya COPYCANE, COPYCANE ni chama kilichoundwa kwa manufaa ya kutetea haki za watunzi wa kazi za sanaa, waimbaji wa muziki na watu wote wanaohusika na kazi ambazo zina haki nakiri za ujuzi ( hataza). Ili wasiweze kunyanywasa au kazi zao zisitumiwe au kuhujumiwa na watu wengine bila ya wao kujua na kunufaika na pesa zitokanazo na vipaji au ujuzi wao.

Lengo la pili la kuundwa kwa chama cha COPYCANE ni kutetea haki nakiri ili mtu yoyote asiweze kuchukua kazi ya msanii au mtunzi kutaka kuitumia au kuirudufu bila idhini ya muhusika na kuweza kupotosha dhana iliyomfanya msanii au mtuzi kutunga . Kwa mfano wale wanaotoa nakala za vitabu au kazi zozote za sanaa, mara nyingi huwa wanatoa nakala sehemu chache wanazohitaji wao huweza kuharibu maana au kupotosha ujumbe uliomo katika kitabu, makala au kazi yoyote ile ya sanaa. Kwa hiyo kwa ujumla COPYCANE ni chama kinachotetea maslahi na haki za watunzi au wale wanaomiliki haki.

COPYCANE ilianzishwa mwaka 1994 na washika wadau katika sekta ya ubunifu au utunzi na uchapishaji wa vitabu na makala, kilianzishwa kutokana na msukumo uliokuwepo katika sehemu nyingi duniani ambapo matukio mengi ya wizi na utoaji nakala bila idhini ya wahusika. Kupitia chama cha haki miliki ya ujuzi duniani ( World Intellectual property organization) kulitokea msukumo kwa nchi mbalimbali kusaini mkataba wa kuheshemu na kutetea haki za watunzi kama njia mojawapo ya kuendeleza uchumi, utamaduni na kuendeleza vilevile vipaji vya uchapishaji na utunzi ili visiangamie.

Serilaki ya Kenya ilitia sahini mikataba kadhaa ili kulinda haki miliki ya ujuzi na ilianzisha chama cha Haki miliki ya ujuzi cha Kenya(Kenya Intelectual Property Organization)

Pia kulikuwa na msukumo kutoka kwa shirika la biashara duniani (WTO) kwa nchi zote zilizo wanachama zianzishe sheria za kulinda haki miliki ya ujuzi(Copy Right Act) ambazo zitawatunza watunzi na wabunifu wa kazi za sanaa.

Akielezea kuhusu ni nani wanachama wa COPYCANE, Bwana Mtua alisema, "COPYCANE wanachama wake ni mashirika na sio watu binafsi" aliendelea kusema kuwa, watu wengi wanaohusika na utunzi na ubunifu wa kazi sanaa wameingia katika chama hicho kupitia mashirika au vyama vyao, kwa mfano wanahabari wa Kenya wanaingia COPYCANE kupitia Muungano wa wanahabari wa Kenya(Kenya Union of Journalists) na wale wenye makampuni ya uchapishaji kama vile Longman, Mcmillan na wengineo wanaingia katika chama hiki kupitia Chama cha wachapaji cha Kenya(Kenya Publishers Association) N.K

Bwana Mtua alisema pia, chama cha COPYCANE kinashirikiana bega kwa bega na shirika la Kenya Co-operate Board ambalo limeundwa na serikali, na nguvu za chama zimetokana na ile sheria ya hakimiliki ya ujuzi (Copry Right Act). Chama hiki kimesajiliwa na Kenya Co-operate Board na kupewa idhini, ruhusa na mamlaka ya kuhakikisha kwamba kazi ambazo inafanya zinaambatana na mamlaka ya kisheria, ila atakaye kiuka aadhibiwe kwa mujibu wa sheria kama ilivyopendekezwa katika Kenya Co-operate Act , hivyo serikali imewapa nguvu ya kutosha.

Akieleza adhabu inayoweza kumkuta mtu atakayepatikana na hatia ya kunakili au kurudufu kazi yoyote bila idhini ya mwenye hakimiliki, bwana Mtua alisema" Mtu yoyote atakayekamatwa akitoa nakala ya kitabu, gazeti, makala au kurudufu kanda muziki atatozwa faini ya shilingi laki nne za Kenya au kutumikia kifungo cha miaka 10 jela"

Kwa kuanzia COPYCANE ilianzia na wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wao wana mtindo wa kutoa nakala vitabu, na kwa vile wengi wa wahadhili wengi wa vyuo vikuu ni watunzi wa vitabu na wandishi hivyo COPYCANE iliongea nao na kukubaliana na kuingia nao mkataba ambao unawaruhusu wao wenyewe kufanya usimamizi katika vyuo vyao.

Akizungumzia kuhusu namna COPYCANE inavyoweza kulinda hakimiliki ya ujuzi kwa kazi za watunzi au wasanii wa Kenya katika nchi za nje, Bwana mtua alisema, chama cha COPYCANE kinaungana na mataifa mengine kupitia mkataba wa kimtaifa unaoitwa Bilateral Agreement ili kulinda kazi na haki zote za watunzi na wabunifu bilateral