Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-16 16:24:10    
Wachina waishio barani Afrika wajiendeleza kwa kuchapa kazi

cri

Kutokana na ongezeko la kasi la uchumi na ufunguaji mlango nchini China, wachina wengi zaidi wanaenda nchi za nje kutafuta nafasi za kujiendeleza. Bwana Wu Guobing ni mzaliwa wa mkoa wa Zhejiang, kusini mwa China, mwezi Machi mwaka 2000 alikwenda Ghana kufanya biashara, ambapo alifungua duka la jumla la idhaa zinazotengenezwa nchini China huko Accra, Ghana. Bwana Wu alisema, Ghana ina hali tulivu ya kisiasa na hali nzuri ya usalama, tena ina mfumo mzuri wa sheria, na serikali ya Ghana ina utaratibu mzuri wa kuvutia vitega uchumi kutoka nchi za nje. Bw. Wu alisema kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji, hivi sasa makampuni makubwa 183 ya China yamewekeza nchini Ghana, na idadi ya wafanyabiashara wa China walioko nchini Ghana pia inaongezeka kwa haraka na kufikia kati ya elfu tatu na nne.

Bwana Yuan Li alikwenda nchini Togo, Afrika magharibi baada ya kuhitimu tu kutoka chuo kikuu, baada ya jitihada za miaka minne, yeye amekuwa meneja mkuu wa kundi la makampuni la biashara ya kimataifa huko Togo. Mwaka 2002 alipokwenda nchini Togo hakuwa na fedha nyingi, alipaswa kukodisha nyumba isiyokuwa na samani, alilala kwenye godoro lililowekwa sakafuni, jambo lililomsumbua zaidi ni kwamba, baada ya nusu mwaka toka afike nchini Togo, kampuni aliyohudumia iliondoka nchini humo. Bw. Yuan Li aliamua kubaki peke yake, alitafuta kazi mwenyewe na kulimbikiza fedha, halafu alianzisha biashara yake kwa kusafirisha bidhaa kutoka China. Baadaye alinunua kiwanda cha nguo cha kushona sare za jeshi la Togo, alisajili kampuni ya kushughulikia utoaji wa mizigo bandarini na alianzisha kampuni ya kuuza magari, na kampuni ya utalii.

Bw. Yuan Li alisema, kuimarika kwa ushirikiano kati ya China na Afrika si kama tu kumeleta manufaa makubwa kwa watu wa Afrika, yeye na wachina wengine waishio katika nchi za Afrika pia wamenufaika kutokana na sera ya China kutoa mikopo yenye riba nafuu na kusamehe ushuru wa bidhaa nyingi za nchi maskini za Afrika. Anatumaini kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika utaimarika zaidi.

Bw. Wu Guobing alisema licha ya mazingira mazuri ya uwekezaji na faida kubwa itokanayo na iashara, maisha ya nchini Ghana pia ni mazuri. Wakazi wenyeji ni wakarimu, na wachina waishio huko wana hadhi muhimu kwenye jamii. Kwa upande mwingine kutokana na kuwa Ghana ni nchi ya pwani, inapakana na bahari ya Atlantiki, hivyo hali yake ya hewa si joto sana wala si baridi sana. Kwa upande wa chakula, Bw. Wu alisema, Ghana ina aina nyingi za samaki wa baharini, hivyo kula samaki wa baharini ni chaguo zuri kutokana na sifa bora na bei ya chini, lakini bei ya mboga ni kubwa, hivyo wachina wengi wanajaribu kulima mboga wenyewe.

Lakini kuishi nchini Ghana hakuna njia nyingi za kujiburudisha kwa wachina, wachina wengi wanapenda kuimba nyimbo za Karaoke, lakini mijini Accra hakuna chumba cha hata kimoja cha Karaoke isipokuwa baa za pombe na Kasino tu. Bwana Wu Alisema, baada ya kumaliza kazi wachina waishio nchini Ghana hawana nafasi nyingi za kukusanyika pamoja, wengi wao huwa wanacheza karata na kucheza chesi tu nyumbani.

Bwana An Youzhong ni mpiga picha maarufu wa China ambaye ameishi nchini Uganda kwa muda fulani, anaipenda nchi hiyo kutokana na mandhari nzuri na hali nzuri ya hewa, anasema Uganda ni nchi mwafaka kwa binadamu kuishi, bila shaka wachina waishio nchini humo wanafurahia maisha na kazi za huko. Bwana An alisema, hivi sasa zaidi ya wachina 1000 wanaishi nchini Uganda, ambao wanaweza kugawanywa kuwa vikundi viwili, kikundi kwa kwanza ni wale wanaotumwa na serikali kutekeleza mikataba ya kutoa misaada na ujenzi wa miradi, kikundi cha pili ni wafanyabiashara wadogo wadogo. Kutokana na kuwa bei za vitu vya maisha ya kila siku huko Uganda ni kubwa zaidi kuliko China, hivyo wafanyabiashara wengi wa China wanapeleka bidhaa zilizotengenezwa nchini China kama vile nguo, viatu na vitu vingine vya maisha ya kila siku nchini Uganda kwa njia ya makontena, halafu kuwauzia wafanyabiashara wa Uganda kwa jumla.

Bwana An Youzhong alisema, kama ajuavyo kufanya biashara nchini Uganda ni rahisi, na gharama za maisha huko ni ndogo. Licha ya bidhaa za matumizi ya kawaida, kununua magari yaliyotumika na kukodisha nyumba ni rahisi zaidi kuliko nchini China, hivyo wafanyabiashara wengi wa China waishio nchini Uganda wanaweza kumudu maisha nchini humo

Bwana An Youzhong alisisitiza kwa usema kuwa, licha ya hali isiyo nzuri sana ya usalama, ambapo afanyabiashara wa China wanapaswa kuwaajiri askari polisi ili kujilinda. Uganda ina mazingira mazuri ya kuishi, ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa la tatu la maji baridi duniani liko karibu na mji mkuu Kampala, hivyo katika wakati wa mapumziko, wachina wengi wanapenda kwenda kuvua samaki na kusafiri kwa mashua kwenye ziwa hilo ili kujiburudisha.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-16