Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-19 18:16:01    
Mji wa Filamu mjini Yinchuan mkoani sehemu Ningxia

cri

Katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China kuna mabaki mengi ya majengo ya kale yaliyojengwa katika enzi mbalimbali za kifalme za zama za kale nchini China, majengo hayo yametapakaa kwenye eneo la jangwa mkoani humo, na Mji wa Zhenbeibao uliosifiwa kuwa ni "Hollywood ya mashariki" ni moja kati ya mabaki hayo.

Mji wa Zhenbeibao uko kwenye umbali wa kilomita 30 kutoka kaskazini magharibi ya Yinchuan, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa kabila la wahui wa Ningxia, magharibi ya China, mji huo ulikuwa mji wa mpakani uliojengwa wakati wa Enzi za Ming na Qing. Mji huo umegawanyika katika sehemu mbili, moja ni mji wa majengo yaliyojengwa katika zama za Enzi ya Ming za karne ya 16, mji wa sehemu hiyo unaitwa "Mji wa Ming" ; na wa sehemu nyingine ni mji mpya uliojengwa wakati wa zama za miaka mitano ya mfalme Qianlong wa Enzi ya Qing mwaka 1740, mji huo unaitwa "Mji wa Qing".

"Mji wa Ming" ulijengwa kwa kuegemea na milima mirefu na mabonde yenye vipengele, ndiyo maana mji huo ulikuwa mji muhimu kwenye ulinzi wa mpaka tangu zama za kale, mji wenye hali maalum wa namna hii unawavutia sana wasanii wa filamu wa China na wa nchi za nje kupiga filamu huko. Mabaki mengi ya kale mjini humo kama vile magofu ya aina mbalimbali, makazi ya zama za kale yaliyoharibika, yote yameoneshwa kwenye filamu nyingi zilizopigwa chini ya uelekezaji wa wasanii hao, hivyo Mji wa Zhenbeibao umesifiwa kuwa ni mji wa filamu, filamu nyingi zilizopigwa mjini humo zimeiwezesha dunia ijue China. Mwongozaji wa walii Niu Shuhui ni msichana mchangamfu sana, amefanya kazi mjini Zhenbeibao kwa miaka 10, alisema mji huo ni nyumbani kwake.

Katika mji huo, hali ya miundo mbinu ni duni sana, pembezoni mwake hakuna maji wala njia, hata hakuna chanzo cha kuleta umeme, mji huo kweli ni kama sehemu iliyoachwa na binadamu. Kutokana na maendeleo ya miaka kadhaa ya karibuni, filamu nyingi zilipigwa mjini humo hivyo majengo mbalimbali yamejengwa mjini humo kutokana na mahitaji ya kupiga filamu. Na utamaduni unaooneshwa kwenye usanifu wa majengo hayo ya filamu huwa unahusu mila na desturi za sehemu ya kaskazini magharibi ya China, hivyo sehemu hiyo imewavutia watalii wengi siku hadi siku, hali kadhalika mji huo umeendelezwa zaidi.

Mwaka 1981, mwandishi maarufu wa vitabu wa China Bwana Zhang Xianliang alitangulia kuujulisha Mji wa Zhenbeibao kwa dunia. Na mwongozaji wa filamu wa China Bwana Zhang Junzhao ni mwongozaji wa kwanza aliyeelekeza upigaji wa filamu iitwayo "Ofisa mmoja na wahalifu wanane" mjini Zhenbeibao, na mpiga picha wa filamu hiyo ni Bwana Zhang Yimou ambaye hivi sasa amekuwa mwongozaji maarufu wa filamu. Bwana Zhang Yimou anaupenda sana mji huo wenye mabaki mengi ya kale ya eneo la magharibi la China tangu wakati huo, na filamu iitwayo "Mtama mwekundu" iliyopigwa chini ya uelekezaji wake katika mji huo ilipata tuzo ya "Dubu wa dhahabu" katika tamasha la filamu la Berlin mwaka 1988.

Tokea hapo, filamu mbalimbali kama vile "Utenzi wa Mto Manjano", "Jumba la ukoo wa Qiao" na nyinginezo zilipigwa kwa mfululizo mjini humo, filamu hizo zimeiwezesha dunia ijue zaidi filamu za China, pia imeiwezesha dunia ijue zaidi eneo la magharibi la China.

Chini ya ukuta mkubwa wa kutia saini za watu mjini Zhenbeibao, mwongozaji watalii msichana Niu Shuhui akifahamisha alisema:

Kwenye ukuta huo, tunaweza kuona saini za wasanii mbalimbali wa filamu, na kila mmoja alitia saini yenye mtindo wake pekee, watu wanaweza kupata taswira kuhusu sura ya msanii huyo.

Ukilinganishwa na "Mji wa Qing", katika "Mji wa Ming", yametapakaa majengo mengi ya udongo wa manjano, majengo hayo yalionesha hali ya zama za kale ambayo yalidhoofika katika miaka mingi iliyopita. Lakini je, ni namna gani wasanii walipiga filamu zinazoonesha sanaa ya China kwa kutegemea ardhi hiyo ya udongo wa manjano yenye hali asili ya kale. Filamu iitwayo "Mtama mwekundu" iliyopigwa katika sehemu hiyo imeonesha vilivyo hali ya zama za kale nchini China.

Mbele ya mlango wa Mwezi wa Jengo moja lililooneshwa ndani ya filamu iitwayo "Mtama mwekundu", hali halisi na historia ya zama za kale zinaonekana kama zimechanganywa. Mtalii kutoka sehemu ya ndani ya China Bibi Li Jun alipigwa picha mbele ya mlango huo, alisema:

Hali ya sehemu hiyo ni tofauti kabisa na ile ya sehemu zilizoko kusini mwa Mto Changjiang, naipenda sehemu hiyo, hali isiyo na msongamano kwenye ardhi hiyo, na hakuna majengo mengi kama ilivyo kwenye miji mingine, hali hiyo haionekani katika sehemu za kusini mwa Mto Changjing.

Sehemu ya "Mji wa Qing" iliyoko kwenye umbali wa mita 200 toka kaskazini ya sehemu ya "Mji wa Ming", ni sehemu ya mji mpya, yaani "Mji wa Qing", ambapo hata kuta za mji umehifadhiwa kikamilifu. Mwandishi maarufu wa vitabu Bwana Zhang Xianliang aliposimulia kuhusu mlango wa mji huo kwenye maandishi yake alisema, mlango asili wa kuta za udongo uliondolewa zamani sana, zamani mlango huo ulikuwa kama tundu kubwa lenye hali duni. Lakini baada ya kuidhinishwa na idara za uhifadhi wa mabaki ya kale mwaka 2000, wakazi wa huko walikwenda Mji wa Guyuan ulioko kwenye sehemu ya mlimani kilomita mia kadhaa nje ya "Mji wa Qing" kutafuta matofali ya zamani yaliyobaki wakakarabati mlango wa mji huo na kudumisha hali asili ya mlango huo.

Watalii wakiingia kwenye "Mji wa Qing" wataona barabara moja inayojulikana kuwa ni barabara ya filamu. Kwenye barabara hiyo, kuna maduka mbalimbali kama vile duka la kuuzia nyama, benki ndogo, mikahawa ya chai na duka la vitambaa, jumba la kuoneshea michezo ya sanaa, na duka la vitambaa vyenye taraza, na barabara hiyo imeonesha hali halisi ya historia ya miaka elfu kadhaa iliyopita nchini China. Mtalii kutoka sehemu ya mashariki ya China Bwana Jiang Haifeng alifurahia sana hali ya sehemu hiyo ya "Mji wa Qing". Alisema:

Niliambiwa mara kwa mara kwamba, baada ya kufika mkoani Ningxia lazima niende kutembelea mji wa filamu. Kweli nimeona kuwa katika sehemu hiyo kuna mabaki mengi ya kale, na vitu vingi vya zama za kale katika Enzi za Ming na Qing vinaonekana katika sehemu hiyo, ambavyo haviwezi kuonekana katika miji mingine, hali kadhalika, vitu vingi na majengo mengi yaliyooneshwa kwenye filamu vinaonekana katika sehemu hiyo.

Watalii wakipanda mlango wa "Mji wa Qing" wanaweza kuangalia Mlima Helan ulioko kaskazini mwa Mkoa wa Ningxia, ambapo wanaweza kuona mandhari nzuri ya mji mzima wa kale, ambapo hali ilivyo ya hivi sasa na hali ya mvuto wa usanii zimechanganywa ambazo haziwezi kutofautiana. Mji wa Zhenbeibao unawavutia watalii kwa mvuto wake pekee.

Idhaa ya Kiswahili 2007-02-19