Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-20 19:10:19    
China ya jitahidi kuongeza ajira

cri

China ni nchi yenye watu bilioni 1.3, ni nchi yenye idadi kubwa kabisa ya watu duniani, hivyo utatuzi wa suala la ajira ni kazi kubwa. Katika miaka ya karibuni, serikali ya China imekuwa ikizingatia kuongeza ajira, na kulichukulia suala hilo kuwa ni kazi muhimu ya kutatua matatizo ya maisha ya watu.

Bw Li Muhan ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa chuo kikuu cha lugha cha Beijing, ingawa bado kuna muda mrefu kidogo kwa yeye kuhitimu masomo yake, lakini dada huyo ameanza kushughulika. Si siku nyingi zilizopita alitoa ombi la ajira kwenye tovuti ya ajira ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya China, baada ya wiki moja tu akapata jibu.

"Hapo zamani, tukitaka kupata ajira katika kampuni tunazopenda, tulitakiwa kutafuta sisi wenyewe katika tovuti za idara mbalimbali za serikali, na shughuli hizo zinachukua muda mwingi. Hivi sasa ni kazi rahisi sana, tutaweza kumaliza kazi hiyo kwa kutoa maombi kwenye tovuti ya ajira."

Tovuti za ajira kwa ajili ya wanafunzi wanaohitimu masomo ya vyuo vikuu vya China ilianzishwa na idara tano zikiwemo kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa pamoja na wizara za elimu, kazi na huduma za jamii. Lengo la kuanzisha tovuti hiyo ni kupunguza shinikizo la ajira linalotokana na ongezeko la mfululizo nchini China. Katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, vyuo vikuu vya China viliongeza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa, hatua hiyo ilitoa fursa ya elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wengi zaidi, lakini imeongeza shinikizo la kutafuta ajira kwa wanafunzi waliohitimu masomo ya vyuo vikuu. Mwaka huu, wanafunzi wa vyuo vikuu milioni 4.9 watahitimu masomo na kutafuta ajira, kiasi hicho ni ongezeko la zaidi ya laki 7 kuliko mwka jana, na ongezko hilo litazidi watu milioni 5 katika mwaka ujao.

 

Ofisa wa wizara ya kazi na uhakikisho wa jamii Bw. Yi Jiankun alisema, China imechukua hatua kadhaa ili kuongeza ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

"Kwa mfano, kabla ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuhitimu masomo yao, vyuo vikuu vinatoa mapendekezo ya kazi kwa wanafunzi hao, na mashirika ya huduma za ajira ya umma pia yameanzisha huduma za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wakati idara husika za serikali zinaanzisha mkutano wa mazungumzo wa kuwasaidia wanafunzi kupata ajira. Moja ya vyanzo vinavyoleta shida kwa ajira za wanafunzi wanaohitimu masomo ya vyuo vikuu ni kukosa uzoefu unaohitajika. Hivyo idara husika za serikali ya China zinaweka utaratibu wa mazoezi kabla ya kuanza kazi, kujenga vituo vya mazoezi katika baadhi ya kampuni na viwanda, ambapo watafundishwa na walimu na kuongezwa uzoefu ili kukuza uwezo wa kazi."

Katika miaka ya karibuni, suala la ajira kwa ziada ya nguvukazi iliyohamishwa kutoka sehemu ya vijiji limekuwa tatizo kubwa nchini China. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2005, jumla ya idadi ya wakulima vibarua kwenye miji ya China ilizidi milioni 125, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 7.55 kuliko mwaka uliopita.

Ili kuwawezesha wakulima vibarua wapate ajira, miji mbalimbali ya China licha ya kuandaa mikutano ya ajira, imeweka utaratibu wa kutoa habari bila malipo kwa wakulima kila baada ya muda maalumu. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka jana miji mbalimbali ya China iliandaa mikutano maalumu laki 4.3 kwa ajili ya wakulima wanaotaka kufanya vibarua mijini na kutoa ajira zaidi ya milioni 6.

Ofisa wa wizara ya kazi na uhakikisho wa jamii ya China Bw. Yin Jiankun alisema, serikali ya China pia imebuni mipango husika ili kukuza uwezo wa kazi kwa wakulima vibarua.

"Tokea mwaka jana tumetekeleza mpango wa kukuza uwezo wa kazi, ambao utatoa mafunzo ya kazi kwa wakulima milioni 40 ili kukuza uwezo wa kazi kwa wakulima wanaofanya vibarua mijini."

Mao Dong ni kijana mwenye umri wa miaka 19 aliyetoka sehemu ya vijiji ya mkoani Henan, sehemu ya kati ya China. Mwaka jana alikwenda kufanya vibarua katika mji wa Suzhou ulioko sehemu ya mashariki mwa China. Huko kijana Ma Dong anafanya kazi ya uchapishaji katika kampuni moja ya uzalishaji wa zana za mawasiliano ya habari, baada ya kuajiriwa alipewa mafunzo kabla ya kuanza kazi rasmi.

"Baada ya kufika kwenye kampuni hiyo, tulipewa mafunzo kwa siku 5, licha ya kufahamishwa habari kuhusu kampuni hiyo, tulipata ufahamu kuhusu usalama kazini, kuzuia maafa ya moto na usalama wa barabarani. Baada ya hapo, walipelekwa na mwalimu wao katika kazi zao, na kufahamishwa ujuzi wa matumizi ya mitambo ya huko. Mafunzo hayo yaliwasaidia kuweka msingi mzuri kwa kazi zao."

Mbali na wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya vibarua mijini, serikali ya China imechukua hatua za kuwasaidia watu wasio na kazi kupata ajira. Kwa mfano, serikali inatoa mikopo midogo kwa watu wanaokosa ajira au kuwapunguzia kodi. Aidha serikali inatoa baadhi ya ajira za huduma za umma kwa baadhi ya watu wenye shida ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa lengo lililowekwa na idara husika, mwaka jana vijana milioni 9 wa miji ya China wangepata ajira, na wafanyakazi milioni 5 waliopunguzwa kutoka kwenye viwanda vya serikali wangepata ajira ili kudhibiti kiasi cha watu wanaokosa ajira kiwe chini ya 4.6%. Hadi mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka uliopita, viwango vingi vya lengo hilo vilitimizwa kabla ya wakati uliowekwa.

Ofisa wa wizara ya kazi na uhakikisho wa jamii ya China Bw. Yin Jiankun alidokeza kuwa hivi sasa serikali ya China imenuia kuunda utaratibu wa muda mrefu wa ajira unaounganisha kazi za ajira na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii. Alisema,

"Kwanza ni kuanzisha hali ya kuhimizana kati ya maendeleo ya uchumi na ongezeko la ajira, kuongeza ajira katika ukuzaji wa maendeleo ya uchumi na kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa ongezeko la ajira. Pili, kutoa uhuru kwa watu wanaotafuta ajira, ambao watachuguliwa na kampuni au viwanda. Tatu, ni kuboresha utaratibu wa huduma za ajira, na kutoa huduma bila malipo kwa wakazi wa mijini na vijijini."

Mbali na hayo, China itaunda utaratibu wa kutoa mafunzo ya kazi kwa wafanyakazi wote; na utaratibu wa utoaji msaada kwa watu waliopunguzwa katika viwanda vya serikali.