Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-20 19:14:14    
Barua 0218

cri

Leo tarehe 18 Februari ni Siku ya kwanza ya Tarehe 1 Januari kwa kalenda ya kilimo ya China, ambayo ni siku ya mwaka mpya wa jadi wa China, kwa niaba ya Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa tunawatakia wasikilizaji wetu popote pale mlipo heri na baraka za mwaka mpya.

Kutokana na mila na desturi za wachina, sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China husherehekewa kwa wiki tatu ambayo inaanzia tarehe 23 mwezi 12 hadi tarehe 15 Januari, kwa kalenda ya kilimo ya China. Katika siku hizo za mwaka mpya, wachina wanasherehekea zaidi siku ya mwisho yaani Tarehe 30 ya mwezi wa 12 kwa kalenda ya kilimo ya China yaani mkesha wa sikukuu, na siku ya kwanza ya Tarehe 1 Januari kwa kalenda ya kilimo ya China, siku hizi mbili ni kama kilele sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China.

Kutokana na maombi ya wasikilizaji wetu, leo kwanza tunapenda kuzungumza kuhusu mila na desturi za China kuhusu kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China.

("Tambiko kwa Mungu wa jiko katika China", Chakula cha Kichina Jiaozi)

Sasa tunawaletea barua za wasikilizaji wetu.

Msikilizaji wetu Mbarouk Msabah Mbarouk wa sanduku la posta 52483 Dubai Falme za Kiarabu ametuletea barua pepe inayozungumzia "juhudi za China katika kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea". Katika barua hiyo Bwana Mbarouk anasema, suala la nyuklia la peninsula ya Korea ni moja kati ya tishio kubwa kwa usalama na utulivu wa kisiasa katika eneo la kaskazini mashariki ya Asia, eneo ambalo linazidi kustawi kiuchumi na kimaendeleo kila kukicha, kama vile Korea ya Kusini , Jamhuri ya watu wa China na Japan, hasa tukizingatia kwamba tayari nchi hiyo imeshafanya majaribio ya silaha hizo.

Hata hivyo lakini ni jambo na kutia moyo sana kuona kwamba Jamhuri ya Watu wa China imekuwa mstari wa mbele kabisa katika juhudi za kutatua suala hilo kwa njia za amani kati ya mazungumzo ya pande sita, ili kuepusha maafa ya vita kutokea katika eneo hilo.

Ushahidi wa hayo ni mkutano wa kipindi cha tatu wa duru la tano la mazungumzo ya pande sita uliofanyika mjini Beijing China mwezi Februari mwaka huu, kati ya Korea ya Kusini, Korea ya Kaskazini, Russia, Marekani na Japan, jambo ambalo linaudhihirishia ulimwengu ni jinsi gani Jamhuri ya Watu wa China ilivyokuwa ni kama "Dalali wa Amani" na pia ni nguzo muhimu katika kupatikana kwa utatuzi wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea kwa manufaa ya mataifa ya eneo hilo na ulimwengu kwa ujumla.

Historia inatukumbusha kwamba zaidi ya miaka 60 iliyopita eneo la Mashariki ya mbali lilishuhudia maafa makubwa ya mashambulizi ya mabomu ya atomiki yaliofanywa na Marekani dhidi ya Japan iliyokuwa ya utawala wa kifashisti na kivamizi katika miji ya Hiroshima na Nagasaki , ili kuilazimisha nchi hiyo kuacha uvamizi wake dhidi ya mataifa mbalimbali katika bahari ya Pasifik.

Bwana Mbarouk anasema, kwa maoni yake binafsi kutokana na fikra mahiri za viongozi wa chama cha kikoministi cha China, ndio maana leo hii tukashuhudia jinsi gani harakati za kupigania fumbuzi wa amani juu ya swala hilo kumekuwa kukipewa umuhimu wa kipekee na viongozi wa China, jambo ambalo linastahiki kupongezwa na Jumuiya ya Kimataifa.

Tunamshukuru sana Bwana Mbarouk Msabah kwa barua yake ambayo inatufuatilia sana matangazo yetu, kweli inatuwezesha kuona kuwa juhudi zetu hazipotei bure, tunafurahi kutambua kuwa wasikilizaji wetu wengi wanatusikiliza na kutufuatilia.

Msikilizaji wetu Mutanda Ayub wa Bungoma Kenya ametuletea barua pepe akisema, angependa kuchukua fursa hii kutuma salamu zake za dhati pamoja na kupongeza wafanyakazi wote kwa kazi ambayo wanatekeleza usiku na mchana. Anasema kwa siku chache ambazo zilizopita alikuwa na shughuli kadha wa kadha vijijini. Kwa hivyo hakuwa na nafasi ya kuwasiliana na Radio China kama kawaida.

Hata hivyo amekuwa akifuatilia vipindi bila kukosa hata siku moja. Vilevile amekuwa na nafasi nzuri ya kukutana na wasikilizaji ambao makao yao yako vijijini kama kule Mautuma, Chwele, Lwanda, Sangalo, Mabanga, Kisochele, Konambaya, Webuye, Sikalame, Ekitale, Lugulu, Lugulu, Mukyuni-Tongaren , Matumbufu, Siaka kijijini kwa Bw. Kennedy Nyongesa Barasa wa Yaya Shop. Angependa kuwashukuru wasikilizaji wote ambao waliweza kumkaribisha na kumsikia akiwafahamisha kuhusu yale aliyojifunza na kujionea nchini China, hasa miji ya Beijing na Shanghai. Anawaomba radhi wasikilizaji wenzake ambao hakukutana nao, lakini kwa sasa ana mpango wa kukutana nao mwezi wa Machi.

Bwana Shariff alisema, kwa sasa anafurahia pamoja na wale waliobahatika na kuwapa zawadi kutoka Radio China Kimataifa. Labda kwa yote angependa kusema zawadi zenyewe zilikuwa chache, lakini amewaomba wasiobahatika wakati huu wasife moyo kwani kutokana na anavyoifahamu Radio China kimataifa pamoja na Wachina, wote ni watu wanaoaminika na juhudi bado zinasonga mbele, anatumai kuwa katika siku zijazo wote watafurahia.

Pia anapenda kuwapongeza wasikilizaji wenzake kama vile Mbarouk Msabah wa falme za kiarabu, Stephen Magoye wa Tanzania, Hamisi Ali Hassani wa Kenya, Mogire Machuki wa Kisii, Kilulu Kulwa wa Tanzania na wengine kwa kuendelea kuwasiliana na Radio China kimataifa bila kuchoka, kama wahenga walivyosema barua ni nusu ya kuonana.

Bwana Shariff anasema yeye na wasikilizaji wenzake wanaishukuru sana Radio China kimataifa, kwani kama isingekuwepo wasingefahamu uhusiano unaoendelea kati ya China na Afrika. Juzi alifurahia kusikia kuwa, Rais Hu Jintao wa China amesema China kamwe haitailazimisha nchi yoyote kufuata mfumo wake wa kijamii wa kimaisha; ushirikiano wa kirafiki kati ya China na nchi mbalimbali duniani ni kwa kuleta maendeleo ya uchumi na jamii, maelewano na amani.

Na mwisho anapenda kuwakumbuka wasikilizaji wenzake Ali Hamisi popote alipo, Ras Franz Manco Ngogo wa Tarime Tanzania, Ken Nyongesa wa Yaya shop, Stephen Magoye wa Tanzania.