Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-26 19:44:55    
Jumba la maonesho ya vipande vya Jian na Du vyenye maandishi ya kichina mjini Changsha

cri

Leo tunawaoongoza kwenda mjini Shangsha mkoani Hunan, katikati ya China kutembelea Jumba la maonesho ya vipande vya Jian na Du, yaani vipande vya mianzi au vya mbao vyenye maandishi ya kichina mjini Changsha.

Katika zama za kale nchini China, kabla ya kuvumbuliwa kwa karatasi, Jian na Du yaani vipande vya mianzi na vya mbao vilikuwa vyombo muhimu ambavyo vilitumiwa kuandikwa maandishi kwa ajili ya kusoma au kuweka kumbukumbu. Mabaki ya vipande hivyo vingi ni ya mianzi, kichina kinasema ni Zhujian, kila kipande cha mwanzi kina urefu wa zaidi ya sentimita 20, na upana sentimita 1.

Na Du ni vipande vya mbao, urefu wa kila kipande cha mbao unalingana na ule wa kipande cha mwanzi, lakini upana wake ni mkubwa zaidi kuliko ule wa kipande cha mwanzi, hata kwenye vipande vya mbao yameandikwa maandishi mengi zaidi yaliyoeleza tukio moja. Katika zama za kale nchini China, watu walitunga vipande vya mianzi au vipande vya mbao kuwa "vitabu" vya kusoma.

Jumba la maonesho ya vipande vya Jian na Du vyenye maandishi lililoko kwenye Barabara ya Baisha mjini Changsha mkoani Hunan lina eneo la zaidi ya mita 14,000 za mraba. Ndani ya jumba hilo kuna chemchemi, na miti ya mianzi, ambapo ujenzi wa jumba hilo ni wenye mtindo asili wa kichina. Jumba hilo lilijengwa kwenye sehemu ya mabaki ya Jengo la Zoumalou yaliyofukuliwa. Mwaka 1996, watafiti wa mambo ya kale waligundua kuwa kwenye mabaki ya Jengo la Zoumalou kuna vipande vya Jian na Du vya enzi ya Madola matatu ya Wei, Shu na Wu ya miaka 2000 iliyopita, vipande hivyo vilifikia laki moja, ambavyo vilizidi vile vya jumla vilivyogunduliwa katika karne ya 20. Mkuu wa Jumba la maonesho ya vipande vya Jian na Du la Changsha Bwana Song Shaohua alisema:

Vipande hivyo vya Jian yaani Zhujian vilizikwa chini ya ardhi kwa zaidi ya miaka 1700, vimeonekana kuwa na hali mbaya ya kuoza, kama watu hawatachukua tahadhari, maandishi yaliyoandikwa kwenye vipande hivyo hata yanaweza kufutwa mara moja. Na vipande hivyo vya mianzi ni vyepesi kama tambi, baada ya kudhoofika kwa miaka mingi, haviwezi hata kuchukuliwa kwa mikono, ila tu kuviweka kwenye kioo halafu kutumia brashi kuvisafisha polepole ili maandishi yaliyoandikwa juu yake yaweze kuonekana vizuri.

Bwana Song Shaohua alisema, kufukuliwa kwa vipande hivyo vya mianzi kumewashangaza na kuwafurahisha sana watafiti wa mambo ya kale wa mkoani Hunan na kote nchini China. Kabla ya hapo, mabaki ya kale yaliyofukuliwa mkoani Hunan mengi yalikuwa ni vyombo vya shaba nyeusi, vyombo vya chuma na vyombo vya kauri. Vipande vya Jian na Du vyenye maandishi vilivyofukuliwa vinadhaniwa kuwa ni ugunduzi mkubwa wa mambo ya kale katika karne ya 20 baada ya kugunduliwa kwa maandishi yaliyochongwa kwenye mifupa ya magamba ya kobe yaliyogunduliwa huko Yinxu katika Enzi ya Shang ya zama za kale pamoja na maandishi ya Dunhuang nchini China. Mkazi wa Changsha Bibi Wu Liping aliyetembelea mara kwa mara Jumba la maonesho ya vipande vya Jian na Du yenye maandishi ya kichina alisema:

Naona ni vigumu kupatikana kwa vipande hivyo vya Jian na Du vyenye maandishi ya kichina ambavyo vimehifadhiwa vizuri mpaka sasa, hata maandishi juu ya vipande hivyo yanaonekana wazi sana.

Katika historia ya China, Kipindi cha madola matatu ya miaka 2000 hivi iliyopita kilikumbwa na vurugu za vita vilivyotokea mara kwa mara, data za historia ya kipindi hicho zilizogunduliwa ni chache sana. Hivyo vipande laki moja vya Jian na Du vyenye maandishi ya kichina vinavyohusu dola la Wu la kipindi hicho vimeziba pengo hilo. Wataalamu wengi wa idara za utafiti wa mabaki ya kale wa China wanaona kuwa, kufukuliwa kwa vipande hivyo vya Jian na Du kutahimiza zaidi utafiti wa mambo ya siasa na utamaduni ya kipindi cha madola matatu, pamoja na mfumo wa kisiasa, uhusiano kati ya watu katika jamii, uhusiano wa kiuchumi, utaratibu wa kodi na kadhalika, hayo yote yameonesha kuwa maendeleo makubwa yanatazamiwa kupatikana katika utafiti kuhusu historia ya zama za kale kwenye kipindi tofuati nchini China, utafiti huo umewekwa kando kwa muda mrefu.

Ili kuwawezesha watu wanaotembelea wavielewe vizuri vipande vya Jian na Du vyenye maandishi ya kichina, Jumba la maonesho la vipande vya Jian na Du la Changsha limefanya juhudi kubwa sana. Mkuu wa jumba hilo Bwana Song Shaohua alisema:

Tulipoandaa maonesho, tuliongeza ujulisho wa ujuzi wa kawaida kuhusu elimu ya Jian na Du, kama vile jinsi vipande vya Jian na Du vilivyotengenezwa na vilitengenezwa kwa vyombo gani. Watazamaji wanapenda kuelewa ujuzi huo. Kwenye maonesho, tuliweka kibanda kimoja maalum kinachoonesha utaratibu wa usanii wa utengenezaji wa vipande hivyo, toka kukatwa kwa mianzi, hadi kutengeneza mianzi kuwa kipande kimoja kimoja, hadi kutungwa pamoja na kuandika maandishi, ili watu wanaotembelea jumba hilo waweze kuelewa namna gani vitabu vya zama za kale za China vilitungwa na kuchapishwa.

Jumba la maonesho ya vipande vya Jian na Du vyenye maandishi la Changsha mkoani Hunan, China lilifunguliwa kwa majaribio mwishoni mwa mwaka 2005. Katika wiki moja baada ya kufunguliwa kwake, watazamaji laki moja hivi walitembelea jumba hilo. Lakini kutokana na kuwa kazi ya kushughulikia mazingira ya sehemu zilizo pembezoni mwa jumba hilo bado haijakamilika, hivyo jumba hilo bado halijafunguliwa rasmi, lakini jumba hilo limewavutia wakazi wa huko na watalii wanaotembela mji wa Changsha. Mtalii Bwana Li Guojun alisema:

Nimeambiwa kuwa kazi ya kushughulikia mazingira ya pembeni ya jumba hilo pamoja na kazi ya utafiti husika imekamilika kwa theluthi moja tu, ni matumaini yangu kuwa wataalamu husika watakamilisha mapema kazi hiyo, ili tuweze kuelewa mambo yote kuhusu kipindi cha madola matatu ya zama za kale nchini China.

Katika jumba hilo la maonesho, mbali na vipande vya Jian na Du vyenye maandishi ya kichina vya zama za kale, pia vimehifadhiwa vyombo vya shaba nyeusi vilivyofukuliwa kwenye sehemu ya Changsha, pamoja na mabaki mengi ya kale vyenye thamani kama vile vyombo vya kauri vya Enzi ya Tang yenye ustawi mkubwa katika zama za kale nchini China.