Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-01 19:06:23    
Mkutano wa amani kuhusu suala la Iraq wafuatiliwa na watu

cri

Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Bw. Hoshyar Zebari, tarehe 28 mwezi Februali huko Baghdad alisema, Iran na Syria zimekubali kushiriki kwenye mkutano wa amani utakaofanyika hivi karibuni, wenye lengo la kuhimiza Iraq kuwa na utulivu. Siku hiyo taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Syria ilithibitisha kuwa Syria itatuma mwakilishi kuhudhuria mkutano huo. Wachambuzi wanasema kutokana na Marekani kuunga mkono Iran na Syria kushiriki mkutano, hivyo mkutano huo utakuwa nafasi nzuri sana ya kupunguza hali ya wasiwasi katika uhusiano kati ya Marekani pamoja na Iran na Syria na kuboresha hali ya usalama nchini Iraq. Lakini kupatikana kwa mafanikio halisi kwa mkutano kinahitaji pande mbalimbali husika ziimarisha kuaminiana.

Habari kutoka upande wa Iraq zinasema, mkutano huo utafanyika tarehe 10 mwezi Machi mjini Baghdad. Licha ya kuwaalika wawakilishi wa nchi jirani za Syria na Iran pamoja na baadhi ya nchi muhimu za kiislamu, Iraq imeamua kuwaalika pia mabalozi wa nchi tano za wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa walioko nchini Iraq kushiriki. Habari zinasema mwanzoni mwa mwezi Aprili, pande mbalimbali husika zitaitisha mazungumzo ya mawaziri kuhusu suala la Iraq, ambapo washiriki wa mazungumzo watakuwa wengi zaidi.

Kutokana na hali ilivyo sasa, malengo ya Iraq kuandaa mkutano wa amani ni pamoja na, Kwanza, kutaka uungaji mkono wa nchi jirani hususan wa Iran na Syria kuhusu shughuli za usalama nchini Iraq, Pili, kuimarisha uhusiano wa nchi kubwa kwenye sehemu hiyo na kupunguza migongano.

Mwaliko wa Iraq uliitikiwa na Marekani kwa furaha. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Condoleezza Rice kwenye mkutano wa kusikiliza ushahidi kwenye bunge la taifa tarehe 27 mwezi Februari alisema, Marekani imekubali kushiriki kwenye mkutano huo pamoja na Iran na Syria. Na anatarajia kuwa serikali za nchi husika zitatumia vizuri fursa hiyo kuboresha uhusiano na Iraq na kutoa mchango kwa ajili ya amani na utulivu wa sehemu hiyo.

Wizara ya mambo ya nje ya Syria ilitoa taarifa tarehe 28 ikithibitisha kuwa, Syria itatuma maofisa kushiriki kwenye mkutano huo, ilisema Marekani na Syria kufanya mazungumzo ni hatua moja ya kuelekea upande sahihi. Hali ya mashariki ya kati inahusiana na mambo mengi ambayo yenye athari kwa mambo mengi, hivyo pande mbalimbali husika zinatakiwa kufanya mazungumzo kuhusu masuala yote ya sehemu ya mashariki ya kati.

Siku hiyo waziri wa mambo ya nje wa Iraq Bw. Hoshyar Zebari alidokeza kuwa, upande wa Iran umekubali kushiriki kwenye mkutano huo, isipokuwa haijafurahishwa na ratiba ya mkutano huo. Katibu wa kamati kuu ya usalama wa taifa ya Iran Bw. Ali Larijani alisema, Iran itashiriki mkutano ilimradi mkutano uendane na maslahi ya Iraq.

Suala linalofuatiliwa zaidi na pande mbalimbali kwa hivi sasa ni kama Marekani na Iran zitafanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa kutumia mkutano huo. Kutokana na maneno ya maofisa wa Marekani, uwezekano wa pande hizo mbili kufanya mazungumzo ya moja kwa moja ni mdogo. Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bw. Tony Snow tarehe 28 alisema, ingawa Marekani imekubali kushiriki kwenye mkutano huo pamoja na Iran na Syria, lakini hii haimaanishi kuwa Marekani itabadilisha msimamo wake kuhusu nchi hizo mbili. Bw. Snow alisisitiza kuwa Marekani haitaweza kufanya mazungumzo ya pande mbili na Iran kabla ya nchi hiyo kuacha mpango wake wa nyuklia. Siku hiyo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bw. Michael McConnell, alisema Marekani haitafanya mazungumzo na Iran peke yake, mambo yatakayozungumzwa kwenye mkutano huo ni kuhusu suala la Iraq tu, wala hayatahusu suala la nyuklia la Iran.

Wachunguzi wanasema kuna mambo mawili yanayoizuia Marekani kufanya mazungumzo moja kwa moja na Iran. Kwanza ni mgongano mkali kati ya nchi hizo mbili kuhusu suala la nyuklia la Iran, na pili ni kulaumiana na kukosa kuaminiana kati ya pande hizo mbili kuhusu suala la Iraq.

Idhaa ya kiswahili 2007-03-01