Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-05 10:05:58    
The Hague-Mahakama ya kimataifa imeifutia mashitaka Serbia kuhusiana na mauaji ya halaiki

cri
Mahakama ya kimataifa tarehe 26 iliifutia mashitaka Serbia kuhusiana na mauaji ya halaiki katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Bosnia na Herzegovina.

Uamuzi wa mahakama hiyo unasema Serbia iliwapa Waserbia fedha na misaada mingine katika vita hivyo, lakini Serbia haikuwa na uwezo wa kuamua mambo ya jeshi la Waserbia na makundi ya kijeshi ya Waserbia, kwa hiyo hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu Serbia kushiriki kwenye mauaji ya halaiki dhidi ya watu wasio Waserbia waliokuwa Bosnia na Herzegovina katika vita hivyo vilivyotokea miaka ya 90 ya karne iliyopita.