|
Nchi wanachama kadhaa muhimu wa shirika la biashara duniani, WTO zikiwemo Marekani, Umoja wa Ulaya, Brazil na India zimeamua kufanya mazungumzo tarehe 5 mwezi Machi huko Geneva pamoja na Katibu mkuu wa WTO Bw. Pascal Lamy, zikijaribu kukwamua mazungumzo ya duru la Doha. Mwandishi wetu wa habari aliyeko Geneva hivi karibuni alimhoji balozi wa China aliyeko WTO Bw. Sun Zhenyu kuhusu mustakabali wa mazungumzo ya duru la Doha.
Mazungumzo ya duru la Doha yalisitishwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka jana kutokana na kuweko mgongano mkubwa kati ya pande mbalimbali kuhusu suala la biashara ya mazao ya kilimo. Baada ya kuingia mwaka 2007, Marekani na Umoja wa Ulaya zilionesha juhudi kuhusu suala hilo. Kwenye mkutano wa mwaka wa baraza la uchumi wa dunia uliofanyika mwishoni mwa mwezi Januari huko Davos, nchi 24 wanachama zilitoa taarifa ikiunga mkono kurejeshwa haraka kwa mazungumzo ya duru la Doha. Hivi karibuni mazungumzo kuhusu mazao ya kilimo pia yalifanyika mara kwa mara kati ya nchi muhimu wanachama, ambapo nia yao ya kisiasa imekuwa dhahiri. Bw. Sun Zhenyu alisema, matokeo hayo yanatokana na uhimizaji wa Marekani.
"rais George Bush wa Marekani ameeleza matarajio yake ya kurejeshwa kwa mazungumzo ya duru la Doha haraka iwezekanavyo, hatua hiyo inahusiana na hali ya kisiasa ya nchini Marekani. Serikali ya Bush haikupata mafanikio katika utatuzi wa masuala ya kimataifa yakiwemo ya Iraq na Afghanistan, kutokana na kuwa mambo ya kisiasa nchini Marekani yanadhibitiwa na chama cha Democrat, hivyo Bw Bush hawezi kupata mafanikio aliyotarajia, hivyo anaona huenda atapata baadhi ya mafanikio katika mazungumzo ya duru la Doha. hivyo amemtaka mwakilishi wa mambo ya biashara wa Marekani afanye juhudi zaidi."
Hivi karibuni WTO iliandaa mkutano na mabalozi wa pande husika ili kufahamu hali ilivyo ya sasa, Bw. Zun Zhenyu alisema, hivi sasa misimamo ya pande mbalimbali bado haijawa na mabadiliko makubwa, hususan viongozi wa Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya bado hazijaamua kupunguza masharti yao katika mazungumzo ya duru la Doha.
"Kwani kama ni katika mazungumzo ya pande nyingi, kila upande unashikilia msimamo wake wa zamani, isipokuwa mwakilishi amepata maagizo ya serikali ya nchi yake. Kwa hiyo maendeleo na mafanikio ya mazungumzo yanategemea maagizo ya serikali."
Bw. Sun Zhenyu alisema, sababu ya kuonesha juhudi kwa Umoja wa Ulaya, Marekani na nchi zinazoendelea ni kuwa, wakati uliobaki kwa mazungumzo ya pande mbalimbali siyo mwingi tena, zikitaka mazungumzo ya duru la Doha yapate mafanikio, kipindi cha nusu ya mwanzo ya mwaka huu ni muhimu sana. Kwanza ni kuhusu Marekani, uidhinishaji wa biashara kwa njia ya mkato ya rais unaishia mwezi Julai, ambayo inahusika na "mpango wa kisheria wa mazungumzo ya biashara huria". Kutokana na mpango huo, bunge la taifa linaweza kutoa kibali cha kukataa mikataba ya biashara iliyofikiwa kati ya rais na nchi au mashirika mengine, lakini halina uwezo wa kuirekebisha hata kidogo. Sasa bado haijafahamika kama rais ataweza kukabidhiwa madaraka hayo tena na bunge la taifa katika miaka mitano ijayo.
"Baadhi ya wabunge wa chama cha Democrat wanaweka mambo yanayofuatiliwa katika uidhinishaji wa shughuli za biashara, na kuzichukulia kama ni masharti, kwa mfano, masuala ya mazingira na vigezo vya wafanyakazi, chama cha Democrat kinataka serikali ya Bw Bush itoe ahadi, na matokeo ya mazungumzo ni lazima yakidhi matakwa yao. Na ni vibaya sana kuweka masharti hayo katika mazungumzo ya pande mbili, lakini masharti hayo yakiwekwa katika mazungumzo ya pande nyingi, basi mazungumzo ya Doha yanakwisha, kwani nchi zinazoendelea zinapinga kithabiti kuhusisha masuala ya vigezo vya wafanyakazi na mazingira katika mazungumzo ya duru hilo."
Pili ni Umoja wa Ulaya, katika nusu ya mwanzo ya mwaka huu, mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya ni Ujerumani, ambayo ni nchi kubwa kabisa katika Umoja wa Ulaya, Chansela wa Ujerumani Bw. Angela Merkel ni mwungaji mkono mkubwa wa mazungumzo ya duru la Doha, hivyo mjumbe wa biashara wa Umoja wa Ulaya Bw. Peter Mandelson anataka kupata mafanikio kwenye mazungumzo ya duru la Doha kwa kutegemea Ujerumani. Mbali na hayo waziri mkuu wa Uingereza Bw. Tony Blair pia anataka mazungumzo ya duru la Doha yamalizike mapema.
|