Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-06 16:33:24    
Weifang-maskani yangu ya pili

cri

Bw. Xu Zhongche ni mfanyabiashara kutoka Taiwan, ambaye hapo awali alifanya biashara ya vito nchini Thailand, na miaka zaidi ya 10 iliyopita alipanua shughuli zake za biashara hadi China bara. Kwenye mji wa Weifang wa mkoani Shandong ulioko sehemu ya mashariki mwa China, mwanzoni alikuwa anajishughulisha na biashara ya aina ya vito vinavyoitwa sapphire, na hapo baadaye alianzisha biashara ya ujenzi na uuzaji wa majengo, na alipata mafanikio katika shughuli hizo zote mbili.

Mji wa Weifang uko kwenye sehemu ya kati ya peninsula ya Shandong, ambao jina la mji huo linajulikana sana kutokana na utengenezaji wa tiara. Mbali na hayo mji huo ni mji wanaoishi kwa wingi wachina waliotoka kisiwani Taiwan, ambao kwa sasa idadi yao ni zaidi ya elfu 70. Tokea China ianze kutekeleza sera za mageuzi na ufunguaji mlango mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, sekta ya kilimo ya Weifang iliendelezwa kwa kasi, na iliwavutia wafanyabiashara wengi kutoka Taiwan kwenda huko kushughulikia biashara ya mazao ya kilimo na nchi za nje.

Lakini Bw. Xu Zhongche aliyetajwa hapo mwanzo, hakujishughulisha na mambo ya kilimo, bali alikwenda mji wa Weifang kutokana na johari ya buluu(sapphire).

"Siku moja katika wakati ule, rafiki yangu mmoja wa Singapore alinitembelea nyumbani akiwa na johari moja ya buluu, aliniuliza kama ninaifahamu, nilimwuliza aliipata kutoka wapi, aliniambia alipewa zawadi na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha jiolojia. Mwaka 1989 nilikwenda Beijing kumtafuta mwanafunzi yule, kwa kufuata habari nilizopata kutoka kwa watu mbalimbali husika, hatimaye nilifika kwenye mji wa Weifang mkoani Shandong."

Kutokana na johari hiyo, Bw. Xu Zhongche aliyekuwa hajatimiza umri wa miaka 30 alifika Weifang. Baada ya kufanya uchunguzi, aligundua kuwa huko kuna mawe mengi ya vito, hata mtu anaweza kuokota mawe ya vito ardhini. Wakazi wa huko hawakuwa na ufahamu kuhusu yale mawe, na waliyatumia kuwasha moto kwa kuyagonganisha.

Baada ya kuona mawe mengi yenye thamani, Bw. Xu Zhongche mwenye uzoefu wa miaka mingi katika biashara ya vito, alifanya uamuzi kuwekeza katika shughuli hiyo. Alianzisha kampuni ya vito inayojulikana kama "Mwangaza wa Buluu", aliandaa semina ya mafunzo ili kuwafundisha wafanyakazi teknolojia ya ukataji wa vito. Hivi sasa wakazi elfu kumi kadhaa wa wilaya ya Changle ya mji wa Weifang, ambako kuna mawe mengi ya vito, wanafanya kazi za sekta ya vito, uchimbaji wa mawe na ukataji vito vimekuwa nguzo ya sekta ya uzalishaji mali ya wilaya hiyo.

Sekta ya ujenzi na uuzaji majengo ilianza kupamba moto katika miaka saba iliyopita, kutokana na kushawishiwa na hali hiyo Bw. Xu aliamua kuacha shughuli za biashara ya vito. Lakini, mwanzoni alipatwa na matatizo mengi:

"Wakati ule nilinunua kiwanja katikati ya mji, nilijenga jengo moja la duka kubwa (department store). Shughuli za duka zilikuwa ni kitu kigeni kabisa kwangu, baada ya miezi michache tu nikapatwa na matatizo makubwa."

Huko karibu na duka la Bw. Xu Zhongxhe, kuna duka lingine kubwa, ambalo biashara yake ilikuwa ikendelea motomoto sana, lakini Bw. Xu alikuwa ni mbumbumbu katika biashara, na alishidwa kuendelea zaidi, na baada ya miezi miwili tu toka alipoanzisha shughuli za duka, ilimbidi afunge duka hilo. Alitafuta mara nyingi wanunuzi wa kununua duka lake, lakini alishindwa.

Kwa bahati wakati ule serikali ya mji wa Weifang iliona hali yake ya shida, ikamsaidia kutafuta mteja ambaye alilinunua jengo lile kwa Yuan milioni 70. Baada ya kuondokana na shida hiyo, Bw. Xu Zhongche hakufa moyo, muda si muda akawekeza katika kujenga jengo lingine lenye ghorofa 20 katikati ya mji. Kutokana na uzoefu wake, alikabidhi duka lililokuwa kwenye sehemu ya chini kwa kampuni moja inayouza bidhaa kwa rejareja na yenye uzoefu mzuri, wakati yeye mwenyewe alikuwa anasimamia nyumba za ofisi za jengo hilo. Safari hiyo alipata mafanikio pamoja na pato kubwa.

Tokea hapo Bw. Xu Zhongche anapenda kuishi katika mji wa Weifang, na alimwoa msichana mmoja wa huko miaka michache iliyopita, na wamezaa watoto wawili. Maisha ya furaha yanamfanya yeye kuchukulia mji wa Weifang kuwa maskani yake ya pili.

Akizungumzia uzoefu wake wa kuwekeza China bara, Bw. Xu anaona mafanikio yake yanatokana na mazingira bora ya uwekezaji yaliyoanzishwa na serikali ya huko. Habari zinasema ili kuvutia wafanyabiashara kutoka Taiwan waende kuwekeza katika mji wa Weifang, serikali ya huko ilibuni sera nyingi za nafuu kuhusu matumizi ya ardhi na ukusanyaji wa kodi, ofisi ya serikali ya huko inayoshughulikia mambo ya Taiwan pia inatoa huduma nzuri kwa wafanyabiashara wa Taiwan. Bw. Duan Wenzhong wa ofisi hiyo alipotoa maelezo kuhusu upande huo, alisema,

"Tunajitahidi kuongeza ufanisi wa kazi zetu kwa ajili ya wafanyabiashara wa Taiwan, na kuanzisha sekta ya uzalishaji inayohusika, uhakikisho mzuri wa utaratibu wa sheria, miundo mbinu ya kisasa na mazingira bora ya maisha."

Mazingira bora ya uwekezaji ya mji wa Weifang yamewavutia wafanyabiashara wengi, hivi sasa kuna viwanda zaidi ya 750 vilivyowekezwa na wafanyabiashara wa Taiwan kwenye mji wa Weifang, Weifang imekuwa sehemu yenye shughuli nyingi za kiuchumi na kibiashara na Taiwan kwenye sehemu ya kaskazini mwa China, ikienda sambamba na mji wa Xiamen ulioko sehemu ya kusini mwa China.

Kutokana na maendeleo mazuri ya viwanda vya wafanyabiashara wa Taiwan, maonesho ya biashara ya Shandong na Taiwan, ambayo hufanyika kila mwaka, yanafanyika katika mji wa Weifang, hadi sasa maonesho hayo yamefanyika mara 12. Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa sera ya chama cha Qinmin cha Taiwan Bw. Zhang Xianyao, ambaye hivi karibuni alishiriki kwenye maonesho ya 12 ya Shandong na Taiwan alisema, mustakabali wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Shangdong na Taiwan katika siku za baadaye utakuwa mzuri zaidi. Alisema,

"Mazingira ya uwekezaji ya mkoa wa Shangdong ni mazuri, Shandong imeendelea sana na kupata maendeleo kuliko nilivyofikiria. Hususan ni mazingira ya uwekezaji ya Shandong, mkoa huo una ardhi nzuri pamoja na nguvukazi nyingi, licha ya hayo viongozi wa mkoa wa Shandong wana mtizamo wa kimaendeleo sana, mambo hayo matatu ni vitu ambavyo wafanyabiashara wa Taiwan wanavihitaji sana kwa hivi sasa."

Ili kuhimiza uwekezaji wa wafanyabiashara wa Taiwan, mwezi Machi mwaka 2005 mji wa Weifang ulianzisha jumuiya ya wafanyabiashara wa Taiwan, Bw. Xu Zhongche alichaguliwa kuwa kiongozi wa awamu ya kwanza wa jumuiya hiyo, ambayo inatoa misaada mingi kwa maisha ya wafanyabiashara wa Taiwan.

Idhaa ya kiswahili 07-03-06