Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-07 10:13:39    
Waziri mkuu wa China atoa ripoti ya kazi za serikali

cri

Mkutano wa mwaka wa Bunge la umma la China umefunguliwa tarehe 5 Machi asubuhi hapa Beijing, ambapo waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao ametoa ripoti ya kazi za serikali. Ikilinganishwa na ripoti za miaka iliyopita, ripoti ya mwaka huu imekuwa na mabadiliko mengi makubwa, ambayo si kama tu imeonesha utekelezaji wa miaka mingi mfululizo wa sera za serikali kuu, bali pia imeeleza njia zenye ufanisi za kukabiliana na matatizo yaliyopo sasa.

Maelezo kuhusu utekelezaji wa miaka mfululizo wa sera za serikali kuu yamewavutia watu zaidi. Katika mwaka mpya, China itaendelea kutekeleza sera za fedha kwa hatua madhubuti, kuendelea na juhudi za kutimiza lengo la kubana matumizi na kuhifadhi mazingira lililotolewa na serikali kuu mwaka jana, vilevile kutekeleza sera mpya kuhusu kufuta kero na ada za masomo kwenye elimu ya lazima vijijini pamoja na kutenga fedha zaidi kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu vijijini. Aidha Waziri mkuu Wen Jiabao pia amewaeleza wajumbe wa Bunge la umma kuhusu hali ya maendeleo ya kazi ya serikali kuu kuhusu kutatua suala la kuchelewesha mishahara ya wakulima vibarua, kazi hiyo ilianza kufanyika mwaka 2004. Bwana Wen Jiabao amesema:

Kazi hiyo imekamilika kimsingi, mishahara iliyocheleweshwa ya wakulima vibarua ipatayo Yuan bilioni 33 imelipiwa. Na serikali imetunga na kutekeleza sera na hatua za kutatua masuala ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, sera na hatua hizo zimelinda haki na maslahi halali ya wakulima vibarua.

Wasomaji wa China kwenye mtandao wa internet waliposoma ripoti aliyotoa waziri mkuu Wen Jiabao wengi wao wamesema, ni dhahiri kuwa ripoti hiyo inaeleza wazi matatizo yaliyopo sasa. Katika ripoti hiyo, waziri mkuu alipofanya majumuisho ya kazi za serikali za mwaka jana, pia alieleza wazi kuwa, lengo lililotolewa na serikali mwanzoni mwa mwaka jana kuhusu kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira halikuweza kutimizwa. Ili kuendelea kusukuma mbele kazi hiyo, kwa mara ya kwanza China imeweka sharti la kwanza kwa ongezeko la uchumi, yaani kwenye msingi wa kuboresha miundo ya uchumi, kuongeza ufanisi na kupunguza matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira, lengo la pato la taifa la China mwaka huu bado ni asilimia 8 . Juu ya hiyo, waziri mkuu Wen Jiabao amesema:

Serikali imetoa lengo la asilimia 8 la ongezeko la thamani ya jumla ya uzalishaji nchini mwaka huu baada ya kuzingatia mahitaji na mambo yanayoweza kutokea, muhimu zaidi ni kwa ajili ya kuwaelekeza watu wa pande mbalimbali watekeleze kwa makini wazo la kujipatia maendeleo kwa njia ya kisayansi, na kuweka mkazo katika kuboresha miundo ya uchumi, kuongeza ufanisi, kupunguza matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu, wasije wakatafuta zaidi kasi ya ongezeko bila kuwa makini, ili tutimize lengo la kupata maendeleo mazuri na ya haraka ya uchumi wetu.

Katika ripoti aliyotoa waziri mkuu Wen Jiabao, maelezo mengi yanahusu hatua mpya kadhaa zilizo muhimu kabisa za serikali ya China mwaka huu kwa ajili ya kutatua matatizo yanayowakabili wananchi. Waziri mkuu Wen Jiabao alipofahamisha alisema:

Kuanzia muhula mpya wa mwaka huu, umeanzishwa na utakamilishwa kwa utaratibu kuhusu udhamini wa serikali na msaada kwa masomo katika vyuo vikuu, vyuo vya kazi za ufundi na shule za sekondari za kazi za ufundi; wakati huo huo kutekeleza zaidi sera ya serikali kutoa mikopo ya kuwasaidia wanafunzi kukamilisha masomo, ili wanafunzi wa familia zenye matatizo ya kiuchumi waweze kusoma katika vyuo vikuu, au kupewa elimu ya kazi za ufundi.

Zaidi ya hayo, waziri mkuu Wen Jiabao pia amejulisha kuwa, mwaka huu serikali kuu itaanzisha utaratibu wa kuhakikisha kiwango cha chini kabisa cha maisha ya wakazi wa mijini na vijijini kote nchini, hii ni hatua nyingine kubwa ya kuimarisha kazi zinazohusu kilimo, vijiji na wakulima, na kujenga jamii yenye masikilizano.

Katika ripoti yake ya kazi za serikali, waziri mkuu Wen Jiabao pia ameeleza sera ya kidiplomasia ya China na sera kuhusu mikoa ya Hong Kong na Makau pamoja na suala la Taiwan. Masuala mengi kuhusu sekta nyingi na yaliyoelezwa vilivyo zaidi, hayakuonekana katika ripoti kama hiyo kwa miaka iliyopita.

Idhaa ya Kiswahili 2007-03-05