Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-07 18:57:16    
Mapishi ya kabichi ya kichina iliyolowekwa kwenye achali pamoja na nyama ya kuku

cri

Mahitaji:

Kabichi ya kichina iliyolowekwa kwenye achali gramu 300, pilipili mboga gramu 100, nyama ya kuku gramu 500, chumvi gramu 5, unga wa pilipili manga gramu 5, sukari gramu 5, wanga gramu 10, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu tangawizi, na pilipili hoho.

Njia:

1. kata nyama ya kuku iwe vipande, vipande na kasha ichangane pamoja na chumvi na wanga. Kata kabichi ya kichina iliyolowekwa kwenye achali na pilipili mboga vipande vipande.

2. washa moto na tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga kwa haraka halafu vipakue. Washa moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi na pilipili hoho, korogakoroga, halafu tia vipande vya pilipili mboga na kabichi ya kichina iliyolowekwa kwenye achali na korogakoroga, baada ya hapo tia chumvi, sukari na korogakoroga halafu tia vipande vya nyama ya kuku, halafu tia wanga wa pilipili manga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.