Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-12 19:12:02    
Manowari za China zashiriki kwenye luteka ya nchi nyingi

cri

Wasikilizaji wapendwa, manowari za nchi nane zilifanya luteka inayojulikana kama "Amani--07" kwenye sehemu ya kaskazini mwa bahari ya Uarabuni karibu na Pakistan. Manowari za jeshi la ukombozi la umma la China zilishiriki kwenye luteka hiyo na kuhitimisha aina mbalimbali za shughuli za luteka hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la baharini la China kushiriki luteka ya baharini ya nchi nyingi.

"Onyo la kujiweka tayari kwa mapambano kwa ngazi ya kwanza, onyo la mapambano ya luteka!"

luteka ya baharini ya nchi nyingi ilianza tarehe 8 mwezi Machi kwa sauti ya onyo ya king'ora. Manowari 12 za Pakistan, Bangladesh, Ufaransa, Italia, Uingereza, Malaysia, China na Marekani zilishiriki kwenye luteka yenye aina 20 za shughuli za kupambana na magaidi.

Mashambulizi ya kweli ya mizinga mikubwa ni shughuli muhimu zilizofanywa na manowari za China katika luteka hiyo. Shabaha za mizinga mikubwa ilikuwa ni maboya ya plastiki yenye rangi ya machungwa yaliyokuwa kwenye sehemu ya mbali na karibu. Manowari mbili za jeshi la baharini la China za "Sanming" na "Lianyungang" zilipiga shabaha hizo. Manowari ya "Sanming" ilipata shabaha yake iliyoko kwenye sehemu ya mbali, kwa kufuata, kanali Qiu Yanpeng aliyeko kwenye manowari ya "Lianyungang", alitoa amri ya kulipua shabaha ile ya karibu.

Muda si muda, habari kuhusu kubomolewa kwa shabaha ile iliyoko kwenye sehemu ya karibu ililetwa, ambayo ilifikishwa kwa haraka kwa jeshi la baharini la Uingereza, ambalo linaongoza luteni hiyo.

""Vizuri sana! Hiyo ni kumbukumbu nzuri. Shabaha zote zimezamishwa, moja ilizamishwa na 'Sanming' na nyingine ilizamishwa na manowari ya 'Lianyungang'. Hayo ni mafanikio makubwa, safi sana!"

Kutokana na mpango wa luteni hiyo, tarehe 9 alasiri, jeshi la baharini la China liliongoza shughuli za kuokoa watu baharini. Hiyo ni mara ya kwanza kwa jeshi la baharini la China kuongoza manowari za nchi nyingi kufanya shughuli za uokoaji baharini. Katika luteka hiyo, vitu viwili vyenye maumbo ya watu vilitumbukizwa baharini kuonesha kama wanamaji wawili walitumbukia majini kwa bahati mbaya, manowari ya China ya 'Lianyungang' ilitoa amri ya kutaka manowari zote zianze kutafuta "watu wale waliotumbukia majini".

Baada ya nusu saa, shabaha la kwanza iligunduliwa na manowari ya jeshi la baharini la Bangladesh. Baada ya muda tena, shabaha ya pili iligunduliwa na manowari ya Pakistan.

Mkuu wa kundi la manowari za China zilizoshiriki kwenye luteka Luo Xianlin baada ya kumaliza shughuli za kufafuta na kuokoa watu baharini alisema, jeshi la baharini la China limebuni mpango kamili sana ili kuhakikisha mafanikio ya shughuli hizo.

Katika luteka ya baharini iliyofanyika kwa siku nne, manowari za nchi nyingi pia zilifanya mazoezi ya kuzuia ndege zilizotoka mbali, kuweka ulinzi dhidi ya mashambulizi ya angani, kufanya doria ya kuvinjari wakati wa usiku na kupeleka mahitaji.

Ofisa mkuu aliyeelekeza katika luteka hiyo wa kundi la manowari za China Qiu Yanpeng alisema, kutokana na luteka hiyo, kundi hilo la manowari la China limeongeza uwezo wake wa kupambana na magaidi baharini na kuimarisha urafiki kati ya China na majeshi ya baharini ya nchi nyingi.