|
Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 12 lilifanya mkutano wa kwanza katika makao yake makuu mjini Geneva.
Mkutano huo wa wiki tatu utajadili ripoti kumi zilizotolewa na mashirika yaliyo chini yake, kukagua kazi ya kikundi cha kupima hali ya nchi zote na kukagua hali ya utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa katika mikutano minne maalumu ya baraza hilo. Licha ya hayo pia utajadili kanuni za kazi mbalimbali za baraza hilo na kufanya kongamano kuhusu unyanyasaji kwa watoto na ukiukaji wa haki za walemavu.
Baraza la haki za binadamu lililoanza kufanya kazi tokea mwezi Juni mwaka jana ni mafanikio makubwa katika mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Kutokana na kuwa hapo kabla tume ya haki za binadamu ilikuwa ni chombo cha kisiasa cha nchi za magharibi kuzishinikiza nchi zinazoendelea, na lilikuwa ni jukwaa la mapambano ya kisiasa kati ya kusini na kaskazini, kwa hiyo ilipoteza heshima yake, na mwaka jana ilitangaza kuvunjwa. Ikilinganishwa na tume ya zamani iliyokuwepo kwa miaka 60, baraza hilo jipya lina maendeleo katika mambo mawili, moja ni kuwa uwakilishi wake umekuwa mkubwa, na imeamua utaratibu wa kupima nchi zote kila baada ya muda fulani badala ya kuchagua nchi fulani tu na kupima kwa vigezo tofauti. Pili ni idadi ya nchi zinazoendelea katika baraza hilo imeongezeka na imefuta hadhi ya uanachama wa daima, nchi wanachama zinaweza tu kuwa na vipindi viwili vyenye miaka sita. Hapo kabla tume ya haki za binadamu ilifanya mkutano wa wiki sita kila mwaka na sasa baraza hilo limeamua kufanya mkutano mara tatu kila mwaka na kila mkutano hautapungua muda wa wiki 10.
Mwaka jana baraza la haki za binadamu lilifanya mikutano mara tatu katika miezi ya Juni, Septemba na Novemba, na ilipitisha maazimio kadhaa ya kulinda haki za binadamu, na lilifanya mkutano maalumu kwa ajili ya migogoro kati ya Afghanistan na Israel. Lakini kutokana na kuwa baraza hilo halijawa na muda mrefu tokea liundwe, kanuni mpya bado ziko katika kipindi cha kutungwa na kazi yake bado haijakuwa katika hali ya kawaida. Kwa mujibu wa mpango, kanuni za kupima hali ya nchi zote zitatangazwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Mkutano wa kwanza wa baraza hilo mwaka jana uliamua kurefusha muda wa madaraka ya wataalamu na watoa ripoti wa baraza hilo kwa mwaka mmoja, uamuzi huo ulisababisha malalamiko ya nchi zinazoendelea kwa sababu watu hao wamewekwa kulenga nchi zinazoendelea tu. Mkutano wa sasa utajadili ripoti zilizotolewa na kikundi cha wataalamu kuhusu haki za binadamu nchini Palestina, Lebanon, Burundi, Liberia na Sudan.
Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Mexico katika Umoja wa Mataifa Bw. Luis Alfonso De Alba, alisisitiza kuwa baraza la haki za binadamu ni lazima lifanye ushirikiano wa kweli na kubadilisha hali ya zamani ya "kuchagua chagua na kuweka vigezo tofauti" na kuhakikisha uadilifu na haki sawa.
Hapo awali tume ya haki za binadamu ilipoanzishwa ilitangaza kuwa tume hiyo itatatua haki za binadamu kwa kufanya mazungumzo na ushirikiano. Lakini kutokana na kuwa katika haki za binadamu maslahi yanayofuatiliwa na nchi zinazoendelea na zilizoendelea ni tofauti na yanahusu utamaduni tofauti na dini tofauti, migongano kati ya pande mbili inaendelea kuwa mikubwa. Katika mikutano kadhaa iliyofanyika mwaka jana nchi zinazoendelea zilipitisha maamuzi ya kuishutumu Israel kuikalia ardhi ya Palestina na kukiuka haki za binadamu, lakini nchi za magharibi zinashinikiza nchi zinazoendelea katika suala la Darfur. Kutokana na hali hiyo mkutano wa sasa hakika utakuwa na migongano mipya.
Idhaa ya kiswahili 2007-03-13
|