Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-14 20:29:38    
Mapishi ya kaa, vitunguu maji na tangawizi

cri

Mahitaji

Kaa gramu 500, vitunguu maji gramu 150, tangawizi gramu 25, vitunguu saumu gramu 5, mvinyo wa kupikia gramu 15, mchuzi wa sosi gramu 10, maji ya wanga gramu 10, sukari gramu 3, mafuta ya ufuta gramu 2, chumvi gramu 3, M.S.G gramu 5, pilipili manga gramu 5.

Njia

1. Mkate kaa awe vipande viwili. Kata vitunguu maji na tangawizi iwe vipande vipande.

2. washa moto, tia mafuta ya kupikia kwenye sufuria mpaka yawe joto la nyuzi 60, baada ya hapo tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi na vitunguu saumu , korogakoroga, kasha tia vipande vya kaa kwenye sufuria, mimina mvinyo wa kupikia, maji, weka chumvi, sukari, mchuzi wa sosi na M.S.G, na korogakoroga, baada ya kuchemka, tia mafuta wa kupikia kidogo, mafuta ya ufuta na pilipili manga, korogakorga, mimina maji ya wanga na kasha pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.