Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-19 15:48:34    
Kutalii kwenye mji wa Xuancheng unaozalisha vyombo muhimu vinavyotumika kwenye vyumba vya kusomea

cri

Brashi ya kichina ya kuandikia, wino, karatasi na jiwe la kuchanganyia wino ni vyombo muhimu vya jadi nchini China. Kadiri idadi ya watu wanaopenda michoro ya picha na maandiko ya maneno ya kichina inavyoongezeka, ndivyo miji yenye umaalum wa utamaduni wa jadi wa China inavyofuatiliwa zaidi na watalii. Leo nitawafahamisha kuhusu mji wa Xuancheng, mkoani Anhui, unaojulikana kwa kuwa mahali penye asili ya uzalishaji wa vyombo muhimu katika chumba cha kusomea. Vyombo hivyo vinachukuliwa kuwa ni mabaki yenye thamani kubwa ya utamaduni kwa ubora wake na ufundi mkubwa wa utengenezaji.

Karatasi ya Xuanzhi ni aina ya karatasi maalumu inayofaa kutumika kwa michoro ya picha na maandiko ya maneno ya kichina kwa kutumia brashi, karatasi ya aina hiyo ni laini lakini ni imara, na hazichujuki kwa muda mrefu. Hivi sasa karatasi ya Xuanzhi zimekuwa karatasi pekee zinazotumika katika michoro na maandiko ya jadi ya China. Kampuni ya Xuanzhi ya China ya wilaya ya Jing ya Xuancheng, ambayo inaongoza katika sekta ya uzalishaji wa karatasi za Xuanzhi nchini China, inajulikana hata katika sehemu za mbali. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. She Guangbin alisema,

"Huko ni sehemu ya asili ya karatasi ya Xuanzhi inayohifadhiwa na serikali, mazingira ya kijiografia ya huko ni ya kipekee, ambapo kuna maji bora ambayo ni raslimali maalumu, lakini kitu muhimu zaidi ni ufundi wa jadi."

Bw. She Guangbin alisema, karatasi za Xuanzhi zinatengenezwa kwa mali-ghafi maalumu zikiwa ni pamoja na magamba ya aina ya miti ya wingceltis pamoja na mabua ya mpunga wa Shatian, ufundi unaotumika katika utengenezaji wa karatasi hizo ni mkubwa, ambao ni kwa hatua zaidi ya 180, na kazi katika hatua zote hizo zinafanywa kwa mikono.

"Sisi tumekuwa na kundi kubwa la mabingwa wa uzalishaji karatasi za Xuanzhi, ufundi mwingi unafundishwa kazini humo, wala ni vigumu kuandikwa kwa maneno. Kila moja ya kazi za hatua zaidi ya 180 inahusika na sifa ya karatasi, ufundi huo wa jadi ulioorodheshwa na serikali mwaka 2006 ni kuwa mabaki ya kiutamaduni yasiyo ya vitu, ufundi huo unafundishwa kizazi hadi kizazi."

Ukweli ni kuwa ni vigumu kuona karatasi za Xuanzhi za bandia, kwani ni shida kubwa kuzalisha karatasi bora inayofanana na Xuanzhi nje ya mazingira ya kimaumbile ya wilaya ya Jing. Aidha mabingwa wa uzalishaji karatasi za Xuanzhi wanatembelea makumbusho ya historia mara kwa mara ili kuangalia michoro ya picha ya zaidi ya miaka mia na ya miaka elfu moja iliyopita, hasa ni kuchunguza hali ya wino ulioko kwenye karatasi hizo ili kupata mwangaza wa kuboresha karatasi za Xuanzhi wanazozalisha.

Licha ya karatasi za Xuanzhi, brashi ya kuandikia inayozalishwa na wilaya ya Jing pia ni maarufu sana. Brashi ya kuandikia ni chombo cha jadi kwa michoro ya picha na maandiko ya Kichina. Kalamu zilizotengenezwa kwa mabua ya matete na kalamu zilizotumika zamani barani Ulaya zilitoweka, lakini brashi za kuandikia za kichina ingawa zilivumbuliwa miaka mingi iliyopita, lakini bado mpaka sasa zinatumika. Brashi za Xuanbi ni brashi ya kuandikia iliyoanza kutumika mapema zaidi kuliko brashi za aina nyingine za kichina, ambazo zinajulikana kwa kutumia mali-ghafi bora na ufundi mkubwa. Kiongozi wa taasisi ya utafiti wa brashi za kuandikia za Xuanbi ya wilaya ya Jing, Bw. She Zhengjun alisema, utengenezaji wa brashi za Xuanbi ni kwa uangalifu mkubwa, brashi tofauti lazima zinatumia manyonya ya wanyama tofauti.

"Brashi zinazojulikana kwa Langhaobi zinatengenezwa kwa manyoya ya mkia wa mnyama anaiyeitwa Kicheche. Brashi zinatumika kwa uchoraji wa michoro mikubwa ya milima na mito zinatengenezwa kwa manyoya ya ngiri, ambayo ni ngumu kidogo, na zinafaa kutumika kwa uchoraji wa michoro ya aina hiyo."

Wino mweusi unatumika sana kwa sanaa ya maandiko ya kichina na uchoraji michoro ya picha ya jadi, wino wenyewe wa aina hiyo ni kitu cha sanaa ya kiutamaduni. Utengenezaji wa wino huo umekuwa na historia ya miaka zaidi ya elfu tano. Wino bora kabisa wa nchini China ni wino unaojulikana kwa Huimo, hivi sasa mji wa Xuancheng umekuwa mahali pa uzalishaji wa wino wa Huimo, hususan kwenye sehemu wilaya ya Jixi.

Kwenye wilaya ya Jixi kuna kampuni moja maarufu ya wino inaojulikana kama Hukaiwen, ambayo kimekuwa na historia ya zaidi ya miaka mia mbili, na ni kiwanda kikubwa chenye teknolojia ya kiwango cha juu kinachoongoza katika sekta ya uzalishaji wino nchini China. Kampuni hiyo bado inazalisha wino kwa kutumia ufundi wa jadi na kwa mikono. Malighafi zinazotumika kuzalisha wino ni masizi ya moshi wa vijiti vya miti ya misonobali vinavyowaka moto, ambayo yanachanganywa na gundi na dawa fulani, yakawa udongo wa ufinyanzi uliochanganywa maji, baada ya kukandwa na kutwangwa kwa muda, yanawekwa ndani ya kulibu, na baada ya kukaushwa yakawa vipande vya wino vyenye maumbo ya aina mbalimbali. Ili kufanya michoro na maneno yaliyoandikwa kuwa na harufu nzuri, wino unatiwa aina fulani za dawa za mitishamba, tena maneno yaliyoandikwa na michoro iliyochorwa itaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi bila kuharibiwa na vidudu. Vipande hivyo vya wino baada ya kukaushwa juani, vinachorwa michoro juu yake kwa rangi ya dhahabu ili kuvifanya vipendeze zaidi.

Kuandika maneno au kuchora michoro kwa wino uliotengenezwa kuwa vipande, kwanza kabisa inatakiwa kuchanganya wino huo na maji. Hivyo jiwe la kuchanganyia maji ni chombo kinachohitajika sana. Mji wa Xuancheng uko karibu na wilaya ya Sh?ambayo inajulikana sana kwa uchimbaji wa mawe ya kuchanganyia wino, na kumekuweko uhusiano mkubwa tangu zamani kati ya sehemu hizo mbili, kwa kuhusishwa na vyombo vinne muhimu katika chumba cha kusomea, mji wa Xuancheng pia umekuwa sehemu muhimu inayouza mawe ya kuchanganyia wino kwa sehemu za nje.

Kiongozi wa jumuiya ya vyombo vinne muhimu katika chumba cha kusomea ya mji wa Xuancheng Bw. Jiang Xianjin alisema, vyombo vinne muhimu katika vyumba vya kusomea ni matokeo ya busara za watu wa China, ambavyo si kama tu ni vyumba vya kiutamaduni katika miaka elfu kadhaa iliyopita, bali pia ni alama ya utamaduni wa jadi na ustaarabu wa taifa la China.

"Vyombo vinne muhimu katika vyumba vya kusomea vina mustakabali mzuri, kwani wachina wana uhusiano mkubwa navyo, hivyo tumekuwa na wazo la kuiendeleza vizuri sekta hiyo na kukuza kwa mfululizo utamaduni wa jadi wa China. Vitu hivyo vya China vimekuwa mchango tuliotoa kwa maendeleo ya binadamu, tunataka kuvifanya vitoe mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya maendeleo ya ustaarabu wa binadamu kutokana na jitihada zetu.

Idhaa ya kiswahili 2007-03-19