Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-21 15:34:43    
Mapishi ya samaki kwa michuzi mitatu

cri

Mahitaji:

Samaki mmoja, chumvi vijiko viwili, , sukari vijiko vitatu, mchuzi wa kupikia vijiko viwili, sosi ya chaza vijiko vitano, mchuzi wa sosi vijiko viwili, pilipili manga kijiko kimoja, sosi ya nyanya vijiko vitatu, sosi ya sukari vijiko vitano, unga wa pilipili hoho vijiko viwili, M.S.G kijiko kimoja, kiazi chekundu kimoja, kitunguu kimoja, karoti moja, vipande viwili vya vitunguu saumu, kiasi kidogo cha tangawizi,

Njia :

1. kata samaki awe vipande, koroga pamoja na chumvi, pilipili manga, vipande vya vitunguu maji, tangawizi, vitunguu saumu, M.S.G, mvinyo wa kupikia, na mchuzi wa sosi.

2. koroga sosi ya sukari, sosi ya nyanya, sosi ya chaza, sukari, chumvi kuwa mchuzi. Mimina maji kwenye sufuria, tia sukari, asali, korogakoroga, tia mchuzi, korogakoroga, halafu upakue. Koroga vipande vya karoti, kiazi chekundu, kitunguu pamoja na chumvi, M.S.G, poda ya pilipili hoho, ya unga pilipili manga. Tia mafuta kwenye sufuria, halafu weka vipande hivyo, chemsha kwa mvuke kwa dakika 15, weka vipande vya samaki, endelea kuchemsha kwa mvuke kwa dakika 5. korogakoroga mchuzi mpaka uwe rojorojo, halafu mimina kwenye samaki.