Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-26 15:08:40    
Kutalii kwenye bonde la Zhangbu mkoani Guizhou

cri

Mandhari nzuri ya mawe yenye maumbo ya ajabu, mashimo yenye maji ya kina kirefu pamoja na miti mbalimbali ya kupendeza kwenye bonde la Zhangbu lililoko katika wilaya ya Pingtang mkoani Guizhoi, sehemu ya kusini magharibi mwa China inawavutia watalii wengi.

Bonde la Zhangbu lililoko upande wa kusini mwa wilaya ya Pingtang, lina urefu wa kilomita 8. Watu wanapoingia kwenye bonde hilo, wanavutiwa mara moja na mandhari nzuri bonde hilo, miti mingi mikubwa imeota kwenye kando mbili za mto Zhengbu, ambao maji yake ni safi sana, mimea mingi ya kale inastawi sana kwenye bonde hilo, na magenge marefu yaliyochongoka yanaonekana huku na huko.

Mawe yaliyoko kwenye bunge la Zhangbu ni yenye maumbo ya ajabu sana, hususan mawe mawili makubwa yaliyoko chini ya miti miwili mikubwa yenye urefu wa mita zaidi ya kumi kwenye kando ya mlima, mawe hayo ni kama yenye maneno ya lugha ya kabila la wahan. Mtu aliyegundua mawe hayo yenye maneno ni mkulima wa huko Bw. Wang Guofu, alipojikumbusha hali ile ya zamani, alisema,

"Mwezi Juni mwaka 2002, Nilipokuwa napita huko niliona kama kuna maneno kadhaa kwenye mawe hayo, niliangalia sana niliona michoro ile ni kama maneno kadhaa ya lugha ya kabila la wahan."

Mwandishi wetu wa habari aliona maneno kadhaa, ambayo baadhi yake yamepangwa pamoja kama sentensi moja inayoeleweka maana yake. Baadhi nyingine ni kama herufi za Lugha ya Kingereza na michoro ya maneno ya Kiarabu. Je maneno hayo ni ya kimaumbile au yalichongwa na watu? Kikundi cha wachunguzi kilichoundwa na wataalamu zaidi ya kumi wa jiolojia walikwenda huko kufanya uchunguzi kuhusu maneno hayo yaliyoko kwenye mawe hayo mawili. Hatimaye wataalamu walisema, maneno yaliyoko kwenye mawe mawili ya bonde la Zhangbu ni ya kimaumbile, ambayo yalikuweko tokea miaka zaidi ya milioni 200 iliyopita. Kiongozi wa kikundi hicho cha uchunguzi, Profesa Li Tingdong alisema,

"Maneno hayo yalikuweko kabla ya miaka kiasi cha milioni 270 iliyopita, maneno hayo yaliundwa na vipande vidogo sana vya viumbe, ambavyo ni vigumu zaidi kuliko mawe yale, hivyo baada ya mawe kuliwa maji ya mvua na hewa katika miaka mingi iliyopita, vipande vidogo vya viumbe vilivyoko kwenye mawe vikajitokeza nje, jinsi ilivyo ni kama maneno yaliyochongwa kwa kisu, sentensi ile ya maneno ilijitokeza kwa bahati tu.

Profesa Li alisema, michoro ya maneno hayo ilitokeza kwa bahati tu, ambayo uwezekano wake ni sehemu moja kwa trilioni 100. Kwa hiyo mawe hayo mawili yenye maneno kabisa yanaweza kusifiwa kama ni moja ya maajabu ya duniani. Mawe hayo yenye maneno yanavutia idadi kubwa ya watalii kwenda kuyaangalia. Bw. Bi alisafiri mahsusi kwenda kuangalia mawe hayo mawili, alisema,

"Maneno yaliyoko kwenye mawe yanaonekana siyo ya kimaumbile, bali ni kama maneno yaliandikwa na malaika."

Kwenye bonde la Zhangbuxia kuna mawe mengi yasiyo ya kawaida kama mawe hayo yenye maneno. Kwenda mbele kwa kufuata mto ule kwa kiasi cha dakika kumi kutoka kwenye mawe yenye maneno, utaweza kuona sehemu nyingine yenye ajabu, kwenye mteremko wa mlima kuna jiwe kubwa lenye umbo la mstatili lenye mwinuko wa nyuzi 40 hivi, kuna matufe mengi ya mawe yaliyoko kwenye jiwe hilo yanaonekana kama yamewekwa juu na watu. Ukubwa wa matufe hayo karibu ni wa namna moja, ambayo kama yalisambazwa kwenye jiwe lile kubwa bila utaratibu, nusu yake iko juu na nusu iliyobaki ya tufe iko ndani ya jiwe, matufe hayo ya rangi ya kijivu nyepesi ni laini kama kioo. Ni kama mawe yenye maneno, matufe hayo pia yaliumbika zamani za kale.

Karibu na kundi la matufe ya mawe, kuna shimo la maji, ambalo maji yake ni maangavu kama kioo. Kwenye sehemu yenye maji machache, watoto kadhaa wa kike wa sehemu ya huko wakiwa miguu mitupu walisimama kwenye maji, muda si muda kundi kubwa la watu wakavutiwa kwenda huko kuangalia. Mwongoza watalii dada Li Ya alituambia, akisema,

"Wanacheza kwenye maji! Kwenye Mto huo kuna samaki wengi wadogo, mtu akisimama au kulala kwenye maji kwa utulivu, samaki wadogo hufika kwenye miguu yake na kuibusu."

Walijitokeza watalii wachache, ambao walivua viatu na kusimama kwenye maji, hata kabla ya kutimia dakika moja, kulikuwa na samaki wengi waliokwenda kwenye miguu yao na kugusa miguu kwa midomo yao.

Mazingira bora yenye milima mikubwa na maji maangavu, ni mahali pazuri sana kwa ukuaji wa mimea pori. Karibu na shimo la maji kuna msitu mmoja wenye eneo la kilomita 5 za mraba. Miti ya kwenye msitu huo Mihenzirani inakua katika miezi yote ya mwaka, na inaonekana kama ni zulia moja kubwa ardhini. Miti hiyo inaota katika nchi za Brazil, Chile na China, lakini ni nadra sana kuonekana kwa msitu wa mihenzirani kama wa bonde la Zhangbuxia.

Miti mikubwa sana inaonekana kwenye sehemu nyingi za bonde la Zhangbuxia. Kati ya miti hiyo mikubwa, kuna miti mikubwa miwili inayoota karibu sana, ambayo jiwe moja kubwa liko katikati ya miti, jinsi ilivyo ni kama mume na mke wakiwa wamepakata mtoto wao mpendwa. Licha ya miti hiyo, kuna baadhi ya miti, ambayo majani yake yanatanuka mchana na kufumba wakati wa usiku, na kufanya watu kuona kuwa ina akili.

Kutembela bonde la Zhangbuxia na kuangalia mawe, maji na miti ya ajabu, wakati mwingine watu wanaweza kusikia nyimbo nzuri za kiutamaduni za huko, inafanya watu kuburudika sana. Haya basi wasikilizaji wapendwa, mliyokuwa mkisikia leo, ni maelezo kuhusu bonde la Zhangbuxia, kipindi hiki cha utalii kinaishia hapa kwa leo, tutakuwa nanyi wiki ijayo wakati kama huu msikose kutusikiliza, kwaherini.

Idhaa ya kiswahili 2007-03-26