Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-26 19:09:45    
Hu Jintao ahojiwa na vyombo vya habari vya Russia kabla ya kufanya ziara nchini Russia

cri

Rais Hu Jintao atafanya ziara ya kiserikali nchini Russia kuanzia tarehe 26 hadi 28 mwezi Machi, na kushiriki kwenye sherehe ya kuzindua "mwaka wa China". Kabla ya ziara yake rais Hu Jintao alihojiwa na waandishi habari wa vyombo 6 vya habari vya Russia hapa Beijing likiwemo shirika la habari la Interfax. Rais Hu Jintao anaamini kuwa, ziara hiyo hakika itaimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Russia.

Mwaka huu ni mwaka muhimu katika kuimarisha maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia, uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa nchi hizo mbili unaingia kwenye kipindi cha pili cha miaka kumi. Kwa kufuatia shughuli za "mwaka wa Russia" zilizofanyika mwaka jana nchini China, shughuli za "mwaka wa China" zitafanyika kwa mara ya kwanza nchini Russia. Rais Hu Jintao atafanya ziara nchi Russia katika wakati huo muhimu. Alisema,

"Ninatarajia kuwa na mazungumzo na rais Putin katika ziara hiyo nchini Russia, kubadilishana maoni kuhusu kuimarisha uhusiano wa ushirikiano wa nchi mbili na masuala mengine yanayofuatiliwa na pande hizo mbili kwa pamoja, na kushiriki pamoja na rais Putin kwenye sherehe za ufunguzi wa 'mwaka wa China', na 'maonesho ya taifa la China". Ninaamini kuwa kutokana na jitihada za pande hizo mbili, uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaimarishwa zaidi."

Hivi sasa uhusiano wa China na Russia umefikia kwenye kiwango cha juu kisichowahi kuonekana hapo kabla. Nchi mbili zimekuwa na ushirikiano mkubwa na kupata mafanikio mengi katika mambo muhimu ya kikanda na kimataifa yakiwemo ya suala la nyuklia la peninsula ya Korea na suala la nyuklia la Iran, na zimefanya kazi muhimu katika kulinda amani na utulivu wa dunia.

Rais Hu Jintao alisisitiza kuwa, kuhimiza kithabiti maendeleo ya maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa China na Russia, kudumisha urafiki kizazi hadi kizazi ni nia ya pamoja na chaguo pekee la nchi na watu wa nchi hizo mbili. Rais Hu Jintao amesema katika mwaka mpya, China inapenda kushirikiana na Russia kuimarisha uhusiano wa nchi mbili kutoka pande nne:

"Kwanza ni kuimarisha kuaminiana katika mambo ya kisiasa zinatakiwa kuendelea kuelewana na kuungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi muhimu ya taifa. Pili, kuhimiza ushirikiano halisi wa kunufaishana katika maeneo ya uchumi, biashara, nishati, sayansi na teknolojia. Tatu, kupanua ushirikiano na maingiliano ya utamaduni wa nchi mbili, na kuimarisha maelewano na urafiki wa nchi na watu wa nchi hizo mbili. Nne, kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili katika mambo ya kimataifa na kikanda, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya nchi mbili."

Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ni sehemu muhimu ya uhusiano wa nchi mbili. Katika miaka ya karibuni, uchumi wa China na Russia umeongezeka kwa kasi, hali ambayo imeleta nafasi nzuri kwa ushirikiano wa uchumi na biashara wa nchi mbili. Kwa mujibu wa takwimu za China, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2006, uwekezaji wa kampuni za Russia nchini China ulikuwa umezidi dola za kimarekani milioni 600, pande mbili zimekuwa na ushirikiano mzuri katika sekta za uzalishaji bidhaa, ujenzi wa majengo, mawasiliano na usafirishaji, kazi za kemikali na uunganishaji wa magari.

Moja ya shughuli muhimu wakati wa ziara ya rais Hu Jintao ni kuzindua shughuli za "mwaka wa China" pamoja na rais Putin. Pande mbili zitafanya shughuli zaidi ya 300 za kuadhimisha mwaka huo. Rais Hu Jintao alionesha matarajio makubwa kwa vyombo vya habari vya China na Russia, amevitaka visaidie watu wa nchi hizo mbili kufahamu hali ya maendeleo ya wenzao na kukuza urafiki wa jadi kati yao.