Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-27 15:07:40    
China yafanya juhudi ili kukamilisha mfumo wa mambo ya fedha vijijini

cri

Kikilinganishwa na miji na sehemu zinazoendelea kwa kasi kiuchumi, kiwango cha utoaji huduma za fedha katika vijiji vya China ni cha chini, hali ambayo inasababisha ukosefu wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya sehemu za vijiji. Hivyo kuharakisha mageuzi na maendeleo ya mambo ya fedha vijijini na kukamilisha mfumo wa fedha vijijini ni moja ya kazi muhimu za uchumi za China katika mwaka huu.

Mfumo wa fedha vijijini nchini China bado uko nyuma, kwa mfano: matawi ya benki kubwa za biashara katika sehemu za vijiji ni machache, hivi sasa, licha ya Benki ya kilimo ya China, benki nyingine 3 kubwa za biashara za kiserikali hazitoi huduma katika sehemu za vijijini, hivyo kuna upungufu wa fedha kwa ajili ya maendeleo vijijini. Aidha aina na maeneo ya bima za kilimo nchini China bado yanahitaji kupanuliwa.

Lakini jambo linalofurahisha ni kwamba, mikutano mingi ya mambo ya fedha ya China iliyofanyika hivi karibuni ilitoa habari nyingi nzuri za kuunga mkono maendeleo ya fedha vijijini. Kwanza hali ya ukosefu wa fedha vijijini inatazamiwa kubadilika. Serikali ya China imesema, itaifanyia mageuzi ya pande zote Benki ya kilimo ya China, ambayo thamani ya mali zake imezidi Yuan za RMB trilioni 4. Baada ya kufanyiwa mageuzi, Benki ya kilimo itaunga mkono maendeleo ya vijiji na kilimo, na kuinua kiwango cha utoaji huduma za fedha.

Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa uchumi wa China ya Chuo Kikuu cha Beijing Profesa Lin Yifu alisema, mageuzi ya Benki ya kilimo yatavifanya vijiji vya China vipate uungaji mkono zaidi. ?

"Benki ya China, Benki ya viwanda na biashara na Benki ya ujenzi ya China ni benki zinazounga mkono maendeleo ya miji na viwanda, na sehemu za vijijini kweli zinahitaji benki kubwa inayotoa huduma kwa kilimo, vijiji na wakulima."

Benki ya posta yenye akiba za Yuan za RMB trilioni 1.6 pia itafanyiwa mageuzi pamoja na Benki ya kilimo. Kutokana na mpango wa serikali ya China, Benki ya posta itajiendeleza vizuri kwa kutegemea nguvu yake, ambayo matawi yake yanatapaka mijini na vijijini kote nchini China, ili kushirikiana na Benki ya kilimo na kutoa uungaji mkono wa fedha kwa ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ya vijijini, na kutoa huduma bora za fedha kwa wakulima.

Licha ya kuzifanyia mageuzi benki kubwa za biashara zinazotoa huduma mahsusi kwa ajili ya maendeleo ya vijiji, China pia inalegeza masharti ya kuingia sokoni ili kuhimiza mitaji ya kigeni na mitaji binafsi kuanzisha benki katika sehemu za vijijini. Kutokana na sheria mpya za kamati ya usimamizi wa sekta ya benki ya China, kuanzisha benki za vijiji katika sehemu za ngazi za wilaya zinazotoa huduma za fedha kwa wakulima na uzalishaji wa kilimo, mtaji unaohitajika kusajiliwa hakutakuwa chini ya Yuan za RMB milioni 3, na mtaji utakaoruhusiwa kusajiliwa katika kuanzisha benki za biashara za miji zinazotoa huduma mbalimbali hautakuwa chini ya Yuan za RMB milioni 100. Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa sekta ya benki ya China Bw. Liu Mingkang anaona kuwa, lengo la hatua hiyo ni kuongeza uwekezaji zaidi katika sekta ya utoaji huduma za fedha vijijini. ?

"China itafanya juhudi kuunga mkono na kuongeza mitaji ya benki, mitaji ya sekta za uzalishaji na mitaji binafsi kuwekeza, kununua na kuanzisha benki za vijiji katika sehemu za vijijini, na tutapunguza kiasi cha mtaji unaotakiwa kusajiliwa ili kuanzisha benki na vitengo vya benki vijijini, na kulegeza masharti ya kuanzisha idara za fedha vijijini, ili kuihimiza idara hizo zijitahidi kuanzisha shughuli mbalimbali za fedha, na kutoa huduma bora."

Wakati huohuo idara ya usimamizi wa sekta za benki ya China pia inaihimiza mitaji binafsi kuanzisha kampuni zinazotoa mikopo midogo katika sehemu za vijijini, ambazo zitatoa huduma mahsusi kwa viwanda vya wakulima na vijiji. Idara hiyo pia inapanga kutoa sera ya riba inayolenga mikopo binafsi, ili kutoa fedha nyingi zaidi kwa sehemu za vijijini.

Huduma nyingine ya fedha itakayokuwa karibu na vijiji nchini China ni sekta ya bima. Mwaka 2006 uhakikisho wa kukabiliana na maafa uliotolewa na bima ya China kwa kilimo, vijiji na wakulima ulifikia Yuan za RMB bilioni 73.3, ambao uliongezeka mara mbili kuliko ule wa mwaka uliopita wakati kama huu. Lakini kwa kuwa hatari ya bima za kilimo ni kubwa, na gharama zake ni nyingi, hivyo kuna tatizo la eneo la bima ya kilimo na aina chache za bima katika sehemu mbalimbali nchini China.

Mkutano wa kazi za fedha wa China uliomalizika hivi karibuni ulisema, inapaswa kukuza shughuli za bima ya kilimo, kuimarisha nguvu za utoaji msaada wa kisera kwa idara mbalimbali za bima vijijini na kutoa aina mpya za bima kutokana na uzalishaji wa kilimo na maisha ya wakulima. Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa sekta ya bima Bw. Wu Dingfu alisema, mwaka huu China itaweka mkazo katika kuunga mkono maendeleo ya vijiji na kilimo. ?

"Mwaka huu tutaweka mkazo katika kuendeleza bima za vijiji, kilimo na wakulima, tutahimiza utoaji wa sera na hatua husika, na kutunga sheria za bima ya kilimo ya kisera pamoja na idara husika. Aidha tutahimiza kuanzisha utaratibu wa fedha za bima zitakazotumika kwa ajili ya kukabiliana na maafa makubwa ya kilimo, ili kuondoa hatari za maafa makubwa yatakayoathiri kilimo. Vilevile tutahimiza kampuni za bima kulenga mahitaji ya wakulima, kuimarisha kazi za kuongeza aina mpya za bima na uvumbuzi wa huduma, ili kukidhi mahitaji ya bima ya wakulima katika matunzo ya uzeeni, afya, kuumia ghafla na kadhalika.

Mambo ya fedha vijijini zinachukua hadhi maalum na kutoa mchango muhimu katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa kilimo na vijiji na kuongeza mapato ya wakulima. Hivyo wataalam wengi wa fedha wa China wanakubali sera za kuunga mkono mambo ya fedha vijijini zilizotolewa hivi karibuni na serikali ya China. Mtaalamu wa mambo ya fedha wa kituo cha utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali Bw. Xia Bin alisema, uungaji mkono wa serikali utavipatia vijiji vya China uungaji mkono mwingi zaidi wa kifedha, ambao utasaidia kuboresha mazingira ya kisera ya mambo ya fedha vijijini, na kujenga mfumo wa mambo ya fedha vijijini ulio kamili zaidi. ?

"Sera hizo zitazidi kukamilisha mfumo wa mambo ya fedha vijijini nchini China, kuunga mkono maendeleo ya kilimo katika vipindi vya kabla, baada na katikati ya uzalishaji, na kuongeza mapato ya wakulima mapema."

Wakati huohuo wataalam wa fedha pia walisema, suala la kiwango chini cha utoaji huduma za fedha za vijiji nchini China haliwezi kutatuliwa mara moja. Hivi sasa maendeleo ya sekta ya fedha vijijini nchini China bado yanakabiliwa na changamoto kubwa. Kwa mfano, kiwango cha mikopo mibaya cha benki ya kilimo ya China ni cha juu, hivyo ili kutimiza mageuzi kikamilifu, ni lazima kutoa mitaji mingi; hivi sasa China bado haina sheria kamili za bima ya kilimo kwa ajili ya kurekebisha uhusiano wa watu katika shughuli za bima. Hali hii ni tatizo katika kueneza bima ya kilimo nchini China. Wataalam wanapendekeza kuwa, China inatakiwa kutoa hatua kamili husika zinazoambatana na mazingira yake, ili kuhakikisha sera zinazounga mkono mambo ya fedha kwa ajili ya vijiji zitumike kwa ufanisi.

Idhaa ya kiswahili 2007-03-27