Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-27 15:49:54    
Waziri mkuu wa Japan aomba msamaha kuhusu suala la "wanawake wa kustarehesha"

cri

Tarehe 26 Machi kutokana na shinikizo la ndani na nchi za nje waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe aliomba rasmi msamaha kuhusu suala la wanawake waliolazimishwa kuwastarehesha askari wa Japan katika vita vya pili vya dunia.

Habari kutoka vyombo vya habari vya Japan zinasema, katika siku hiyo kwenye mkutano wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Juu la bunge la Japan, mbunge kutoka Chama cha Kikomunisti Bi. Haruko Yoshikawa alipouliza kama serikali itaomba rasmi msamaha kuhusu suala la wanawake waliolazimishwa kuwastarehesha askari wa Japan kwenye vita vya pili vya dunia, waziri mkuu Bw. Shinzo Abe alijibu, akiwa waziri mkuu anaomba msamaha kutokana suala hilo, na serikali inakubali msimamo wa waziri mkuu wa zamani Bw. Yohei Kono katika mazungumzo yake. Alisema, anawahurumia na kuwaomba msamaha wanawake hao waliodhalilishwa.

Mwaka 1993 baada ya uchunguzi kufanyika, waziri mkuu aliyekuwa madarakani wakati huo Bw. Yohei Kono katika mazungumzo yake alikiri kwamba jeshi la Japan liliwahi kujihusisha na vituo vya wanawake wa kuwastarehesha askari wa Japan vilivyokuweko katika peninsula ya Korea na China na kuwalazimisha wanawake wa Asia kuwa wanawake wa kuwastarehesha askari wa Japan wakifuatana na jeshi, kuhusu jambo hilo waziri mkuu huyo aliomba msamaha. Baadaye mazungumzo yake hayo yanaitwa "mazungumzo ya Kono Yohei". Hivi karibuni, baadhi ya wabunge walijaribu kukana ukweli wa historia hiyo na kutaka uchunguzi ufanyike upya. Bw. Shinzo Abe ambaye hapo awali alikubali "mazungumzo ya Yohei Kono", baadaye aliunga mkono kauli hiyo ya wabunge, na kusema hakuna ushahidi unaoonesha kuwa serikali na jeshi la Japan iliwalazimisha wanawake kufanya kazi ya kuwastarehesha askari wa Japan. Msimamo huo wa Yohei Kono ulisababisha malalamiko mengi ya kimataifa. Baraza la juu la bunge la Marekani limekuwa likichunguza azimio ambalo linataka Japan iombe msamaha kuhusu suala hilo lililotokea katika vita vya pili vya dunia, na mbunge mmoja wa Kamati ya Mambo ya Nje ya bunge la Marekani anaona kuwa msimamo wa Japan kuhusu suala hilo ni kichekesho.

Kabla ya hapo, kikundi cha mazingira cha Asia na Pasifiki katika Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Marekani mwezi Februari kwa mara ya kwanza kiliwaalika wanawake watatu waliolazimishwa kutoa huduma ya kuwastarehesha askari wa Japan washiriki kwenye mkutano wa wazi. Kwenye mkutano huo wanawake hao walieleza kwa kirefu jinsi walivyodhalilishwa na kubakwa, na waliomba serikali ya Marekani iihimize serikali ya Japan iombe radhi rasmi. Bunge la Marekani liliwahi kutoa miswada mingi ya maazimio kuhusu suala hilo, lakini serikali ya Japan ilituma watu wengi kwenda kuwashawishi wabunge nje ya bunge, miswada hiyo haikupitishwa. Lakini baada ya Chama cha Democrat kudhibiti bunge, hali imebadilika, na vyombo vya habari pia vimekuwa na msimamo mkali. Gazeti la Marekani la Washington Post tarehe 24 lilichapisha makala ya mhariri ikimkosoa Bw. Shinzo Abe kuwa na "msimamo wa ajabu" na wa "kuchukiza".

Licha ya vyombo vya habari vya nchi za nje, pia kuna vyombo vya habari vya nchini Japan ambavyo vilichapisha makala nyingi kumkosoa Bw. Shinzo Abe kuhusu kukataa ukweli wa historia. Gazeti la Japan Yomiuri tarehe 4 lilisema, kupingana na msimamo wa Marekani "kutaleta hasara tu kwa taifa la Japan".

Katika mazingira kama hayo ya shinikizo kubwa, mnamo tarehe 11 Machi kwenye Redio ya NHK ya Japan Bw. Shinzo Abe alisema, kwa dhati ya moyo anaomba msamaha kwa wanawake waliolazimishwa kuwastarehesha askari wa Japan, wanawake ambao waliumizwa rohoni na kudhalilishwa. Tarehe 26 kwenye mkutano wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Juu la Bunge la Japan kwa heshima ya waziri mkuu Bw. Shinzo Abe aliomba radhi tena. Kuhusu suala hilo, naibu waziri mkuu wa zamani wa Japan alisema kutuliza suala hili ni muhimu, lakini cha muhimu zaidi ni kuomba msamaha wa kweli na kuonesha kwa vitendo.

Idhaa ya kiswahili 2007-03-27