Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-27 19:16:11    
Marais wa China na Russia wazindua "Mwaka wa China"

cri

Sherehe ya kuzindua "Mwaka wa China" wa Russia ilifanyika usiku wa tarehe 26 mwezi Machi kwenye ukumbi wa ikulu ya Russia mjini Moscow. Rais wa China Hu Jintao anayefanya ziara nchini Russia na rais Putin wa Russia walishiriki sherehe ya uzinduzi. Uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa China na Russia umeingia kipindi cha pili cha miaka kumi na kufungua kwenye ukurasa mpya kwenye historia ya uhusiano wa nchi mbili.

kutokana na makubaliano waliyofikia wakuu wa nchi hizo mbili, pande mbili zilifanya shughuli za "Mwaka wa Russia" mwaka 2006 nchini China, ambapo shughuli zaidi ya 300 za mwaka huo zilishirikiwa na watu wengi wa nchi hizo mbili, na uhusiano wa nchi mbili uliimarishwa kwa kiwango kisichowahi kutokea katika historia. Mwaka huu pande mbili zinafanya shughuli za "Mwaka wa China" nchini Russia. Tarehe 26 usiku, wakuu wa nchi hizo mbili walizindua sherehe za kuadhimisha "Mwaka wa China" kwenye ukumbi wa ikulu ya Russia mjini Moscow.

Ikulu ya Kremlin ni jengo la kisasa lililojengwa kwa mawe ya marumaru na vioo, ukumbi wake una viti 600. Tarehe 26 usiku, viti vyote ukumbini vilijaa watu, nyuma ya jukwaa iliwekwa alama kubwa ya "Mwaka wa China", ambayo ni panda mdogo aliyevaa koti jekundu la jadi ya kichina pamoja na dubu wa rangi ya kahawia aliyevaa nguo nyeupe za jadi ya kirussia wakishikana mkono, kunyanyua bendera za mataifa yao na kurukaruka kwa furaha. Rais Hu Jintao akitoa hotuba kwenye sherehe ya uzinduzi alieleza maana muhimu ya kufanya shughuli za "Mwaka wa

China".

"Mwaka huu tunafanya shughuli zaidi ya 200 za 'Mwaka wa China' nchini Russia zikiwa ni pamoja na za kisiasa, kiuchumi, sayansi, teknolojia na utamaduni. Tunatarajia kuwaonesha warussia historia, utamaduni, mageuzi na ufunguaji mlango wa China kwa shughuli hizo ili kuimarisha maelewano na urafiki wa watu wa nchi hizo mbili, kukuza ushirikiano na maingiliano wa nchi hizo mbili kwenye maeneo mbalimbali na kuongeza nguvu mpya kwa ajili ya kudumisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia."

Rais Putin alipotoa hotuba akisema,

"Uamuzi niliofanya pamoja na Rais wa Hu Jintao wa kuanzisha shughuli za kuadhimisha mwaka wa China na Russia ni jambo lenye umuhimu wa kimkakati. Uzoefu umedhihirisha kuwa uamuzi huo ni sahihi na umeleta mafanikio mengi. Lengo la shughuli hizo ni kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya nchi zetu mbili na kusaidia watu wetu kufahamu vizuri zaidi hali ya wenzao na kudumisha uhusiano mzuri wa nchi zetu mbili."

Baada ya sherehe ya uzinduzi, wasanii wa China walifanya maonesho ya nyimbo na ngoma zenye umaalumu wa kimashariki. Baada ya maonesho kumalizika, watazamaji wa Russia walipongeza maonesho murua wa wasanii wa China kwa makofi ya muda mrefu.