Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-28 18:55:10    
Mapishi ya supu ya muhindi na vipande vya mbavu za nguruwe

cri

Mahitaji

Muhindi mmoja, mbavu za nguruwe gramu 200, tangawizi gramu 5, vitunguu maji gramu 5, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, na chumvi vijiko vitatu.

Njia

1. kata kata mbavu za nguruwe ziwe vipande, kata muhindi uwe vipande vipande, kata kata vitunguu maji na tangawizi.

2. chemsha maji kwenye sufuria halafu tia vipande vya mbavu za nguruwe kwenye sufuria ili kuondoa damu, na kasha vipakue.

3. washa moto, mimina maji kwenye sufuria, tia vipande vya mbavu za nguruwe, vipande vya muhindi, vitunguu maji na tangawizi, halafu mimina mvinyo wa kupikia, baada ya kuchemka, punguza moto, endelea kuchemsha kwa dakika 40, baada ya hapo tia chumvi halafu ipakue. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kunywawa.