Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-28 19:11:11    
Marais wa China na Russia wazindua "Maonesho ya mwaka wa China"

cri

"Maonesho ya mwaka wa China", ambayo ni maonesho ya kitaifa yanayochukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa ya China yanayooneshwa katika nchi za nje kuhusu mambo ya maeneo mengi ya China. Maonesho hayo yalizinduliwa tarehe 27 mwezi Machi nchini Russia na rais Hu Jintao, ambaye hivi sasa anafanya ziara nchini Russia pamoja na rais Putin wa Russia.

"Maonesho ya kitaifa ya China" ni moja ya shughuli muhimu za kitaifa katika shughuli za maadhimisho za "Mwaka wa China", kauli-mbiu ya maonesho hayo ni 'ushirikiano wa kunufaishana na maendeleo yenye mapatano'. Idara na kampuni zaidi ya 200 kutoka mikoa 31 ikiwemo mikoa ya utawala maalumu ya Macau na Hong Kong inashiriki kwenye maonesho hayo yenye vitu na bidhaa zaidi ya elfu 15 na picha zaidi ya elfu moja, yanayofanyika kwenye eneo lenye mita za mraba kiasi cha elfu 20, maonesho hayo yanahusu maeneo zaidi ya 30 yakiwemo ya siasa, uchumi, utamaduni, sayansi na teknolojia, maisha ya watu na mandhari ya kimaumbile. Maonesho hayo yanawakilisha kiwango cha kisasa cha maendeleo ya sekta mbalimbali za China. Rais Hu Jintao alipotoa hotuba kwenye sherehe ya uzinduzi wa maonesho hayo, alisema,

"Maonesho hayo yatawaonesha watu wa Russia historia ndefu na ustaarabu wa murua wa China, kuonesha mwendo wa mageuzi na ufunguaji mlango pamoja na ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, na yanaonesha mafanikio yaliyopatikana katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa China na Russia. 'Maonesho ya mwaka wa Russia' yaliyofanyika mwezi Novemba mwaka jana nchini China yaliwapa watu wa China kumbukumbu nzuri sana. Ninaamini kuwa, 'Maonesho ya mwaka wa China' pia yatakuwa tamasha linalokuza urafiki wa jadi wa watu wa nchi hizo mbili na chombo cha kuhimiza ushirikiano wa pande mbili."

"Maonesho ya mwaka wa China" yanajitahidi kuonesha sura ya mageuzi, ufunguaji mlango, utulivu na ustawi ya China; Kuimarisha ushirikiano kati ya China na Russia katika maeneo ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, mawasiliano ya habari pamoja na ndege na mambo ya anga ya juu; kuhimiza maelewano na ushirikiano wa mikoa ya nchi hizo mbili; na kuonesha kiwango cha kisasa cha sekta ya uzalishaji wa bidhaa ya China. Katika miaka ya karibuni uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Russia uliendelezwa vizuri, uwekezaji wa kila upande umekuwa mkubwa na kuongezeka kwa haraka. Katika hotuba yake rais Hu Jintao alieleza matarajio yake:

"China na Russia zinajitahidi kuhimiza maendeleo ya uchumi wake. Ushirikiano halisi wa pande mbili katika maeneo mbalimbali umeimarisha kwa kiwango kikubwa na kuwa na mustakabali mzuri. Natarajia kuwa pande hizi mbili zitatumia nafasi muhimu ya "Mwaka wa Taifa" kutafuta na kuimarisha sehemu mpya za ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, mbali na kupanua maeneo yake, pia zinatakiwa kuongeza ushirikiano, kuinua kiwango cha ushirikiano, kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati, na kunufaisha watu wa nchi hizo mbili!"

Habari zinasema madhumuni ya "Maonesho ya mwaka wa China" yana lengo la kuhimiza kampuni, viwanda na bidhaa bora za China kuingia kwenye soko la Russia na kuwa chombo muhimu cha kuimarisha uhusiano wa kampuni na viwanda vya nchi hizo mbili na kupanua ushirikiano kwa pande zote. Inatarajiwa kuwa thamani ya makubaliano yatakayosainiwa na kampuni na viwanda vya pande hizo mbili inatazamiwa kufikia dola za kimarekani bilioni 4.3. Hali kadhalika rais Putin pia ana matumaini makubwa na maendeleo ya China, alisema anaamini kuwa, kutokana na maonesho hayo, pande mbili zitaanzisha miradi mingi ya ushirikiano, na aliyatakia mafanikio "Maonesho ya mwaka China" nchini Russia.