Kituo cha kimataifa cha kupunguza athari ya maafa ya ukame kilianzishwa tarehe 2 Aprili mjini Beijing, kituo hicho kilianzishwa chini ya ushirikiano kati ya Kamati ya upunguzaji wa atahari ya maafa ya China na Shirika la mikakati ya upunguzaji wa athari ya maafa duniani la Umoja wa Mataifa.
Maafa ya ukame ni moja kati ya maafa zinazotokea mara kwa mara na kwa muda mrefu kabisa ambazo huleta hasara kubwa kabisa za kiuchumi. Takwimu zilizofanywa zimeonesha kuwa, katika eneo la dunia nzima, karibu nusu ya nchi zote duniani zilikubwa na athari mbaya ya maafa ya ukame, mwanzoni mwa majira ya siku za joto ya mwaka jana Mkoa wa Sichua na Mji wa Chongqing nchini China ilikumbwa na maafa makubwa ya kame ambayo hayakutokea katika miaka mingi iliyopita, ambayo yalileta athari mbaya kwa maisha ya wakazi wa sehemu hizo. Katika hali ya kuongezeka kwa joto kote duniani, matatizo mbalimbali yaliyosababishwa na maafa ya ukame kama vile upungufu wa maji, hali ya kuvia kwa mazingira ya viumbe, upunguzaji wa nafaka, na kuongezeka kwa idadi ya watu wenye matatizo ya kiuchumi, yote hayo yamekuwa sababu kubwa za kuathiri vibaya maendeleo endelevu ya uchumi na jamii ya kanda mbalimbali hata dunia nzima.
Serikali ya China siku zote inatilia maanani kufanya utafiti na usimamizi wa athari ya maafa ya ukame, na imepata uzoefu mwingi katika kupunguza athari ya maafa ya ukame. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya upunguzaji wa athari ya maafa ya China ambaye pia ni naibu waziri wa mambo ya raia Bwana Li Liguo alisema: (??)
China imeanzisha mfumo wa kusimamia athari ya maafa ya ukame, mfumo wa kufuatilia, kuchunguza, kutoa tahadhari na tathimini juu ya athari ya maafa ya ukame, imeanzisha mfumo wa kueneza teknolojia husika, na idara za kufanya utafiti, hivyo China imekuwa na seti moja ya sera, hatua na mbinu za kupunguza athari ya maafa ya ukame. Ili kupunguza hasara zinazosababishwa na maafa ya ukame, na kupunguza athari yake, China inaimarisha bila kusita ujenzi wa miundo mbinu, na kuongeza uwezo wa idara na watu husika wa kukabiliana na maafa, ambapo imetekeleza miradi mbalimbali ya kisayansi na kiteknoloji kwa ajili ya kupunguza athari ya maafa.
Katika miaka ya karibuni, Kamati ya upunguzaji wa maafa ya China na jumuia nyingi za kimataifa pamoja nchi mbalimbali duniani zimefanya shughuli nyingi za kupunguza athari ya maafa na kuanzisha utaratibu wa ushirikiano wenye ufanisi. Kuanzishwa kwa Kituo cha kimataifa cha kupunguzaji athari ya maafa ya ukame mjini Beijing chini ya ushirikiano wa China na shirika la Umoja wa Mataifa kunaonesha kuwa, ushirikiano wa kimataifa na kikanda katika kazi za kupunguza athari ya maafa ya ukame umepiga hatua kubwa kwa kuelekea utekelezaji halisi wa mipango.
Naibu mkurugenzi wa kituo cha upunguzaji wa athari ya maafa katika wizara ya mambo ya raia ya China Bwana Fang Zhiyong alisema:
Kituo cha kimataifa cha kupunguzaji athari ya maafa ya ukame kitategemea mbinu za teknolojia zinazohusika na anga ya juu kwa kufanya uchunguzi na usimamizi wa athari ya maafa ya ukame kote duniani, ili kuanzisha hatua kwa hatua mfumo wa upashanaji wa habari na utoaji wa huduma; kuimarisha ujenzi wa maktaba ya data za tarakimu na ujuzi unaohusika, kuanzisha tovuti kwenye mtandao wa internet na vituo vya upashanaji wa habari, na hatua kwa hatua kuunganisha tovuti na vituo hivyo na vile vya nchi mbalimbali na jumuia za kimataifa duniani, ili kuwa na mfumo wa kuhimiza kazi ya kupunguza athari ya maafa ya ukame.
Habari zinasema kuwa, kituo hicho cha kimataifa cha kupunguza athari ya maafa ya ukame kitasaidiwa na serikali ya China na idara mbalimbali za China hivyo maendeleo ya siku za mbele ya kituo hiki hakika yatafurahisha.
Idhaa ya kiswahili 2007-04-03
|