Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-04 16:17:44    
Maisha ya wafugaji wa kabila la Wamongolia yaboreshwa

cri

Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ulioko kaskazini mwa China unajulikana kwa kuwa na mbuga pana za kimaumbile, wafugaji wa kabila la Wamongolia waliwahi kuishi maisha ya kuhamahama, walitafuta maji na malisho huku wakiweka makambi kila mahali walikoenda. Hivi sasa maisha ya wafugaji kwenye mbuga za Mongolia ya ndani yamepata mabadiliko makubwa.

Mbuga ya Uzumqing ni sehemu moja ya mkoa wa Mongolia ya ndani ambayo utamaduni na mila za kabila la Wamongolia zinahifadhiwa vizuri. Mbuga hiyo ina mandhari nzuri na uwanda mpana wa majani, ni moja ya vituo vikubwa ambako mifugo inazalishwa kwa wingi nchini China. Kondoo wa huko wanaotoka katika bustani ya wanyama ya Uzumqing wana umbo kubwa, nyama laini, na ladha nzuri, wanapendwa sana na waislamu wa nchi za mashariki ya kati. Kila mwaka kondoo na ng'ombe hai na bidhaa za mifugo hao zinasafirishwa nje kwa wingi.

Zamani wafugaji wa huko walikuwa wakichunga mifugo yao kwa kuiachia huru malishoni, hivi sasa wamebadilisha njia ya ufugaji ya kutegemea hali ya hewa na kufuatana na maji na malisho, wanatumia njia ya kisayansi. Mfugaji hodari wa kijiji cha Baiyimhuobur Bwana Buhebayar alisema ufugaji wa kisayansi si kama tu umeinua kiwango cha maisha ya familia yake, bali pia umewawezesha kuwa na muda mwingi zaidi wa kujiburudisha. Licha ya kuweza kucheza mieleka ya kimongolia mara kwa mara, mwaka jana yeye pia alijiunga na ujumbe wa ukaguzi wa wafugaji kutembelea sehemu yenye ufugaji wa kisasa nchini Canada. Alisema:

"Tulitembelea mashamba 10 ya ufugaji nchini Canada, ambayo ni ya kiwango kikubwa na kisasa, mazingira ya kimaumbile yanayohifadhiwa vizuri, na mfumo kamili wa ufugaji kutoka kuzaliana, kufuga, na kutengeneza bidhaa zinazotokana na nyama za mifugo. Sisi tunapaswa kubadilisha njia ya jadi ya ufugaji, kuingiza usimamizi wa kisasa wa ufugaji kutoka nje ili kuendeleza uzalishaji wa mifugo."

Katika uwanda wa majani wa Uzumqing, ni jambo la kawaida kwa wafugaji kufanya utalii katika nchi za nje. Miaka 9 iliyopita, Bwana Buhebayar aliitembelea Australia akifuatana na ujumbe wa ukaguzi wa wafugaji ulioandaliwa na wilaya ya huko, jambo lililompa picha nzuri ni ufugaji wa zamu. Yaani kuligawanya shamba la malisho katika sehemu mbalimbali, kila baada ya muda fulani sehemu moja inapumzishwa na sehemu nyingine zinaendelea kutumika kwa malisho. Baada ya kurudi nyumbani, Bw. Buhebayar aligawanya shamba lake la malisho lenye hekta zaidi ya 600 katika sehemu 8, na kufuga mifugo katika sehemu mbalimbali kwa zamu. Wakati huo huo yeye alipunguza idadi ya kondoo, na kuagiza ng'ombe wenye sifa bora. Kufanya hivyo shamba la malisho limefufuka vizuri, na viumbe wa kimaumbile wamekuwa na uwiano, na mapato yake pia yameongezeka. Mwaka jana baada ya kurudi kutoka Canada, Bw. Buhebayar alipanga kuingiza teknolojia na njia ya usimamizi kwa kuendeleza ufugaji wa mifugo kwenye mazingira mazuri ya viumbe kutoka Canada. Mbali na Bw. Buhebayar, wafugaji wengine wengi katika uwanda wa majani wa Uzumqing pia wanajifunza kutumia mbinu mpya za ufugaji. Mkuu wa kijiji kingine cha wilaya hiyo Bwana Tao Getao alisema:

"Kijiji chetu kinazalisha mifugo zaidi ya 40,000 kwa mwaka. Zamani wafugaji walikuwa wanasubiri mifugo yao kununuliwa nyumbani, lakini mwaka huu wameenda mijini kuuza wanyama wao kwa kampuni zenye sifa nzuri ya kusindika na kutengeneza bidhaa za nyama, au kufanya utengenezaji wa hatua ya mwanzo ili kuongeza thamani ya mifugo yao."

Katika uwanda wa majani wa Uzumqing, wafugaji wengi wameanza kutumia usimamizi wa kisayansi, kupanua maeneo ya malisho na kutumia mitambo husika. Zamani ikitokea dhoruba ya theluji ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa wafugaji, walipaswa kupambana na maafa. Lakini hivi sasa hata katika majira ya baridi, familia za wafugaji wa huko zinaishi katika hali yenye masikilizano. Katika kijiji cha Manduhubaolige, wanaishi wafugaji zaidi ya familia 100 wa kabila la Wamongolia, mkuu wa kijiji hicho Bwana Suyila Bater alifahamisha:

"Kwa sababu wafugaji wameanza kufanya ufugaji wa kutumia malisho kwa zamu, na zaidi ya asilimia 80 ya wafugaji wa kijiji chetu wamejenga vibanda vya kudumu vya mifugo, hivyo kondoo na ng'ombe hawaogopi tena dhoruba ya theluji. Wafugaji wa kijiji hicho pia wanatumia mitambo ya kuzalisha umeme kwa nguvu ya upepo, na kuwa na simu nyumbani. Hivi sasa wafugaji wanajitahidi kujipatia mapato makubwa na kuishi maisha mazuri."

Idhaa ya kiswahili 2007-04-04