Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-04 18:48:47    
Mkutano wa wakuu wa Umoja wa ushirikiano wa kanda ya Asia Kusini wafunguliwa

cri

Mkutano wa 14 wa wakuu wa Umoja wa ushirikiano wa kanda ya Asia Kusini ulifunguliwa tarehe 3 huko New Delhi, mji mkuu wa India. Pamoja na viongozi wa nchi wanachama wa umoja huo, wajumbe wa nchi tano wachunguzi za China, Korea ya Kusini, Japan, Marekani na Umoja wa Ulaya, pia walihudhuria ufunguzi wa mkutano huo. Huu ni mkutano wa kwanza wa wakuu kufanyika baada ya umoja huo kupokea nchi mpya mwanachama na wachunguzi.

Mada muhimu za mkutano huo ni ushirikiano wa nchi wanachama katika kuwasaidia nchi maskini kujiendeleza, katika sekta za biashara, elimu na mapambano dhidi ya ugaidi, na taarifa au tangazo la pamoja linatarajiwa kutolewa kwenye mkutano huo. Katika ufunguzi wa mkutano huo, waziri mkuu wa India ambayo ni nchi mwenyeji Bw. Manmohan Singh aliipongeza Afghanistan kuwa nchi mwanachama wa nane wa umoja huo, pia alizikaribisha China, Korea ya Kusini, Japan, Marekani na Umoja wa Mataifa, zikiwa ni wachunguzi wa umoja huo, kutuma kwa mara ya kwanza wajumbe wao kuhudhuria kwenye mkutano huo.

Bw. Singh alisema kanda ya Asia Kusini inafanya mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi ambayo hayajawahi kutokea hapo awali, na mchakato wa mageuzi hayo huenda unaleta maumivu. Ndiyo maana inabidi kila nchi mwanachama wa Umoja wa ushirikiano wa kanda ya Asia Kusini ifanye jitihada kubwa zaidi, na serikali za nchi hizo pia zinapaswa kuondoa migongano zilizoko na kushikamana katika kutimiza lengo la pamoja. Alisisitiza kuwa hivi sasa umaskini na maradhi ni matatizo mawili makubwa yanayozikabili nchi za Asia Kusini, hata hivyo kuna fursa nzuri za kuinua maisha ya wananchi na kuharakisha maendeleo ya kanda hiyo.

Waziri mkuu wa Pakistan akihutubia kwenye ufunguzi huo alisema, Asia ya Kusini iko katika makutano ya njia. Alifafanua kuwa nchi za kanda hiyo zimepata mafanikio kadhaa, lakini zina nguvu kubwa ambazo bado hazijatumika. Kukabiliana na dunia inayobadilika kwa haraka, ni lazima nchi za kanda hiyo zikabiliane na changamoto, kuchambua nguvu na kasoro zao ili kuchukua hatua halisi badala ya kuwa mjadala usio na kikomo. Alisema "Tunajitahidi kuleta maendeleo ya Umoja wa ushirikiano wa kanda ya Asia Kusini. Inatubidi tutumie ushujaa, nia imara, busara na upeo wa mbali, kuibadilisha Asia ya Kusini iwe kanda yenye uhai, maendeleo na ustawi zaidi, hili ni jukumu letu la pamoja. Tunapaswa kubadilisha mtindo wa kufikiria na msimamo wetu ili kutimiza lengo hilo."

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan anayehudhuria mkutano huo kwa mara ya kwanza, alisema kuwa nchi mwanachama wa umoja huo kunanufaisha Afghanistan na nchi wanachama wengine. Alisema "Afghanistan kuwa nchi mwanachama rasmi wa umoja huo kunatoa nafasi kwa kuongeza maingiliano kati ya watu wa kanda hiyo na kuleta faida kubwa zaidi kiuchumi. Kwa hiyo tunatoa kipaumbele sera ya kufanya ushirikiano wa kikanda, sera ambayo pia ni kiini cha mkakati wa maendeleo ya taifa ya Afghanistan."

Kwa niaba ya serikali ya China, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Zhaoxing alitoa hotuba kwenye mkutano, alisema "Serikali ya China inaunga mkono lengo la Umoja wa ushirikiano wa kanda ya Asia Kusini na maeneo yanayopewa kipaumbele na umoja huo kuyaendeleza. China inapenda kufanya maingiliano na umoja huo kwa msingi wa kuheshimu nchi wanachama wa umoja huo, na kufuata moyo wa usawa, kuaminiana, kushirikiana na kupata ushindi kwa pamoja. China ina nia ya kupanua wigo wa ushirikiano halisi na umoja huo na kuhimiza amani na maendeleo katika kanda ya Asia Kusini na dunia."