Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-11 15:00:36    
Watu wa kabila la Wa-elunchun waishio milimani

cri

Mliyosikia ni sauti iliyoko kwenye filamu iliyopigwa katika miaka ya 60 ya karne iliyopita iitwayo "Watu wa kabila la Wa-elunchun". Filamu hiyo ilionesha watu wa kabila la Wa-elunchun wenye idadi ya watu wasiozidi elfu 10 walivyoishi sehemu ya milimani kwa kuwinda wanyama pori. Sasa ni miaka zaidi ya 40 imepita, watu wa kabila la Wa-elunchun wameondoka kutoka sehemu ya milimani na kuacha maisha ya uwindaji. Waandishi wetu wa habari hivi karibuni walitembelea familia ya Bw. He Shenglu katika kijiji wanakoishi watu wengi wa kabila la Wa-elunchun katika mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, kaskazini mashariki mwa China.

Bwana He Shenglu mwenye umri wa miaka 50 alikuwa mwindaji hodari kabisa katika kijiji chake, lakini tangu serikali ya huko ianze kutekeleza sera ya kupiga marufuku uwindaji mwaka 1996, Bw. He Shenlu ameacha kushika bunduki kwa miaka zaidi ya 10, lakini akizungumzia shughuli za uwindaji mara moja alionesha furahi zake. Akisema:

"zamani tulipoishi sehemu ya milimani, tulikuwa tunaishi maisha ya kuhamahama kwa ajili ya kufuata mawindo. Makazi yetu yalikuwa karibu na wanyama pori, na kwenye sehemu ya mtelemko wa mlima na karibu na mito."

Miaka zaidi ya 50 iliyopita, watu wa kabila la Wa-elunchun walikuwa wako katika kipindi cha jamii ya asili, hawakuwa na mawasiliano na nje, na waliishi katika nyumba zilizofanana na mahema zilizofumwa kwa magamba ya miti inayopatikana kwa wingi milimani, na walikuwa wanahama mara kwa mara. Mawindo yao yalikuwa ni dubu weusi, nguruwe pori, sungura pori na wanyama wengine waishio katika sehemu zenye baridi. Bw. He Shenglu alipokuwa na umri wa miaka 16 alifaulu kumwinda dubu mweusi, dubu mwitu ni mnyama mkali sana, hivyo mtu yeyote akimwinda dubu mwitu yeye husifiwa sana kama Bw. He Shenglu, ambapo wanakijiji wote walikusanyika pamoja kusherehekea mafanikio yake.

Wakati huo watu wa kabila la Wa-elunchun walifuata kanuni ya kugawana mawindo kwa usawa, mtu mmoja akifanikiwa kupata mnyama, kila mkazi wa kijijini aliweza kupewa fungu lake, hasa wazee, wanawake na watoto ambao walichukuliwa kuwa ni watu wasio na uwezo wa kuwinda.

Baada ya kuzaliwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, watu wa kabila la Wa-elunchun waliacha maisha ya uwindaji na kubadilika hatua kwa hatua kuwa watu wa jamii ya zama za hivi sasa, wakapewa huduma za matibabu, elimu, nyumba na kujengewa barabara. Kutokana na msaada wa serikali, watu wengi wa kabila la Wa-elunchun wameondoka sehemu za milimani na kuacha kabisa maisha ya uwindaji. Bw. He Shenglu na familia yake wanakaa katika nyumba kubwa ya matofali chini ya mlima, nyumba hiyo ilijengwa na serikali, na tena wanaweza kupata ruzuku ya maisha kila mwezi kutoka kwa serikali.

Ingawa hivi sasa maisha yao bado si mazuri sana, lakini Bw. He Shenglu na mke wake Tu Yuqin wana matumaini mazuri kwa maisha ya siku zijazo. Binti yao wa kwanza tayari ameolewa, binti yao wa pili na mwanao wanasoma kwenye shule ya sekondari ya kabila la Wa-elunchun. Shule hiyo ilijengwa na serikali kwa ajili ya watu wa kabila la Wa-elunchun, wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo hawalipi chochote. Bi. Tu Yuqin alisema ana matumaini makubwa na binti yao wa pili He Xu. Alisema:

"Matokeo ya masomo ya binti yangu ni mazuri, baada ya kumaliza masomo yake ya kwenye shule ya sekondari ya chini, mwakani nataka kumpeleka Beijing kusoma kwenye shule ya sekondari ya juu."

Msichana He Xu ambaye yuko kidato cha tatu kwenye shule ya sekondari ya chini ni fahari ya wazazi wake. Ingawa yeye bado ni mdogo lakini ana mawazo yake binafsi kuhusu maisha yake ya baadaye. Alisema:

"Natarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Makabila Madogo Madogo cha Beijing kujifunza mambo kuhusu kabila la Wa-elunchun, baada ya kuhitimu masomo nitarudi nyumbani kujenga wilaya inayojiendesha ya kabila la Wa-elunchun."

Msichana He Xu anaongea vizuri lugha ya Kichina, yeye pia anapenda kusikiliza muziki wa aina mbalimbali. Ingawa alizaliwa nje ya mlimani, lakini bado anapenda kutembelea sehemu ya mlimani akiwa na nafasi, kama ilivyo kwa wazazi wake, yeye pia amepata picha nzuri na kumbukumbu nyingi kwa maisha ya sehemu ya mlimani. Alisema:

"Nikifika tu sehemu ya mlimani huwa najisikia vizuri, nataka kupiga makelele, hewa ya mlimani ni nzuri zaidi kuliko sehemu nyingine. Ninapenda milima ambao nilizaliwa kwenye sehemu ya mlimani."

Umbali wa kijiografia hauwezi kuwatenganisha watu wa kabila la Wa-elunchun na milima sehemu babu zao walikoishi kizazi hadi kizazi.

Idhaa ya kiswahili 2007-04-11