Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-10 15:10:10    
Mji wa Wuxi waendeleza chapa zenye historia ndefu

cri

Mji wa Wuxi ulioko kusini mashariki mwa China ni chimbuko la shughuli za viwanda na biashara ya kitaifa ya zama za karibuni nchini China. Bidhaa za chapa nyingi maarufu zenye historia ndefu zinatengenezwa mjini humo. Chapa hizo ambazo zilianzishwa kwa juhudi na busara za watu wa vizazi kadhaa, ni mali zisizopatikana kwa urahisi. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uungaji mkono wa serikali ya mji huo na juhudi za kampuni husika, kampuni za chapa maarufuzenye historia ndefu zimeanza tena kupata maendeleo.

Wachina wanapozungumzia mji wa Wuxi hukumbuka bidhaa tatu za kipekee za mji huo, yaani vinyago vilivyofinyangwa kwa udongo, gluten na chakula cha mbavu za nguruwe kilichopikwa kwa mchuzi wa soya. Kampuni ya Sanfengqiao iliyoanzishwa mwaka 1927 ni kampuni maarufu kutokana na chakula cha mbavu za nguruwe kilichopikwa kwa mchuzi wa soya. Mbavu za nguruwe zilizopikwa na kampuni hiyo ni tamu sana na kinapendwa na wakazi wa mji huo.

Chakula cha Mbavu za nguruwe kilichopikwa na kampuni ya Sanfengqiao si kama tu zinapendwa na wakazi wa mji wa Wuxi, bali pia kinafurahiwa na watu kutoka miji mbalimbali nchini China. Kwenye kampuni hiyo mwandishi wa habari alikutana na Bw. Xu Qing kutoka mjini Shanghai ambaye alikwenda kununua chakula cha mbavu za nguruwe zilizopikwa kwa mchuzi wa soya.

"Nimetoka Shanghai, nimekuja hapa kununua mbavu za nguruwe. Niliifahamu kampuni hii toka zamani, na nimewahi kuja hapa mara kwa mara, chapa ya Sanfengqiao ni maarufu tena chakula cha mbavu za nguruwe kinachopikwa na kampuni hiyo ni kitamu sana."

Kutokana na juhudi za watu wa vizazi kadhaa, kampuni ya Sanfengqiao imekuwa kampuni yenye matawi 13 ambayo kila mwaka inaweza kutengeneza tani elfu 5 za chakula cha mbavu za nguruwe na thamani ya mauzo ni Yuan milioni 100. chakula cha Mbavu za nguruwe zilizopikwa kwa mchuzi wa soya ambazo ni bidhaa muhimu ya kampuni hiyo zinauzwa vizuri nchini China na hata duniani. Kutokana na sifa nzuri ya chapa hiyo, kampuni ya Sanfengqiao imewekwa kwenye orodha ya kampuni za chapa zenye historia ndefu nchini China na wizara ya biashara ya China.

Kuwekwa kwenye orodha hiyo si kama tu kumeipatia kampuni hiyo sifa nzuri, bali pia kumesukuma mbele maendeleo ya kampuni hiyo. Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Sanfengqiao Bw. Hu Yaoming alieleza kuwa katika siku za usoni utaratibu wa kisasa wa uendeshaji utaanzishwa katika kampuni hiyo, ili kuongeza uwezo wa kupata maendeleo endelevu. Alisema,

"Ni lazima kampuni yetu ifanye uvumbuzi ili kupata maendeleo mapya. Kama kampuni yetu haiwezi kukidhi mahitaji ya wateja na haiwezi kwenda na wakati bila shaka itashindwa. Ni lazima tufanye uvumbuzi kwenye sifa na aina za bidhaa, njia na mawazo kuhusu uendeshaji wa kampuni yetu."

Mbali na kampuni ya Sanfengqiao bado kuna kampuni nyingine ambazo zinafanya juhudi kustawisha chapa zenye historia ndefu. Hoteli ya Jufengyuan ambayo ilianzishwa mwaka 1867 katika Enzi ya Qing ni maarufu katika kupika vyakula vya kienyeji vya Wuxi. Vyakula vilivyopikwa kwenye mkahawa wa hoteli hiyo ni vitamu na vyenye ladha ya kipekee. Wakazi wengi wa mji huo wanafahamu vizuri vyakula vilivyopikwa kwenye mkahawa huo. Bw. Li Ke alisema,

"Vyakula vya kienyeji vya Wuxi vilivyopikwa na mkahawa wa Jufengyuan ni maarufu zaidi, kwa mfano nyama iliyopikwa kwa kuchanganywa na maharage yaliyogandishwa na supu ya samaki vyote ni vyakula maarufu vya mkahawa huo."

Vyakula vilivyopikwa na mkahawa wa Jufengyuan ni maarufu mjini Wuxi, hata wafanyakazi wengi wa mikahawa ya miji mingine wanakwenda kujifunza kutoka kwa wapishi wa mkahawa wa Jufengyuan. Wafanyakazi wa mkahawa wa Songhelou wa mji wa Suzhou ambao pia ni mkahawa wenye historia zaidi ya miaka mia moja wanafanya mashindano ya kupika chakula na wafanyakazi wa mkahawa wa Jufengyuan mara kwa mara, ili kuinua uwezo wao wa kupika chakula.

Baada ya kupata maendeleo katika miaka zaidi ya mia 1 iliyopita, Jufengyuan ambayo zamani ilikuwa mkahawa mdogo hivi sasa imekuwa hoteli kubwa ambayo inatoa huduma mbalimbali. Ili chapa hiyo yenye historia ndefu izidi kustawi, katika hali ya hivi sasa yenye fursa nyingi za kupata maendeleo, wafanyakazi wa hoteli hiyo wana imani kubwa na wako tayari kukabiliana na changamoto. Meneja mkuu wa hoteli hiyo Bw. Tang Weiliang alisema,

"Kutokana na utandawazi wa uchumi duniani, sekta za huduma na biashara za China zimefungua mlango, hali hiyo si kama tu ni changamoto kwa maendeleo ya hoteli yetu, bali pia ni fursa nzuri. Tuna matumaini kuwa tutarithi na kuendeleza urithi mzuri wa mapishi ya vyakula vya kienyeji vya Wuxi, na kuwapatia wanunuzi vyakula bora zaidi."

Mjini Wuxi bado kuna kampuni nyingi za chapa zenye historia ndefu kama kampuni ya Sanfengqiao na Hoteli ya Jufengyuan. Kampuni hizo ni za sekta mbalimbali zikiwemo mikahawa, mauzo ya bidhaa ya rejareja, vyakula na dawa. Lakini baadhi ya kampuni hizo zinakabiliwa na matatizo mengi kutokana na ujenzi wa mji, marekebisho ya utaratibu na uendeshaji usio mzuri. Naibu mkurugenzi wa kamati ya uchumi na biashara ya mji wa Wuxi Bw. Huang Jianhua anaona kuwa, chapa zenye historia ndefu ni urithi wa kihistoria na kiutamaduni wenye thamani kubwa, mji huo unachukua hatua ili kustawisha chapa hizo.

"Chapa hizo zenye historia ndefu zimeonesha utamaduni wa mji wa Wuxi na maendeleo ya sekta za viwanda na biashara mjini humo, hivyo zina hakimiliki na athari ya kipekee. Mwanzoni mwa mwaka huu tulianza kutunga mpango wa kustawisha chapa zenye historia ndefu. Baada ya mpango huo kupata maendeleo kadhaa, tutaanzisha shirikisho la chapa zenye historia ndefu. Kama kazi hiyo ikifanikiwa, chapa zenye historia ndefu zitastawi tena."

Bw. Huang Jianhua alisema chapa zenye historia ndefu za mji wa Wuxi ni chapa zilizoanzishwa na wachina kwa kujitegemea katika maendeleo ya sekta za viwanda na biashara za China. Chapa hizo zina msingi na fursa nzuri ya kupata maendeleo na kuwa chapa maarufu kwenye masoko ya nchini na duniani. Ili kustawisha chapa hizo, mji wa Wuxi umezipatia chapa hizo uungaji mkono na misaada mbalimbali, ikiwemo kusukuma mbele mageuzi ya viwanda, kuunga mkono uwekezaji na utoaji wa madeni, kukamilisha utaratibu wa ajira, kuhifadhi urithi wa kiutamaduni na kulinda hakimiliki.

Idhaa ya kiswahili 2007-04-10