Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-10 18:53:18    
Shughuli za "Mwaka wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo" zaendelea vizuri

cri

Huu ni mwaka wa 35 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan uwe wa kawaida, na mwaka huu pia umeamuliwa na viongozi wa nchi hizo mbili kuwa "Mwaka wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo", ambapo nchi hizo mbili zitafanya shughuli za aina mbalimbali za utamaduni na michezo, ili kuongeza zaidi maingiliano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Naibu mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano na nje katika Wizara ya utamaduni wa China Bwana Zhang Aiping alisema, serikali ya China inatilia maanani sana shughuli hizo. Akisema:

Mwaka jana waziri mkuu wa Japan Bwana Shinzo Abe alipofanya ziara nchini China siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa Japan alifikia maoni ya pamoja na waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao kuhusu kuandaa shughuli za "Mwaka wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo" wakati wa kuadhimisha miaka ya 35 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan uwe wa kawaida. China imeanzisha Kamati ya maandalizi inayoundwa na wahusika wa idara na wizara 7 chini ya uongozi wa mwenyekiti wake Bwana Sun Jiazheng ambaye ni waziri wa utamaduni wa China. Na viongozi wa China na Japan wamekubaliana kuwa, ni lazima kuufanya mwaka huu wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo uwe mwaka wa kuongeza maelewano, kuimarisha urafiki na maingiliano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Hali kadhalika Japan pia ilianzisha kamati ya kushughulikia utekelezaji wa mpango husika. Mkurugenzi wa idara ya kamati hiyo Bwana Uchida Kinya alisema:

Mwaka huu ni mwaka wa 35 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya Japan na China uwe wa kawaida, na kuamua mwaka huu wenye umuhimu mkubwa kuwa mwaka wa maingiliano kati ya Japan na China kwenye sekta za utamaduni na michezo, madhumuni yake ni kuongeza zaidi maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili. Naibu mkurugenzi wa Idara ya utekelezaji wa mpango Bwana Kono Akira alisema:

Wazo la mwaka huu wa maingiliano ni kuwajulisha wananchi wa China sura mpya ya Japan na wajapan, pia kuwawezesha wajapan wengi zaidi waelewe utamaduni wa China ili kuhimiza maingiliano na maelewano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili hasa vijana wa nchi hizo mbili.

Kuanzia mwezi Desemba mwaka jana hadi mwezi Januari mwaka huu, kamati ya utekelezaji wa mpango ya Japan zimeanzisha shughuli mbalimbali zinazohusika, kuthibitisha kauli mbiu na alama za shughuli za "Mwaka wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo". Tarehe 5 Aprili mwaka huu, kamati hiyo imewachagua mchezaji filamu maarufu ambaye pia ni mwimbaji maarufu wa Japan Bi. Sakai Noriko na mchezaji wa mpira wa meza wa Japan Bi. Fukuhara Ai kuwa mabalozi wawili wa kuzidisha urafiki kati ya Japan na China.

Na naibu mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano na nje katika Wizara ya utamaduni ya China Bwana Zhang Aiping alisema, tarehe 12 Aprili, China itafanya maonesho ya michezo ya sanaa kwa kufunguliwa kwa "Mwaka wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo"?idara husika za China zimefanya maandalizi ya muda mrefu, ambapo mawaziri wakuu wa China na Japan watatazama maonesho hayo ya michezo ya sanaa.

Bwana Kono Akira wa idara husika ya Japan alieleza imani yake kuwa, shughuli mbalimbali hakika zitaongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wa Japan na China.