Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-11 19:20:59    
Mapishi ya mseto wa kuku

cri

Mahitaji

Pilipili mboga moja, nyama ya kuku gramu 50, yai moja, mboga gramu 20, vitunguu maji gramu 5, bakuli moja la wali, sosi ya kambamti gramu 5, chumvi gramu 5.

Njia

1. kata pilipili mboga na nyama ya kuku iwe vipande vipande na kasha livunje yai na vilikoroge yai.

2. washa mototia mafuta kwenye sufuria, halafu mimina yai lililokorogwa, likaange yai na lipakue

3. washa moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, na korogakoroga kasha tia vipande vya nyama ya kuku, na vikoroga, halafu tia mboga na vipande vya pilipili mboga, sosi ya kambamti, na korogakoroga, halafu tia wali, na punguza moto, baada ya kupunguza moto korogakoroga kwa haraka, tia chumvi pamoja na chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, kasha ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.