Ufunguzi wa Mwaka 2007 wa maingiliano kati ya China na Korea ya kusini ulifanyika usiku wa tarehe 10 Aprili kwenye Jumba la michezo ya sanaa la taifa huko Seoul, mji mkuu wa Korea ya kusini. Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao ambaye yuko ziarani nchini Korea ya kusini na waziri mkuu wa Korea ya Kusini Bwana Han Duck Soo walihudhuria ufunguzi huo. Ufunguzi huo uliandaliwa chini ya uongozaji wa wasanii wa nchi mbili China na Korea ya kusini, na waendeshaji wa China na Korea ya kusini waliendesha pamoja ufunguzi huo.
Huu ni mwaka wa 15 tangu China na Korea ya kusini zianzishe uhusiano wa kibalozi. Mwishoni wa mwaka 2005, Marais wa China na Korea ya kusini waliamua kuwa mwaka 2007 uwe mwaka wa maingiliano kati ya China na Korea ya kusini, ili kuongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili, na kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano na uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili kwenye sekta mbalimbali. Ili kuandaa vizuri shughuli mbalimbali za mwaka huu wa maingiliano, kila upande ulianzisha kamati ya maandalizi inayoundwa na maofisa wa idara mbalimbali zinazohusika, pia kuanzisha ukurasa maalum kwenye tovuti za mtandao wa internet. Shughuli za mwaka huu wa maingiliano zitakuwa kumi kadhaa, ambazo zinahusu sekta mbalimbali za siasa, uchumi na biashara, utamaduni na elimu, sayansi na teknolojia na michezo.
Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao ambaye alifika Korea ya kusini tarehe 10 asubuhi, pamoja na waziri mkuu wa Korea ya kusini walipanda jukwaani kwa pamoja na kutoa hotuba zenye uchangamfu sana. Bwana Han Duck Soo alisema, Korea ya kusini na China zinakaribiana kijiografia, zinafafana kiutamaduni, na zinasaidiana kiuchumi. Kwenye msingi huo maendeleo ya kasi yamepatikana katika ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye sekta za siasa, utamaduni na uchumi. Alisema:
Katika maingiliano ya utamaduni, "mawimbi ya Korea ya kusini yameibuka nchini China katika mtindo wa kufuata mambo ya kisasa na maonesho ya filamu za televisheni; na nchini Korea ya kusini watu wanapendelea zaidi kwenda China kufanya biashara, kusoma au kutalii, hayo yote yameonesha kuwa, maingiliano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili yameendelea kwa kina kwenye mambo mbalimbali. Alieleza matumaini yake kuwa, kufunguliwa kwa Mwaka wa maingiliano ya Korea ya kusini na China kutaacha kumbukumbu nyingi kwenye historia ya urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Bwana Wen Jiabao alipotoa risala alisema, China na Korea ya kusini zinafanya maingiliano ya kirafiki tangu enzi na dahari. Maingiliano ya kiutamaduni na kibiashara kati ya nchi hizo mbili si kama tu yamesukuma mbele maendeleo ya pamoja ya nchi hizo mbili, bali pia yameweka kumbukumbu mpya kwenye historia ya utamaduni wa kale wa mashariki ya duniani. Maingiliano ya kirafiki kati ya China na Korea ya kusini kwenye sekta ya utamaduni yanafanyika kwenye msingi wa urafiki mkubwa kati ya wananchi wa nchi hizo mbili, na pia yamekuwa msingi imara wa urafiki kati ya nchi hizo mbili. Alisema:
Maingiliano ya kirafiki siku zote ni mambo makuu ya uhusiano kati ya China na Korea ya kusini. Leo tunaandaa kwa pamoja shughuli za Mwaka wa maingiliano kati ya China na Korea, tunatakiwa kufanya maingiliano ya moyoni, kusukuma mbele urafiki na maendeleo ili kujenga siku nzuri za mbele zenye masikilizano na ustawi.
Wasanii wa China na Korea ya kusini walifanya maonesho murua ya michezo ya sanaa kwa watazamaji wapatao zaidi ya 1500.
Watazamaji wa Korea ya kusini waliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa maonesho ya michezo ya sanaa kwenye ufunguzi wa Mwaka wa maingiliano kati ya Korea ya kusini na China yaliwavutia sana, na wana imani kuwa shughuli hizo za maingiliano hakika zitasukuma mbele maingiliano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.
|