Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-12 19:42:43    
Kutangaza mafanikio ya nyuklia kwa Iran kunazingatia zaidi mtizamo wa kisiasa kuliko wa kiteknolojia

cri

Rais Mohmoud Ahmadinejad wa Iran hivi karibuni alitangaza "mafanikio mapya ya nyuklia", yaani Iran hivi sasa imeanza kuzalisha kwa wingi nishati ya nyuklia, mwakilishi wa kwanza wa Iran kwenye mazungumzo ya nyuklia Bw Ali Larijani alihakikisha kuwa, wahandisi wa nchi hiyo wameweka hewa ya UF6 katika kinu cha kuzalisha uranium nzito. Tarehe 10 mwezi Aprili makamu wa rais wa Iran ambaye pia ni mwenyekiti wa idara ya atomiki ya nchi hiyo Bw. Gholam Reza Aghazadeh alisema, Iran imebuni mpango wa kuweka mashinepewa 3,000 kwenye zana za nyuklia zilizoko Natanz. Lakini idadi halisi ya mashinepewa bado haijaweza kuthibitishwa. Hata kama Iran imeshaweka idadi hiyo ya mashinepewa, wachambuzi pia wanashuku kama Iran imeshakuwa na uwezo wa kuendesha mashinepewa 3,000 kwa wakati mmoja. Wataalamu wanasema si sahihi kufikiria kuwa Iran imeshakuwa na uwezo wa kuzalisha kwa wingi nishati ya nyuklia kutokana na upande mmoja tu wa Iran kutangaza hivyo, bali itapata uamuzi baada ya kutolewa matokeo ya uchunguzi wa maofisa wa ukaguzi wa Umoja wa Mataifa.

Lakini ni kwanini Iran inatangaza habari hiyo kwa kukabiliana na shinikizo, na huku vyombo vya habari vikiwa na mashaka? Wachambuzi wanasema msimamo mkali wa Iran kuhusu suala la nyuklia ni kutokana na mawazo yake.

Kwanza, Iran inaona kuwa endapo itasitisha shughuli zake za kusafisha uranium kwa kufuata matakwa ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, itaonesha udhaifu wake mbele ya baraza la usalama. Nchi tatu za Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani bado zinashikilia kutatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya kidiplomasia na mazungumzo. Iran inafahamu vizuri kikomo cha msimamo wa nchi hizo tatu: hata nchi hizo tatu zinataka Iran lazima isitishe shughuli zake za kusafisha uranium, Iran bado inaweza kudumisha utafiti wake kuhusu mashinepewa. Hivyo ingawa Iran imewekewa vikwazo mara mbili na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na suala la nyuklia, lakini Iran inatarajia kutangaza "mafanikio ya nyuklia" kuwa uwezo wa kuongeza uzito wa maneno yake kwenye mazungumzo yatakayofanyika kati yake na nchi tatu za Umoja wa Ulaya.

Pili, ukweli ni kwamba Marekani inatumia vigezo viwili kuhusu suala la nyuklia, ambayo inafanya Iran kushikilia msimamo mkali kuhusu suala la nyuklia. Mwishoni mwa karne iliyopita wakati India ilipofanya majaribio ya nyuklia, Marekani iliiwekea vikwazo India na kuzuia usafirishaji wa nishati na teknolojia za nyuklia kwa India. Lakini hapo baadaye kutokana na maslahi yake yenyewe Marekani ililegeza vikwazo dhidi ya India na kusaini mkataba wa ushirikiano wa matumizi ya nyuklia ya kiraia na India. Iran iliilazimisha jumuiya ya kimataifa kuitambua India kuwa nchi yenye nyuklia kutokana na uendelezaji wa teknolojia ya nyuklia, hivyo Iran pia inatarajia kutoa habari mara kwa mara kwa nchi za magharibi kuwa "mpango wa nyuklia wa Iran umepata maendeleo" ili kuzilazimisha nchi za magharibi kutambua maendeleo ya mpango wake wa nyuklia.

Wachambuzi wa habari wanasema, kwa nchi ya Iran, ingawa kuna mfano wa India, tena mazungumzo ya nyuklia hayajafungwa kabisa, lakini "mafanikio ya nyuklia" iliyoyatangaza Iran si lazima yailetee manufaa.

Kwani Marekani, ambayo ni nchi muhimu sana katika suala la nyuklia la Iran, haitalegeza msimamo wake kwa urahisi kutokana na habari iliyotangazwa na Iran. Katika siku ambayo Bw Ahmadinejad alitangaza habari hiyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bw Sean McCormack alisema, vitendo vya Iran vimethibitisha tena kuwa, Iran inadharau maazimio husika ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Nia ya kitendo hicho cha Marekani ni kuifahamisha Iran kuwa, Marekani haitabadilisha msimamo wake kuhusu Iran kutokana na kutangazwa mafanikio yake ya nyuklia ila tu kufuata maazimio husika ya baraza la usalama na kusitisha mara moja shughuli za kusafisha uranium.