Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-16 19:42:49    
Kwenda kuangalia taa za jadi mkoani Qinghai

cri

 

Katika kipindi hiki cha utalii nchini China tunawafahamisha taa nyingi zilizopangwa kwenye mstari, ambazo ni vitu vya sanaa ya jadi vya wilaya Huangyuan, mkoani Qinghai ulioko kwenye sehemu ya magharibi mwa China. Taa za Huangyuan zimekuwa na historia ya zaidi ya miaka 200, taa za Huangyuan ni zenye maumbo mbalimbali na rangi za kuvutia, kwenye taa za Huangyuan, ambazo ni vitu vya sanaa, kuna michoro iliyochorwa kwa ufundi mkubwa, hivyo zinawavutia sana watu. Mwaka 2005, taa za Huangyuan ziliorodheshwa kuwa mabaki ya kundi la kwanza ya kiutamaduni yasiyo ya vitu na zinalindwa kitaifa.

Bw. Jingshi alianza kufanya utafiti kuhusu taa za Huangyuan toka miaka mingi iliyopita. Alisema taa za Niyuan zimekuwa na historia ndefu na zilianza kuwepo katika kipindi cha kati cha enzi ya Qing zaidi ya miaka 200 iliyopita. Wakati ule wafanyabiashara wa Huangyuan walitengeneza taa zenye matangazo ya biashara kwenye sehemu ya nje na zenye mishumaa iliyowaka ndani yake ili kuvutia wateja wakati wa usiku. Hapo baadaye taa za aina hizo zilitengenezwa kwa ufundi mkubwa zaidi, zikawa na vitako, michoro na maumbo mbalimbali, baada ya kupita miaka kadhaa tena, taa za aina hiyo zenye matangazo zilibadilishwa kuwa taa nyingi kubwa zinazopita juu ya barabara.

Kila moja ya taa zilizopangwa katika mstari ni kitu kimoja cha sanaa. Mchakato wa utengenezaji wa taa za Huangyuan ni kama ufuatao: Kwanza, kutengeneza maumbo yake, ambayo moja ni la kutundikwa na lingine ni la kukaa chini, kuna maumbo zaidi ya 10 ya taa yakiwemo ya maua ya plum, mstatili na kipepeo, halafu michoro ya maua, majani na watu inachorwa kwenye frame za taa. Baada ya frame za taa kutengenezwa tayari, fremu hizo zinafunikwa kwa aina ya kitambaa chembamba na chepesi cha shashi, kisha michoro kuhusu hadithi zinazopendwa sana na watu, desturi na mila, mambo ya watu mashuhuri na hadithi kuhusu malaika, inachorwa kwenye kitamba hicho. Bw. Jingshi alisema, kila ifikapo usiku, mistari ya taa huwa inawaka kwenye mji wa Huangyuan, desturi hiyo inaendelea hadi sasa. Katika kipindi cha siku kuu ya taa ya tarehe 15 mwezi wa kwanza kwa kalenda wa kichina, shughuli kubwa za maonesho ya taa hufanyika huko. Alisema,

"Nchini China kuna jadi ya kushiriki kwenye maonesho ya taa katika sikukuu ya taa ya tarehe 15 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, kwa kuendana na kuiendeleza mila hiyo, watu wa mji wa Huangyuan wametengeneza taa zinazopangwa katika mstari. Kila ikifika usiku wa tarehe 15 mwezi wa kwanza, mistari mia kadhaa ya taa inaangaza kwa mwangaza mwingi mtaa mzima wa mji huo."

 

Tarehe 4 mwezi Machi mwaka 2007 ilikuwa siku kuu ya taa ya China. Maonesho ya kwanza ya mistari ya taa yalifanywa kwenye uwanja wa mji wa Xining mkoani Qinghai. Usiku huo zaidi ya mistari 400 ya taa iliwafurahisha sana watalii wa nchini na wa nchi za nje. Kila taa ina urefu wa mita 2 na kimo cha sentimita 60, taa hizo zinaning'inizwa kwenye fremu za chuma au kuwekwa chini. Watu wanapotembea katikati yake, wanaona kuwa, mto wa taa wa chini umeungana na nyota za angani, tena wanajisikia wao wenyewe wako mbinguni na kuburudishwa mno. Bibi Li Yun, ambaye ni mwenyeji wa huko, alitoka nyumbani kuangalia taa kila siku katika siku zile na kupiga picha nyingi mbele ya taa.

"Mwaka huu zimeoneshwa taa nyingi sana, watazamaji pia ni wengi, tunakutakia nyumbani kwetu na nchi yetu ziwe na hali motomoto kama taa hizo"

Taa zilizooneshwa katika maonesho ya mwaka huu, si kama tu zimedumisha ufundi wa utengenezaji, bali pia zilitumia teknolojia ya kisasa ya elektroniki, mwangaza na sauti pamoja na vifaa vya aina mpya, licha ya hayo michoro iliyoko kwenye taa pia ilikuwa ya kupendeza zaidi. Mbali na kutumia michoro ya kawaida, vilitumika tarizi, picha za kivuli na ukataji karatasi. Michoro iliyoko kwenye taa hizo ni pamoja na mambo na hadithi yaliyoko katika vitabu vya fasihi, mandhari nzuri na mabaki ya mkoa wa Qinghai, ambayo inaonesha utamaduni na sura ya jiografia ya China. Msanii wa huko Bw. Ren Yugui alisema,

"Michoro iliyoko kwenye taa za mwaka huu, ni pamoja na hadithi za malaika na hadithi za kihistoria pamoja na hadithi za jadi, kuangalia kwa mchakato wa maendeleo ya mistari ya taa ya mji wa Huangyuan, taa hizo ni za kuunganisha utamaduni wa jadi na sayansi na teknolojia ya kisasa."

Bw. Ren Yugui alisema, taa za mji wa Huangyuan ni vitu vya sanaa ya kiwango cha juu vyenye aina nyingi za utamaduni, zimekusanya ufundi na sanaa za kazi za seremala, uchongaji, uchoraji, mapambo, tarizi, picha za vivuli, sanaa ya kuandika na muziki, zikionesha kuwa watu wa huko kupenda kwao na mustakabali mzuri wa maisha.

Katika miaka ya karibuni, wilaya ya Huangyuan imenuia kufanya taa za Huangyuan kuwa kitu maarufu cha kiutamaduni, imetenga fedha zaidi ya Yuan milioni 1 ili kuanzisha kampuni ya utafiti na utengenezaji wa taa, kununua zana na vyombo, kukusanya data husika, kuanzisha hifadhi ya mafaili, kuandaa mabingwa wanaorithi ufundi wa taa za jadi, kuchapisha vijitabu vya matangazo, na imeshirikisha wataalamu, wasanii na mafundi wenyeji ili kuhifadhi, kuendeleza na kufanya mageuzi ya kisanaa kuhusu taa za jadi. Mkuu wa wilaya ya Huangyuan Bibi Ma Yuying alisema,

"Mistari ya taa za Huangyuan ni vitu bora vya sanaa vyenye aina nyingi za utamaduni, tunawakaribisha marafiki wa nchi mbalimbali waje mkoani Qinghai kuangalia taa zetu na kufahamu sanaa na jadi ya Huangyuan."

Idhaa ya Kiswahili 2007-04-16