Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-17 19:34:05    
China imeonesha juhudi zake za kiujenzi katika suala la Darfur

cri

Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Zhai Jun hivi karibuni akiwa mjumbe maalum wa serikali ya China alifanya ziara nchini Sudan. Alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari kwanza alimwambia kuwa, maendeleo mapya yamepatikana katika suala la Darfur, kwani ameambiwa na balozi wa Sudan nchini China kuwa, Sudan, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zimefikia kauli moja katika mambo yote ya utekelezaji wa kipindi cha pili wa pendekezo la amani la Bwana Kofi Annan. Bwana Zhai Jun alisema:

China inaweza kufanya juhudi za kiujenzi katika mambo yote ya utatuzi wa suala la Sudan, na siku zote China inafanya juhudi hizo. China ni nchi mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, pia ni nchi rafiki wa Sudan, China haitaki kuona mgogoro unatokea katika nchi rafiki yake, kwani hali isiyo ya utulivu na matatizo mengine yanaweza kuathiri maendeleo ya nchi hiyo. Kwa jumla China imefanya juhudi kubwa na zenye ufanisi kusaidia kutatua mgogoro wa Darfur. Kwa mfano, mshauri wa Rais wa Sudan alipoitembelea China, mjumbe wa taifa wa China Bwana Tang Jiaxuan pia alikuwa na mazungumzo naye. China pia imefanya mawasiliano ya karibu na majadiliano ya mara kwa mara na nchi wajumbe wa Baraza la usalama, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Hivyo tunaweza kusema kuwa China imeonesha umuhimu wake mkubwa katika kuiwezesha Sudan ikubali pendekezo la Bwana Annan. Bwana Zhai Jun alisema:

Hivi karibuni nilifanya ziara nchini Sudan, nilikwenda kwenye sehemu ya Darfur na kutembelea kambi tatu za wakimbizi ambazo ni kubwa zaidi katika sehemu hiyo. Niliona hali ya jumla ya sehemu nilizokwenda ni ya utulivu, siyo mbaya sana kama watu wa nchi za magharibi wanavyosema, na serikali ya Sudan inaweza kudhibiti hali ya mambo. Lakini kuwepo kwa kambi za wakimbizi kunaonesha kuwepo kwa matatizo ya wakimbizi na matatizo ya kibinadamu, lakini niliona hali ya jumla ya kambi hizo si mbaya, maisha ya wakimbizi yanaweza kuhakikishwa, sehemu hiyo hakuna vurugu.

Lakini hivi karibuni, lawama fulani dhidi ya China zimekuwa zikitokea duniani, watu fulani wanaona makampuni ya China kuwekeza nchini Sudan na China kuiuzia Sudan silaha kumechangia mgogoro wa sehemu ya Darfur, hivyo China inapaswa kuwajibika na msukosuko wa kibinadamu huko Sudan. Bwana Zhai Jun alisema:

Malalamiko hayo hayana msingi hata kidogo. Kwani Darfur iko mbali na China, tatizo la Darfur lilisababishwa na hali ya kunyang'anya maliasili ya maji na majani kati ya makabila mbalimbali ya huko, China haiwajibiki na hali hiyo. Watu fulani wanataka kusema kuwa, uhusiano kati ya China na Sudan ni mzuri, hivyo China inatakiwa kuwajibika na suala la Darfur. Kweli kuna uhusiano mzuri kati ya China na Sudan, uhusiano huo ni wa kunufaishana, ambao unalingana na kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani. China imetoa misaada kadhaa kwa Sudan ikilenga kuisaidia Sudan kujiendeleza na kuboresha maisha ya wananchi wa Sudan. Suala la Sudan kijuujuu ni suala la mgogoro wa kijeshi, lakini kama wananchi wa Sudan wanaweza kuishi maisha mazuri, na uchumi wa Sudan unaweza kupata maendeleo makubwa, tunaona matatizo yote yatatoweka.

Bwana Zhai Jun alisema watu fulani wanahusisha silaha za sehemu ya Darfur na China, hii haina msingi hata kidogo. Kwani China ikifuata kwa makini kanuni zilizowekwa inauza silaha chache sana kwa nchi zenye mamlaka kwa lengo la kujilinda kwa nchi hizo, wakati wa kuuza silaha hizo China inapata dhamana husika.

Bwana Zhai Jun alisema, watu fulani waliotishia kususia Michezo ya Olimpiki ya Beijing ili kushinikiza serikali ya China ni wa aina mbili, wa kwanza ni wajinga, na wa pia ni watu wenye nia ovu. Alisema, Michezo ya Olimpiki ya Beijing ni jambo kubwa katika michezo ya Olimpiki, kanuni moja ya Olimpiki ni kutoifanya michezo iwe ya kisiasa, hivyo kuhusisha mambo tofauti hakulingani na kanuni hiyo. Na watu fulani hawajawahi hata kwenda Darfur na hata hawajui suala la Darfur ni suala la namna gani, hali kadhalika hawaelewi msimamo na umuhimu wa China katika suala la Darfur, na wao kutoa tishio hakika wana kusudi baya.

Idhaa ya Kiswahili 2007-04-17