Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-18 14:40:05    
Mapishi ya doufu na viazi

cri

Mahitaji

Doufu gramu 250, viazi gramu 50, vitunguu maji na tangawizi kila kimoja gramu 5,chumvi gramu 3, pilipili manga gramu 5, mchuzi wa sosi gramu 5, kiligirani gramu 10.

Njia

1. kata viazi na doufu ziwe vipande, kata vitunguu maji na tangawizi ziwe vipande.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe na joto la nyuzi 80, tia vipande vya doufu na viazi vikaange, mpaka viwe rangi ya hudhurungi, kisha vipakue.

3. washa moto tena, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, pilipili manga korogakoroga, mimina mchuzi wa sosi na maji, tia vipande vya viazi, baada ya kuchemka, tia vipande vya doufu, chumvi, punguza moto endelea kuchemsha kwa dakika 3, vipakue. Tia vipande vya kisibiti, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.