Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-20 17:57:00    
Kufuata njia ya maendeleo ya utandawazi wa miji kwa kufuata hali halisi ya nchi

cri

Mkutano wa 21 wa Baraza la Shirika la mipango ya makazi ya binadamu la Umoja wa Mataifa unaendelea kufanyika huko Nairobi Kenya, kiongozi wa ujumbe wa China ambaye pia ni naibu waziri wa ujenzi wa China Bibi Fu Wenjuan alipotoa hotuba kwenye Mkutano huo alisema, ili kusukuma mbele maendeleo endelevu ya utandawazi wa miji, ni lazima kushikilia njia ya kufuata hali halisi ya nchi.

Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, mwaka 2007 utafungua ukurasa mpya wa historia ya binadamu, kwamba kuanzia sasa, kila watu wawili kote duniani mmoja ni mkazi wa mjini, na binadamu wameanza kuingia kwenye zama za utandawazi wa miji. Na asilimia 95 ya ongezeko la idadi ya wakazi wa mijini itaonekana katika nchi zinazoendelea. China ikiwa nchi kubwa kabisa inayoendelea, mchakato wa utandawazi wa miji unaendelea kwa kasi vilevile. Bibi Fu Wenjuan alisema:

China iko katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya utandawazi wa miji. Mwaka 2006, kiwango cha utandawazi wa miji nchini China kiliongezeka na kufikia asilimia 43.9 kutoka asilimia 26.4 ya mwaka 1990, na kila mwaka watu kati ya elfu 10 na elfu 13 hivi wanahamia mijini kutoka vijijini.

Kuharakishwa kwa mchakato wa utandawazi wa miji kunapohimiza ongezeko la uchumi pia kunasababisha matatizo mengi, hasa tatizo la umaskini, na tatizo la upanuzi wa makazi ya hali duni mijini

yamekuwa ni matatizo makubwa kote duniani. Takwimu zilizotolewa na idara husika ya Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, mwaka 2007, watu wapatao bilioni moja kote duniani wataishi katika nyumba zenye hali duni mijini. Ili kuifanya dunia nzima ifuatilie suala hilo, Shirika la mipango ya makazi ya binadamu la Umoja wa Mataifa limeweka kauli mbiu ya mkutano huo kuwa ni "maendeleo endelevu ya utandawazi wa miji?kuweka mkazo katika kufanya mipango ya fedha na mpangilio wa miji ili kupunguza hali ya umaskini mijini. Bibi Fu Wenjuan alisema:

Mfumo wa China ni tofuati na nchi nyingine, baada ya wakulima kuhamia mijini, nyumbani kwao vijijini bado kunakuwa na mashamba yao, hii ni kazi nzuri iliyofanyika nchini China. Kwani kama wakulima walioingia mijini watapokeza ajira, wanaweza kurudi nyumbani kwao kuendelea na kilimo. Lakini kama wakihamia kabisa mijini, kama hawataweza kupata ajira za kudumu, watakuwa wakazi wa mijini wanaoishi hali ya umaskini.

Lakini katika miji ya China, vilevile kuna sehemu fulanifulani ambapo watu kadhaa wenye matatizo ya kiuchumi wanajenga vibanda vya kuishi, hata kuna "kijiji cha mjini" katika miji mbalimbali mikubwa, Bibi Fu Wenjuan alisema:

Serikali ya China inatilia maanani kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi au wenye mapato ya chini kupata nyumba za kuishi, na kutoa sera mbalimbali za kukidhi mahitaji ya watu wenye hali tofauti.

Wakati wa kutatua suala la makazi mijini, serikali ya China pia imesisitiza kudhibiti mpangilio wa makazi ili ujenzi wa makazi uwe na mpangilio mwafaka, na kushikilia kuleta maendeleo ya uwiano ya miji mikubwa, wastani na midogo, ili maendeleo ya mchakato wa utandawazi wa miji yalingane na mazingira na raslimali. Alisema:

Mji wa Yantai ni mfano mzuri katika maendeleo endelevu ya mji nchini China. Mji huo haukubomoa nyumba nyingi zilizojengwa zamani, bali zilifanya ukarabti wa miundo mbinu kwenye sehemu ya makazi yaliyojengwa zamani, kufanya hivyo kumesifiwa na watu wengi.

Kwa kuwa serikali ya China imeshikilia kithabiti utekelezaji wa mkakati wa maendeleo endelevu, hivyo mafanikio dhahiri yamepatikana katika kusukuma mbele maendeleo mazuri ya utandawazi wa miji, kuongeza nafasi za ajira ili kupunguza umaskini, na kuboresha mazingira ya makazi ya binadamu.

Lakini Bibi Fu Wenjuan alisema, hali isiyo ya uwiano kati ya maendeleo ya miji na vijiji nchini China bado inaonekana dhahiri sana, China inatakiwa kufanya juhudi kubwa na za muda mrefu, ili kutimiza lengo la kutokomeza umaskini na kuwawezesha wananchi wote waishi maisha mazuri.