Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-25 18:17:10    
Mapishi ya vichipukizi vya mianzi na mbavu za nyama ya nguruwe

cri

Mahitaji 

Vichipukizi vya mianzi gramu 200, nyama za mbavuni nyama ya nguruwe gramu 100, pilipili manga gramu 5, vipande vya tangawizi gramu, mchuzi wa sosi vijiko vitatu, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, chumvi vijiko viwili, sukari kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja.

Njia

1. ondoa gamba la mizizi ya vichipukizi vya mianzi, osha mbavu za nyama ya nguruwe na uzikate ziwe vipande.

2. washa moto halafu tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi, korogakoroga, tia vipande vya nyama za mbavuni ya nguruwe, korogakoroga, tia vichipukizi vya mianzi, mimina mvinyo wa kupikia, mchuzi wa sosi, mimina maji chemsha kwa nusu ya saa, tia chumvi, sukari, chembechembe za kukoleza ladha. Vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.