Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-25 18:50:40    
Kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya ndani wa Palestina kumeonesha mgongano kwenye eneo la usalama

cri

Waziri wa mambo ya ndani wa Palestina Bw. Hani Kawasmeh tarehe 23 mwezi Aprili alimkabidha waziri mkuu Ismail Haniyeh ombi la kujiuzulu. Ingawa ombi hilo lilikataliwa, na Bw. Hani Kawasmeh aliamua kubaki na wadhifa huo, lakini wachambuzi wanaona kuwa kwa kiwango fulani, kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya ndani wa Palestina, kunaonesha mgongano katika eneo la usalama ndani ya serikali ya nchi hiyo.

Vyombo vya habari vya Israel tarehe 24 mwezi Aprili vilitoa habari zikisema, Bw. Mohammed Madhoun ambaye ni msaidizi wa waziri mkuu Ismail Haniyeh alithibitisha kuwa, Bw. Hani Kawasmeh alitoa ombi hilo kwenye mkutano wa baraza la serikali ya Palestina uliofanyika tarehe 23. Katika ombi lake hilo alieleza kutoweza kupata maendeleo kwa mpango wake wa kumaliza vurugu kwenye sehemu za Palastina na kurudisha utaratibu wa sheria na jamii ya huko.

Hapo baadaye ofisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Palestina alidokeza kuwa, mpango wa Bw. Hani Kawasmeh ni kufanya mageuzi kuhusu vikosi kadhaa vya usalama vya Palestina vilivyokumbwa na matatizo ya ufisadi na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na kufanya usimamizi mkali kuhusu vitendo vya kuwa na silaha kwenye mahali pa umma. Mpango huo ni mzuri kwenye kuimarisha usalama wa Palestina na kuzuia mapambano makubwa, lakini mpango huo ulikwama kutokana na kukosa ushirikiano wa viongozi husika wa idara ya usalama. Licha ya hayo Bw. Hani Kawasmeh alilalamika kwa kukosa madaraka ya kutosha katika kuchukua uamuzi.

Japokuwa hatimaye Bw. Hani Kawasmeh aliamua kubaki madarakani, na kitendo chake hicho kimetoa shinikizo kwa viongozi husika wa Palestina, lakini wachambuzi wamesema kutaka kwake kujiuzulu kunaonesha kuwa mgongano wa makundi mawili makubwa katika eneo la usalama wa nchi bado haujaondolewa kabisa.

Mwezi Februali mwaka huu, kabla ya kundi la chama cha ukombozi wa Palestina Fatah kusaini "makubaliano ya Mecca" na kundi la kiislamu nchini Palestina, Hamas, majeshi ya pande hizo mbili yalipambana kwa muda wa miezi kadhaa, na kusababisha vifo vya watu na majeruhi wengi, ingawa "makubaliano ya Mecca" yaliweka kanuni za kusimamisha mapigano kwa pande mbili, lakini hazikuafikiana kuhusu suala muhimu la madaraka ya udhibiti ya majeshi ya usalama ya Palestina, tena suala kuhusu kuondolewa na la kuhusu "jeshi la utekelezaji" la Hamas, ambalo lilileta wasiwasi mkubwa kwa uhusiano wa pande hizo mbili, pia halikutatuliwa. Ingawa katika wakati wa mwisho wa mazungumzo ya "marathon" yaliyofanyika hapo baadaye kati ya pande hizo mbili, yalithibitisha mteule wa nafasi ya waziri wa mambo ya ndani, na kuondolea mbali vikwazo kwa uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Lakini vyombo vya habari vimeona kuwa, tangu kuasisiwa kwa serikali mpya ya Palestina, vyombo vya habari vilitoa habari chache sana kuhusu Bw. Hani Kawasmeh na maendeleo aliyopata katika uendeshaji utawala isipokuwa vilitoa habari nyingi kuhusu migongano kati ya Fatah na Hamas; mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas bado anatekeleza mpango wake wa usalama.

Tarehe 18 mwezi Machi ambayo ilikuwa siku ya pili tangu kuapishwa kwa serikali mpya ya Palestina, alimteua kiongozi kijana wa Fatah Bw. Mohammad Dahlan kuwa mshauri wa usalama wa taifa akisimamia majeshi yote ya usalama nchini Palestina. Tarehe 15 mwezi Aprili, Abbas alitoa amri ya mwenyekiti akitaka iundwe kamati ya usalama ya Palestina ili kuunganisha majeshi ya Palestina na kupunguza mapambano ya kisilaha ndani ya nchi hiyo. Kundi la Hamas lilinung'unika kuhusu uamuzi wa Bw Abaas kumwingiza Bw Mahammad Dahlan katika kamati ya usalama ya taifa, ambaye hana uhusiano mzuri na kundi la Hamas, pia lilitoa malalamiko kuhusu kundi la Fatah kuendelea kuhodhi nafasi muhimu katika idara za usalama.

Ingawa sasa Hani Kawasmeh ameondoa ombi la kujiuzulu, lakini suala la udhibiti wa majeshi kati ya makundi makubwa mawili ya Palestina bado halijatatuliwa kimsingi, jambo hilo litakuwa na hatari kwa utulivu wa nchi hiyo katika siku za baadaye.