Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-02 20:09:56    
Mapishi ya nyama ya kondoo

cri

Mahitaji: Nyama ya kondoo gramu 500, karoti moja, vipande vya vitunguu maji gramu 5, nusu ya figili, mchuzi wa sosi vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, unga wa pilipili manga kijiko kimoja

Njia:

1. osha nyama ya kondoo, kuchemsha maji tia vipande vya nyama ya kondoo na figili, baada ya kuchemka, ondoa figili na pakua nyama ya kondoo.

2. kata karoti iwe vipande, washa moto tia vipande vya vitunguu maji na nyama ya kondoo kwenye sufuria, korogakoroga, tia chumvi, sukari, unga wa pilipili manga, mimina mchuzi wa sosi, korogakoroga, halafu mimina maji, baada ya kuchemka, punguza moto, tia vipande vya karoti, endelea kuchemsha mpaka maji yakauke, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.