Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-03 19:15:51    
Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la usalama wa Iraq wafanya juhudi kuboresha usalama nchini Iraq

cri

Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la usalama wa Iraq ambao pia ni mkutano wa wajumbe wa makubaliano ya kimataifa kuhusu Iraq, unafanyika mjini Sham el-Sheikh tarehe 3 na tarehe 4. Mkutano huo utafanya juhudi kuboresha hali ya usalama nchini Iraq, kusukuma mbele mazungumzo na ushirikiano kati ya Iraq na nchi jirani, na kuanzisha rasmi mpango wa makubaliano ya kimataifa ya Iraq (ICI) unaoisaidia Iraq kufanya ukarabati.

Nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, nchi wajumbe wengine wa kundi la nchi nane zikiwemo Ujerumani, Japan, Italia na Canada, wajumbe wa Misri, Bahrain na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) watahudhurai Mkutano huo.

Mkutano huo kwanza utafanya juhudi kuanzisha uhusiano wa kiwenzi kati ya Iraq na jumuiya ya kimataifa, na kuisaidia serikali ya Iraq kukabiliana na changamoto kwa mchakato wa ukarabati kwenye sekta za siasa, uchumi na jamii. Huu ni mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu suala la Iraq ndani ya miezi miwili baada ya mkutano wa kimataifa wa ngazi ya mabalozi kuhusu suala la Iraq uliofanyika mwezi Machi mjini Baghdad, na mkutano huo ni wa ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje. Hii imeonesha matumaini makubwa ya serikali ya Iraq kuhusu kuboresha hali ya usalama nchini humo na kupata misaada ya kijamii na kiuchumi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa wakati inapofanya ukarabati wa nchi, pia imeonesha ufuatiliaji mkubwa wa jumuiya ya kimataifa kuhusu suala la Iraq.

Aidha mkutano huo utafanya majadiliano kuhusu uwezekano wa kuboresha hali ya usalama mapema kwa kutuma kikosi cha kulinda usalama nchini Iraq. Wajumbe watakaohudhuria mkutano huo wanatoka nchi kubwa na mashirika ya kikanda ambazo ni zenye athari kubwa kuhusu suala la Iraq. Wote wanaona kuwa jambo muhimu zaidi ni kuisaidia Iraq kurejesha usalama na kutuliza hali nchini humo, halafu kuanzisha utaratibu mzuri wa utawala. Mkutano huo utafanya majadiliano kuhusu kutuma kikosi cha kulinda usalama kinachoundwa na askari wa nchi za kiarabu kwenda Iraq, au kuisaidia serikali ya Iraq kuunda kikosi cha ulinzi wa usalama kupitia Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya hayo, mkutano huo utasukuma mbele na kuimarisha mazungumzo na ushirikiano kati ya serikali ya Iraq na nchi jirani. Nchi za Kiarabu zitakazohudhuria mkutano huo zimesema zinafuatilia sana suala la Iraq, na kutumai kutoa mchango mkubwa kwenye utatuzi wa suala hilo. Nchi hizo pia zimesema zitatoa uungaji mkono mkubwa wa kisiasa kwa serikali ya Iraq, na kutoa mwito wa kuzitaka jumuiya ya kimataifa hasa nchi za Ghuba na nchi zilizoendelea kutoa msaada wa kiuchumi kwa serikali ya Iraq. Hii imeonesha kuwa nchi kubwa za Mashariki ya Kati zikiwemo Misri, Syria na Iran zinapenda kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye suala la Iraq na kuongeza athari zao duniani; pia imeonesha wasiwasi ya nchi za Ghuba kuhusu usalama wa sehemu hiyo.

Nne, mpango wa makubaliano ya kimataifa ya Iraq ambao unalenga kuisaidia Iraq kufanya ukarabati unatazamiwa kuanza rasmi. Mwezi Julai mwaka jana kutokana na uungaji mkono wa Benki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na serikali ya Iraq zilianzisha mpango wa makubaliano ya kimataifa ya Iraq. Mpango huo unahusiana na sekta za siasa, uchumi, jamii na usalama za Iraq, lengo la mpango huo ni kusukuma mbele maendeleo ya taifa na mchakato wa mageuzi ya uchumi wa Iraq, kuisaidia Iraq kusimamia vizuri maliasili za jamii; pia unaitaka jumuiya ya kimataifa iongeze uwekezaji na msaada wa kifedha, kupunguza au kufuta madeni na kutoa uungaji mkono kuhusu usimamizi na utaalamu kwa serikali ya Iraq. Aidha wajumbe wa makubaliano ya kimataifa ya Iraq watatoa ahadi kuhusu utekelezaji wa mpango huo, kutoa msaada kwa mpango wa maendeleo na mageuzi ya Iraq katika miaka mitano ijayo, kuimarisha uwekezaji, na kuisaidia serikali ya Iraq kukabiliana na changamoto na kutekeleza mpango wa ukarabati wa nchi na maendeleo ya uchumi.