Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-09 20:34:27    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na njegere

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 300, karoti moja, njegere gramu 150, vipande vya vitunguu maji,, tangawizi na vitunguu saumu kila kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, mchuzi wa sosi vijiko viwili, sukari vijiko viwili, siki vijiko viwili, maji ya wanga vijiko vitano.

Njia

1. osha nyama ya ng'ombe, halafu uikate iwe vipande vidogovidogo, ondoa maganda ya karoti halafu uikate iwe vipande vidogovidogo.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia njegere, kaanga, halafu ziapkue.

3. washa moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi na vitunguu saumu kwenye sufuria korogakoroga, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, korogakoroga, halafu tia vipande vya karoti, korogakoroga, tia sukari, siki, mchuzi wa sosi, chumvi, korogakoroga, mimina maji ya wanga, korogakoroga tia njegere korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.