Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-11 19:18:59    
Boma la Marwi-ushahidi mkubwa wa urafiki kati ya China na Sudan

cri

Boma la Marwi lililoko kwenye sehemu ya kaskazini ya Sudan, ni kituo kikubwa cha pili cha kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji kilichojengwa kwenye mto Nile baada ya Boma la Aswan nchini Misri, pia ni mradi mkubwa kabisa wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji nchini Sudan hata barani Afrika. Boma hilo linachukuliwa kuwa ni mfano mpya wa urafiki kati ya China na Sudan. Tarehe 20 mwezi Mei mwaka 2003, kampuni ya CCMD JV ya China ilipata kandarasi ya ujenzi wa Boma la Marwi, meneja mkuu wa kampuni hiyo Bwana Zhou Shangmin alisema:

"Mto Nile ni mto mrefu kabisa duniani, Boma la Marwi ni boma kubwa kabisa liliojengwa kwenye mto huo, lina urefu wa kilomita 11, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa boma hilo bila shaka litaleta manufaa makubwa kwa Sudan."

Bw. Zhou alisema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Boma la Marwi, bwawa la Marwi litakuwa na uwezo wa kutunza mita za ujazo bilioni 14 za maji, na kuwanufaisha watu milioni zaidi ya 3. Na ujenzi wa boma hilo pia umetoa nafasi za ajira kwa watu zaidi ya 2500 wa huko. Hivi sasa katika sehemu karibu na Marwi, miundombinu ya aina mbalimbali kama vile barabara, shule, hospitali na uwanja wa ndege imejengwa, lakini miaka 4 iliyopita sehemu hiyo ilikuwa jangwa na ilikuwa na wakazi wachache tu. Mhandisi wa Sudan aliyefanya kazi kwa miaka miwili kwenye boma hilo Bwana Halid Ahmed ameona kihalisi mabadiliko ya maisha yake kutokana na ujenzi wa boma hilo. Alisema:

"Bila shaka ujenzi wa Boma la Marwi utabadilisha hali ya kijamii ya sehemu yetu. Zamani sisi tuliishi maisha magumu kweli, ujenzi wa boma hilo umeongeza mashamba ya kulima, ujenzi wa barabara umetuwezesha kuwasiliana kwa urahisi zaidi, na tatizo la upungufu wa umeme litatatuliwa, naamini kuwa maisha yetu ya siku zijazo yatakuwa mazuri zaidi."

Kwenye Boma la Marwi, wafanyakazi 2400 wa China wanafanya kazi pamoja na wafanyakazi wa huko mchana na usiku, wanapaswa kuvumilia hali ya joto, mashambulizi ya dhoruba ya mchanga na usumbufu wa mbu, lakini hawana malalamiko hata kidogo. Mradi wa Boma la Marwi umesifiwa ni "mradi wa magenge matatu" nchini Sudan, na umefuatiliwa sana na serikali ya China na Sudan. Konsela wa kiuchumi na kibiashara wa China nchini Sudan Bwana Hao Hong alisema, Boma la Marwi ni mradi mkubwa unaohusiana na mpango wa maendeleo ya Sudan na maisha ya watu wa nchi hiyo. Alisema:

"zamani Sudan ilikuwa na kilowatt laki 8 tu umeme, kituo cha kuzalisha umeme cha Boma la Marwi peke yake kitazalisha kilowatt milioni 1. 25 za umeme. Boma hilo likiweza kukamilika kwa wakati mwaka 2008, utoaji umeme nchini Sudan utaongezeka maradufu."

Bw. Hao Hong alidhihirisha kuwa, ushirikiano kati ya makampuni ya China na Sudan kweli ni ushirikiano wa kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili kwenye msingi wa usawa na kunufaishana. Katibu mkuu wa baraza la uenezi la Sudan Bwana Bakri Mulah alisema:

"Boma la Marwi litakuwa boma kubwa kabisa barani Afrika. Kama isingekuwa msaada wa China, basi Sudan isingeweza kukamilisha mradi huo mkubwa. Utoaji kwa mwingi wa umeme wa boma hilo si kama tu utahimiza maendeleo makubwa ya uchumi nchini Sudan, bali pia utazinufaisha nchi za jirani."