Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-14 19:04:35    
Wajenzi wa mradi wa kuzalishaji umeme wa China nchini Sudan

cri

Kwenye jangwa lililoko kaskazini mwa Khartoum, mji mkuu wa Sudan, watu wanaweza kuona minara mirefu ya chuma ya rangi ya fedha, minara hiyo ya nyaya za umeme ni ya mfumo mpya wa umeme kwenye sehemu ya kaskazini mwa Sudan, ambao unajengwa na wahandisi wa kampuni ya mradi wa kuzalisha umeme ya mji wa Harbin wa China.

Kituo cha uzalishaji umeme cha Jili ni mradi wa kwanza wa umeme wa ushirikiano wa China na Sudan, ambao unachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa nchini Sudan. Naibu meneja wa mradi wa umeme wa Sudan wa kampuni ya mradi wa uzalishaji umeme ya Harbin Bw. Xu Hong alisema,

"Ushirikiano wa kwanza kati ya kampuni yetu na Sudan ulianza mwaka 2000 kwa ujenzi wa kipindi cha kwanza wa kituo cha kuzalisha umeme cha Jili. Tulifanya kazi vizuri sana katika mradi huo, kituo hicho kilianza kuzalisha umeme miezi 8 kabla ya wakati uliopangwa. Baada ya kituo hicho kuanza kuzalisha umeme, hali ya upungufu wa umeme kwenye mji mkuu wa Khartoum ilipunguzwa kwa kiasi kikubwa. Kiasi cha uzalishaji umeme wa kituo hicho cha uzalishaji umeme kilichukua 35% ya jumla ya umeme unaozalishwa katika nchi nzima ya Sudan."

Kampuni ya mradi wa uzalishaji umeme ya Harbin pia ilichukua kandarasi ya kujenga boma(ukingo mkubwa ) la bwawa la maji la Marwi, ambalo ni ujenzi wa kipindi cha kwanza cha mradi wa kuzalisha umeme unaochukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa hivi sasa barani Afrika, kampuni hiyo imekabidhiwa kujenga njia ya nyaya za kusafirisha umeme zenye urefu wa kilomita 1,776 , vituo 7 vya kubadilisha nguvu za umeme, ambayo ikiwa pamoja na kituo cha uzalishaji umeme cha Jili cha Sudan, vitaunda sehemu muhimu ya mfumo wa umeme wa Sudan katika siku za baadaye. Baada ya ujenzi wa miradi hiyo miwili ya umeme kukamilika, Sudan itakuwa na uwezo wa kuuza umeme kwa nchi jirani.

Hivi sasa wafanyakazi 3,500 wa China wa kampuni ya ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme ya Harbin wanashiriki kwenye ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Jili na ujenzi wa boma la Marwi nchini Sudan, mhandisi wa umeme Bw. Wei Yong alifika Sudan kufanya kazi mwaka 2000, ambapo alifunga ndoa muda mfupi kabla ya hapo, mwanzoni hakuzoea mazingira ya nchini Sudan.

Mwanzoni baada ya kufika Sudan, sikuzoea mazingira tofauti ya kijiografia, hali ya hewa na utamaduni ya Sudan, tena mazingira ya maisha yetu yalikuwa magumu, hatukuwa na viyoyozi, mboga za kutosha na maji safi ya kunywa, na nilishidwa kulala vizuri."

Bw. Wei Yong alifanya kazi kwa miaka minane nchini Sudan, alisema, mazingira magumu yalimfanya aone kuwa, kazi zake ni muhimu, na kufahamu kuwa, kuisaidia nchi hiyo maskini ya Afrika ni jukumu lake la fahari. Alisema nchini Sudan aliona wasudan ni watu wema, ambao wanafanya urafiki na watu wa China. Mfanyakazi wa Sudan Bw. Ali Muhammad aliyefanya kazi pamoja na wafanyakazi wa China, alisema,

"Mimi ni mmoja wa wasudan waliofanya kazi mapema zaidi katika kampuni ya China. Ninaipenda sana kampuni hiyo, na nimekuwa na uzoefu mkubwa. Ni rahisi kufanya kazi kwa mapatano na wachina, mimi sijafanya kazi katika kampuni moja tu ya China, nimewahi kufanya kazi katika kampuni nyingine ya China kabla ya miaka mitatu iliyopita. Bila shaka kituo cha kuzalisha umeme cha Jili kitatoa mchango mkubwa kwa ongezeko la umeme nchini Sudan, na kwa maendeleo ya uchumi wa Sudan."

Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kipindi cha kwanza cha kituo cha uzalishaji umeme cha Jili, upungufu wa umeme kwenye mji mkuu wa Khartoum utapungua, tena uchumi wa Sudan utapata maendeleo ya kasi, serikali ya Sudan imekadiria kuwa, mwaka huu pato la nchini la Sudan litakuwa na ongezeko la 13%.

Konsela wa mambo ya uchumi katika ofisi ya ubalozi wa China nchini Sudan Bw. Hao Hongshe alisema, mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa na kampuni ya Harbin nchini Sudan utahimiza maendeleo ya uchumi wa Sudan. Aliongeza kuwa kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kilowati milioni 1.04, kwa hiyo kituo hicho ni kituo kikubwa cha uzalishaji umeme nchini Sudan.

Idhaa ya Kiswahili 2007-05-14