Mkutano wa 60 wa afya duniani ulifunguliwa tarehe 14 Asubuhi kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva barani Ulaya, na pendekezo lililotolewa na nchi chache kuhusu kuiruhusu Taiwan kuwa nchi mwanachama wa Shirika la afya duniani WHO siku hiyo lilikataliwa kwenye mkutano huo, na pendekezo hilo halijawekwa kwenye ajenda ya muda ya mkutano huo, na hii ni mara ya 11 kwa mkutano huo kukataa pendekezo kuhusu suala la Taiwan.
Mkutano wa 60 wa afya duniani siku hiyo asubuhi ulifanya mkutano usio wa wazi wa Kamati ya mambo ya jumla baada ya sherehe ya ufunguzi. Kamati hiyo ilitoa pendekezo la kufuta pendekezo kuhusu suala la Taiwan kutoka kwenye ajenda ya muda, na mkutano wa pili wa wajumbe wote uliofanyika siku hiyo mchana ulifanya majadiliano kuhusu pendekezo hilo lililotolewa na kamati ya mambo ya jumla.
Kwenye mkutano huo, nchi mbili zilizounga mkono pendekezo hilo na nyingine mbili zinazopinga pendekezo hilo zilieleza misimamo yao. Akiwa mjumbe anayeunga mkono kufuta pendekezo linalohusu Taiwan, waziri wa afya wa Pakistan Bw. Mohammad Nasir Khan alieleza msimamo wa Pakistan akisema:
"Pendekezo lolote kuhusu kuiruhusu Taiwan kujiunga na Shirika la afya duniani halina msingi wa kisheria, na linapingana na kanuni inayokubalika kwa jumuiya ya kimataifa, kitendo ambacho pia kinakwenda kinyume na Katiba ya Umoja wa Mataifa."
Bw. Mohammad Nasir Khan pia anaona kuwa Shirika la afya duniani linapaswa kuweka mkazo zaidi katika kufuatilia masuala muhimu likiwemo suala la afya duniani, wala si kujihusisha na jaribio kama hilo la Taiwan lenye kusudio la kisiasa ambalo halihusu mambo ya afya. Alisema:
"Mkutano wa afya duniani unalazimishwa mara kwa mara kujadili suala la Taiwan, kitendo ambacho si sahihi, kwani hadhi ya Taiwan ilithibitishwa katika zaidi ya miaka 30 iliyopita, na kanuni zinazohusika zimewekwa kwenye azimio la Umoja wa Mataifa na Shirika la afya duniani."
Kiongozi wa ujumbe wa China ambaye pia ni waziri wa afya Bw. Gao Qiang alieleza bayana kuwa, hatua hiyo ya utawala wa Taiwan siyo kwa ajili ya afya ya watu wa Taiwan, bali inatokana na kusudio la kisiasa. Alisema:
"Pendekezo hilo limefichua uongo wa utawala wa Taiwan wa kulinda afya ya watu, na kufichua kusudi lake la kisiasa la kuifarakanisha China. Pendekezo hilo halifuatilii maisha ya wakazi wa Taiwan, bali linajaribu kutafuta kujitenga kwa Taiwan, ili kuwatumikia mwanasiasa fulani wa Taiwan kwenye kampeni yake ya uchaguzi."
Bw. Gao Qiang pia alieleza ufuatiliaji wake kuhusu afya ya umma ya Taiwan. Alisema:
"Serikali ya China siku zote inafuatilia afya ya watu wa Taiwan, na inapenda kulinda haki na maslahi ya afya ya watu wa Taiwan kadiri iwezekanavyo. Serikali ya China itafanya juhudi zote kufanya shughuli zitakazosaidia mambo ya afya ya Taiwan, na kuhimiza mawasiliano kati ya kando mbili za mlango bahari wa Taiwan. Hayo si maneno tu, tumefanya vitendo halisi."
Baada ya majadiliano hayo, Mkutano huo ulifanya upigaji kura kuhusu pendekezo la Kamati ya mambo ya jumla ya kufuta kwa pendekezo linalohusu Taiwan.
"Korea ya Kusini, kura ya ndio. Jamhuri ya Moldova, kura ya ndio. Romania, kura ya ndio. Russia, kura ya ndio, Rwanda ..."
Baada ya kupiga kura, mwenyekiti mpya wa Mkutano wa 60 wa afya duniani ambaye pia ni waziri wa afya wa Australia Bi Jane Halton alitangaza matokeo, akisema:
"Kura za ndio ni 148, kura za hapana ni 17, watu 165 walifanya upigaji kura, pendekezo linalopitishwa linahitaji kupata kura 83, hivyo pendekezo hilo limepitishwa kwa zaidi ya nusu ya kura zote!"
|