Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-16 16:30:53    
Mapishi ya uyoga mweusi na kiazi kitamu

cri

Mahitaji:

Kiazi kitamu kimoja, uyoga mweusi gramu 100, nyama ya ng'ombe gramu 50, sukari kijiko kimoja, chumvi vijiko viwili,chembechembe cha kukolea kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, wanga kijiko kimoja

Njia:

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, koroga pamoja na chumvi, mvinyo wa kupikia na wanga.

2. weka uyoga mweusi kwenye maji, ondoa mizizi wake. Halafu ukata uwe vipande.

3. ondoa gamba la kiazi kitamu, halafu ukikate kiwe vipande.

4. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe joto la nyuzi ya 60, tia vipande vya nyama ya ng'ombe kwenye sufuria, korogakoroga, ipakue. Washa moto tena, tia vipande vya kiazi kitamu, uyoga mweusi, nyama ya ng'ombe, koroagkoroga, tia chumvi, sukari na chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.