Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-18 21:25:17    
Tolyatti- Rais Putin asisitiza kuwa Russia na Umoja wa Ulaya kutatua masuala ya pande mbili na ya kimataifa kwa njia ya mazungumzo

cri

Rais Vladimir Putin wa Russia tarehe 18 huko Tolyatti, kusini mwa nchi hiyo amesema, Russia na Umoja wa Ulaya zitashughulikia kutafuta njia inayokubalika kwa pande zote kutatua masuala yaliyopo ya pande mbili na ya kimataifa. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya kumaliza kwa mkutano wa 19 wa wakuu kati ya Russia na Umoja wa Ulaya amesema, mkutano huo wa wakuu umeeleza tena kupenda kufanya mazungumzo ya kiujenzi, na kuweza kupata ufumbuzi unaokubalika kwa pande zote.

Chansela wa Ujerumani ambaye ni mwenyekiti wa zamu ya hivi sasa ya Umoja wa Ulaya Bi. Angela Merkel amesema mkutano huo umeonesha kuwa Russia na Umoja wa Ulaya si kama tu zinadumisha ushirikiano katika masuala mbalimbali, bali pia zinapanua ushirikiano kati yao katika sekta mbalimbali.